Ukweli uliopo katika kutafuta utajiri

Umomi

JF-Expert Member
Mar 31, 2020
677
983
USISUMBUE AKILI YAKO KWA MANENO YA KUAMBIWA KITU FLANI KINALIPA:

KWA MFANO:

Ukipata nafasi ya kufika kule *Mbozi, Mbeya* ukakutana na habari za watu wanaotajirika kutokana na *kilimo cha kahawa*, kwa kweli unaweza kuwehuka, na kujiona kama mtu uliyechelewa kweli kweli.

Wakati unarudi, kama ukishuka Mafinga, Njombe na kufuatilia stori na kutazama mamilionea walioupata umilionea kutokana na biashara ya miti na mbao, unaweza kudhani kwamba hapa duniani fursa inayowatoa watu kiuharaka ni mbao pekee!

Pitia maeneo ya Ruaha Mbuyuni, Iringa kutana na wakulima wa nyanya na vitunguu wakikuonesha Coaster walizonunua kwa kilimo cha msimu mmoja pekee. Aisee kama una akiba utanunua shamba muda huo huo na kuachana na ajira, kama ulikuwa mwajiriwa.

Ukitoka pale ukaenda mpaka *Mang'ula na Ifakara Morogoro,* ukakutana na habari za watu wanavyopiga hela kwenye *mpunga*, kichwa chako kinaweza kuwaka moto. Unaweza kujizaba vibao na kujimaindi, afu utajiuliza, "Nilikua wapi siku zote hizi?"

Ukitoka kule jisogeze mdogo mdogo hadi *Kariakoo, Dsm* kisha kutana na wafanyabiashara wa maduka pale ambao wana gepu la kufuata bidhaa kule China, Uingereza na Dubai. Utapigwa na butwaa utakapoona watu wakiongelea milioni mia tatu, milioni mia saba, bilioni mbili kama vile wanaongelea elfu kumi kumi. Usipokua na utulivu unaweza kuamini kwamba biashara zinazolipa ni maduka na unaweza kuanza kupambana kupata fremu pale!

Usiende kwanza Zanzibar, bali chukua hata bus au Fastjet uende chapchap kule *Arusha*. Hapo utakutana na stori za mabilionea wa madini wanaotikisa jiji. Ukisimuliwa ABC za madini na namna ya kucheza nayo, unaweza kuacha kila kitu na kuanza kuhangaika na biashara ya madini. Hapo sijakutajia jeuri utakayoiona kwa watu wanaofanya biashara ya utalii. Nakwambia hela ulizozisikia Kariakoo utaziona ni cha mtoto sana kabisa!

Unapoendelea kutafakari, rudi mtandaoni. Kama ukibahatika kukutana na watu wanaoitwa *Network Marketing* utakoma kuchagua. Wakikuelezea stori zao, wakikusimulia walivyonunua ma-Range Rover Vouge yao, wakikuonesha picha zao walizokua wanakula bata *Dubai, Paris, Mauritius na Disneyland - Marekani*, nakwambia korosho utaziona takataka.

Mbao utazihesabu kama biashara ya utumwa, maduka ya Kariakoo utayaona kama michosho na mpunga wa Ifakara utaiona kama madudu flani ya walugaluga waliochelewa! Sasa mara kumi hata ya Network Marketing wa bidhaa, usiombe ukutane na fursa ya digital currency, hakika nakwambia utatembea kifua mbele ukiamini kutajirika ni ishu ya kufumba na kufumbua.

Hapo sijaamua kusafiri na wewe kwenda kwa wale tunaokinadi kilimo kama dhahabu inayoelea. Ukisikiliza wafuasi wa kilimo, ukasikiliza hesabu wanazokupatia unaweza kusema wanaohangaika na madini wanapoteza muda! Ngoja niuchune nikupeleke kwenye fursa ya samaki kuzitoa Mwanza kupeleka DR-Kongo, ngoja nisikurushe roho na habari ya korosho, ngoja nikaushie habari ya ufuta!

KUNA MAMBO MATANO YA KUFAHAMU:-

1.
Usipokua na utulivu wa fikra, hizi habari za fursa za biashara na ujasiriamali zinaweza kugeuka kuwa kama miluzi mingi, na itakupoteza.

2. Mtu yeyote asikudanganye ya kwamba kuna biashara bora kuliko nyingine. Kila biashara, fursa unayoiona huku duniani inao uwezo wa kutengeneza matajiri. Kuna matajiri kutokana na kumiliki shule, wengine kwa kumiliki mabasi, wengine kwa kuwa na vituo vya mafuta, wengine kwa kilimo, wengine kwa udalali n.k. Usisahau kuwa biashara inayomtajirisha mmoja, mwingine akiingia ndio inaweza kumfilisi na kumpoteza kabisa! Kawaulize waliolizwa kwenye kilimo, watakusimulia.

