Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,174
- 25,446
Kitendo cha kuwabaini 'wasaliti' ndani ya vyama vya siasa ni kitendo kikubwa. Ni ukweli kuwa kikulacho ki nguoni mwako. Lakini,kujua kuwa kikulacho kiko sehemu gani ya nguo ni jambo la mfano. Kumjua unayekula,unayelala,unayekunywa na unayeishi naye kuwa si mwenzio si mchezo.
Kuanzia mwaka 2013,CHADEMA ilijitikisa na kujisafisha. Wengine huita kujivua gamba. Iliwabaini wasio waaminifu chamani mwao na kuwashughulikia kinidhamu. Waliokumbwa na mtikiso huo ni Zitto Kabwe,Prof. Kitila Mkumbo,Samson Mwigamba, Alberto Msando,Juliana Shonza na Mtela Mwampamba,kutaja wachache.
Kufikia sasa,pamoja na propaganda na maneno yote ya wakati huo,wote hao ni wanachama wa CCM isipokuwa Zitto ambaye ni Kiongozi wa ACT Wazalendo. Wote sasa ni wapinzani wa waziwazi wa CHADEMA. Baada ya kubainika,sasa ni dhahiri.
Mara tu baada ya kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa BAVICHA Taifa,Patrobas Katambi naye 'akashtukiwa' kuwa hayupo kichama. Akawa anapewa taarifa na kushirikishwa kwa mipaka. Akawa 'anatengwa'. Leo,amejiunga na CCM.
Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni. Intelijensia ya CHADEMA is super and unique. Inaona mbali kwa darubini kali!