3. Mtu yeyote asikuchanganye na miluzi yake hata ukaamini kwamba kuna fursa inayoweza kumfaa kila mtu. Sio kila fursa inayompa faida John inaweza kukupa faida wewe Juma. Ukifuatilia kwa umakini utabaini kwamba mafanikio hayakai katika uzuri wa fursa, bali yanatokana na mchukua fursa. Mwingine anaweza kujifunza na kumudu kuifanya network
marketing, lakini mwingine nature ya network marketing haimfai, isipokua akienda kule Mafinga akazamia kwenye mbao, mwaka mmoja mbali, utaona ana Semitrela zake mbili na mambo yanaenda.

Kuna watu wanapotea kiuchumi kwa kung'ang'ana na fursa kwa kukariri. Kisa kuna mtu alinunua Range Rover-Vogue katika network marketing na wewe unaendelea kukomaa, mwaka wa tano sasa hata bodaboda huna, kumbe ungeenda zako Mbozi kwenye kahawa sasa hivi usikute na nyumba ungekua umeshajenga. Kisa wanaoenda China wanatoka na wewe unahangaika na biashara za maduka, mwaka wa ishirini bado hakujasomeka na kumbe ungeenda zako kwenye madini huko Mererani muda huu ungekua umeshanunua helkopta yako!

4. Ni kweli kwamba inatakiwa tujifunze fursa mbalimbali, lakini ifike sehemu mtu uchague kukomaa na fursa fulani pasipo kurukaruka. Utajiri hauji kwa mtu kuwa bize na kila fursa inayoingia, bali unakuja kwa kujifunza fursa nyingi na ku-stick na eneo moja, ama maeneo machache ambayo, utajitambulisha nayo na watu watakutambua. Na ukishakua katika kukomaa na maeneo yako (fursa ulizoamua kukomaa nazo), usianze tena kuyumbayumba na kutamani ya wengine.

5.
Lazima ifike mahali utambue kwamba kila mtu anahitaji fedha za kutosha lakini hatuhitaji kiwango sawa cha fedha kwa sababu makusudi na malengo yetu hayafanani. Nikisema hivi, sikushauri uhangaike na fursa kwa motive ya hela pekee, bali ufanye vitu kama sehemu ya kuufurahia mchakato wa kazi; na fedha ziwe ni matokeo na sio lengo namba moja

Fursa zipo nyingi kuwa makini katika maamuzi.
 
5. Lazima ifike mahali utambue kwamba kila mtu anahitaji fedha za kutosha lakini hatuhitaji kiwango sawa cha fedha kwa sababu makusudi na malengo yetu hayafanani. Nikisema hivi, sikushauri uhangaike na fursa kwa motive ya hela pekee, bali ufanye vitu kama sehemu ya kuufurahia mchakato wa kazi; na fedha ziwe ni matokeo na sio lengo namba moja

Fursa zipo nyingi kuwa makini katika maamuzi.

Niwahi seat ya mbele tena dirishani kabisaaa
 
USISUMBUE AKILI YAKO KWA MANENO YA KUAMBIWA KITU FLANI KINALIPA:

KWA MFANO:

Ukipata nafasi ya kufika kule Mbozi, Mbeya ukakutana na habari za watu wanaotajirika kutokana na kilimo cha kahawa, kwa kweli unaweza kuwehuka, na kujiona kama mtu uliyechelewa kweli kweli.

Wakati unarudi, kama ukishuka Mafinga, Njombe na kufuatilia stori na kutazama mamilionea walioupata umilionea kutokana na biashara ya miti na mbao, unaweza kudhani kwamba hapa duniani fursa inayowatoa watu kiuharaka ni mbao pekee!

Pitia maeneo ya Ruaha Mbuyuni, Iringa kutana na wakulima wa nyanya na vitunguu wakikuonesha Coaster walizonunua kwa kilimo cha msimu mmoja pekee. Aisee kama una akiba utanunua shamba muda huo huo na kuachana na ajira, kama ulikuwa mwajiriwa.

Ukitoka pale ukaenda mpaka Mang'ula na Ifakara Morogoro, ukakutana na habari za watu wanavyopiga hela kwenye mpunga, kichwa chako kinaweza kuwaka moto. Unaweza kujizaba vibao na kujimaindi, afu utajiuliza, "Nilikua wapi siku zote hizi?"

Ukitoka kule jisogeze mdogo mdogo hadi Kariakoo, Dsm kisha kutana na wafanyabiashara wa maduka pale ambao wana gepu la kufuata bidhaa kule China, Uingereza na Dubai. Utapigwa na butwaa utakapoona watu wakiongelea milioni mia tatu, milioni mia saba, bilioni mbili kama vile wanaongelea elfu kumi kumi. Usipokua na utulivu unaweza kuamini kwamba biashara zinazolipa ni maduka na unaweza kuanza kupambana kupata fremu pale!

Usiende kwanza Zanzibar, bali chukua hata bus au Fastjet uende chapchap kule Arusha. Hapo utakutana na stori za mabilionea wa madini wanaotikisa jiji. Ukisimuliwa ABC za madini na namna ya kucheza nayo, unaweza kuacha kila kitu na kuanza kuhangaika na biashara ya madini. Hapo sijakutajia jeuri utakayoiona kwa watu wanaofanya biashara ya utalii. Nakwambia hela ulizozisikia Kariakoo utaziona ni cha mtoto sana kabisa!

Unapoendelea kutafakari, rudi mtandaoni. Kama ukibahatika kukutana na watu wanaoitwa Network Marketing utakoma kuchagua. Wakikuelezea stori zao, wakikusimulia walivyonunua ma-Range Rover Vouge yao, wakikuonesha picha zao walizokua wanakula bata Dubai, Paris, Mauritius na Disneyland - Marekani, nakwambia korosho utaziona takataka.

Mbao utazihesabu kama biashara ya utumwa, maduka ya Kariakoo utayaona kama michosho na mpunga wa Ifakara utaiona kama madudu flani ya walugaluga waliochelewa! Sasa mara kumi hata ya Network Marketing wa bidhaa, usiombe ukutane na fursa ya digital currency, hakika nakwambia utatembea kifua mbele ukiamini kutajirika ni ishu ya kufumba na kufumbua.

Hapo sijaamua kusafiri na wewe kwenda kwa wale tunaokinadi kilimo kama dhahabu inayoelea. Ukisikiliza wafuasi wa kilimo, ukasikiliza hesabu wanazokupatia unaweza kusema wanaohangaika na madini wanapoteza muda! Ngoja niuchune nikupeleke kwenye fursa ya samaki kuzitoa Mwanza kupeleka DR-Kongo, ngoja nisikurushe roho na habari ya korosho, ngoja nikaushie habari ya ufuta!

KUNA MAMBO MATANO YA KUFAHAMU:-

1.
Usipokua na utulivu wa fikra, hizi habari za fursa za biashara na ujasiriamali zinaweza kugeuka kuwa kama miluzi mingi, na itakupoteza.

2. Mtu yeyote asikudanganye ya kwamba kuna biashara bora kuliko nyingine. Kila biashara, fursa unayoiona huku duniani inao uwezo wa kutengeneza matajiri. Kuna matajiri kutokana na kumiliki shule, wengine kwa kumiliki mabasi, wengine kwa kuwa na vituo vya mafuta, wengine kwa kilimo, wengine kwa udalali n.k. Usisahau kuwa biashara inayomtajirisha mmoja, mwingine akiingia ndio inaweza kumfilisi na kumpoteza kabisa! Kawaulize waliolizwa kwenye kilimo, watakusimulia.

3. Mtu yeyote asikuchanganye na miluzi yake hata ukaamini kwamba kuna fursa inayoweza kumfaa kila mtu. Sio kila fursa inayompa faida John inaweza kukupa faida wewe Juma. Ukifuatilia kwa umakini utabaini kwamba mafanikio hayakai katika uzuri wa fursa, bali yanatokana na mchukua fursa. Mwingine anaweza kujifunza na kumudu kuifanya network
marketing, lakini mwingine nature ya network marketing haimfai, isipokua akienda kule Mafinga akazamia kwenye mbao, mwaka mmoja mbali, utaona ana Semitrela zake mbili na mambo yanaenda.

Kuna watu wanapotea kiuchumi kwa kung'ang'ana na fursa kwa kukariri. Kisa kuna mtu alinunua Range Rover-Vogue katika network marketing na wewe unaendelea kukomaa, mwaka wa tano sasa hata bodaboda huna, kumbe ungeenda zako Mbozi kwenye kahawa sasa hivi usikute na nyumba ungekua umeshajenga. Kisa wanaoenda China wanatoka na wewe unahangaika na biashara za maduka, mwaka wa ishirini bado hakujasomeka na kumbe ungeenda zako kwenye madini huko Mererani muda huu ungekua umeshanunua helkopta yako!

4. Ni kweli kwamba inatakiwa tujifunze fursa mbalimbali, lakini ifike sehemu mtu uchague kukomaa na fursa fulani pasipo kurukaruka. Utajiri hauji kwa mtu kuwa bize na kila fursa inayoingia, bali unakuja kwa kujifunza fursa nyingi na ku-stick na eneo moja, ama maeneo machache ambayo, utajitambulisha nayo na watu watakutambua. Na ukishakua katika kukomaa na maeneo yako (fursa ulizoamua kukomaa nazo), usianze tena kuyumbayumba na kutamani ya wengine.

5.
Lazima ifike mahali utambue kwamba kila mtu anahitaji fedha za kutosha lakini hatuhitaji kiwango sawa cha fedha kwa sababu makusudi na malengo yetu hayafanani. Nikisema hivi, sikushauri uhangaike na fursa kwa motive ya hela pekee, bali ufanye vitu kama sehemu ya kuufurahia mchakato wa kazi; na fedha ziwe ni matokeo na sio lengo namba moja

Fursa zipo nyingi kuwa makini katika maamuzi.

Dah Nimekubali sana Hii ni zaidi ya Nondo.
 
Back
Top Bottom