Ukweli uliofichwa sasa umefunuliwa, ni kuhusu T. B Joshua

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,632
697,794
Nimechukua muda wa kutosha kusoma kitabu kinachotoboa siri za utapeli wa TB Joshua kinachoitwa "The TB Joshua I Know-Deception of the Age Unmasked" kilichoandikwa na Bi. Hephzibah Bisola Johnson ambaye alikuwa mtumishi wake wa karibu sana kwa muda wa miaka 14.

Infact Bisola alikuwa right-hand person wake aliyekwenda naye kila mahali. Pia nimesikiliza video clips 32 zinazomhusu TB Joshua; nimesoma articles mbalimbali zinazohusu sakata hili; nimesikiliza mahojiano mbalimbali ya watu waliotajwa kwenye kitabu cha Bi Bisola Johnson; nimefuatilia Tweets na page zao za social media; nimesoma maelezo ya watoto wa marehemu waliokufa au kupotea wakiwa ndani ya Sinagogi la TB Joshua bila ndugu kupata maelezo ya kueleweka; nimesikiliza maelezo ya watu maarufu wakiwemo wacheza mpira na wacheza filamu waliowahi kutekwa na uongo wa TB Joshua na kisha kujikuta wakimpa fedha nyingi bila sababu yoyote. Wacheza mpira waliotajwa ni pamoja na Nwankwo Kanu aliyewahi kuichezea timu ya Arsenal na Emmanuel Amunike aliyekuwa kocha wa Timu yetu ya Taifa Stars.

Nimefuatilia pia taarifa zinazohusu kesi zinazomkabili TB Joshua Afrika Kusini zilizofunguliwa na wazazi wa mabinti wadogo waliopelekwa kwake kwaajili ya kuombewa na kisha kufanya nao mapenzi; Nimefuatilia comments na maandiko ya watu wanaomtetea; Nikarudi pia kutazama clip za mahubiri na uponyaji katika Sinagogi lake; n.k, n.k. Ili kujumuisha naomba niseme yafuatayo:

1. Anaendelea kuamini kuwa TB Joshua ni Nabii wa kweli. Na kwamba anafanya miujiza ya kweli, basi ajue anafanya hivyo at his or her own risk! Kama ulienda kwake ukapona, basi ujue ni imani yako tu... siyo TB Joshua. Endelea kumuamini Mungu wako aliyekuponya.

2. Zile kauli za 'wametumwa wamchafue..' hapa hazina mashiko hivyo usikimbilie kijifunika na blanketi hilo.. Tulia. Omba hekima ya Mungu. Kumbuka Hypnosis (yaani kupumbazwa) is real.

2. Kama una maji yake, sticker, mafuta, au chochote chake, ni afadhali utupe tu. Inawezekana unaendelea kujiunganisha na roho usizozijua.

3. Nawashauri wakristu wenzangu tuache kupenda miujiza kupita kiasi hadi kufikia kupumbazwa nayo. Tutulie, na kumtafuta Mungu katika Roho na Kweli. Siyo katika watu, miti, mapango, wala mahekalu...

Kwa anaetaka kusoma kitabu hicho kinapatikana Amazon.

The level of detail in this book is scary. Na mwandishi amesema yuko tayari kupelekwa mahakamani na TB Joshua kama aliyoyasema ni ya uongo. Bi Johnson ameanza kwa kuwataka radhi watu wote na kusema maneno haya: "Please forgive me oo. We did these atrocities together with him oo. I was part of it oo." Ila sasa ametubu na anaamini Yesu Kristo ameshamsamehe. Hivyo anawiwa kuwasaidia watu wengine wasiendelee kupotea.

Pia unaweza kusikiliza mahojiano youtube.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukielewa kuwa watu wanafanya vitu ili kutafuta hela na si bwana Nani sijui,hutajisumbua nao!!
Maisha ni halisi na watapigwa wengi maana akili ni Kama pira mpaka itanuke kisawasawa Kuna matokeo lzm uwe umepitia.. heri wanaopevuka mapema kiakili.
 
Ila ujasilia Mali wa kwenye dini na siasa ndio unaolipa zaidi duniani kwa sasa.

Tukitoka kazini tumepigika kweli kweli, ukifika nyumbani mama nanii naye kakuendea kwa sangoma kichwa kinawashwa moto, Biashara ulizoanzisha haziendi kwa kukosa usimamizi thabiti, ada ya watoto haijai wakati January inakaribia matokeo yake hizo stress unaenda kuziondolea kwa TB Joshua, huko hata ukiambiwa uuze nyumba na mali zako zote halafu upeleke hela yote ikaombewe ni Ndiyo tu matokeo yake tunazidi kujaza vichaa tu mijini.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kiukweli kabisaa toka moyoni mwangu sijawahi muamini yule jamaa, kwenye Tv huwa napita kama simuon, kuna siku i think mwanang alinambia mama kwann hupendi kumsikiliza nkamwambia sina Iman nae tu na si kingine.

Na sio yeye tu karibia wote wanaojiita manabii sijawahi kuwaamini sijui kwann. Kuna wakat nliumwa sana sanaa na tumbo jiran yang mmoja akanambia twende mahali nkupeleke na kama nlifungwa ufaham sikuuliza wapi. Mara paap kanisani nkamuuliza kanisa gani hili akanitajia jina, anyway sabab nlishafika nkasema wacha niingie.

Toka tumeingia kanisan ni shuhuda za watu kufanikiwa tuuu mara nlkuwa na gar moja baada ya kuombewa nkapata tano
Mara sijui nn nkasema ayaa sasa hapa Mbingun tunaenda kwa magari au nyumba? Hawahubir neno la Mungu
Hawahubir watu waijue kweli ya Mungu na kuacha yasiyompendeza wao n mafanikio tu. Nkasema daah Mungu okoa kizaz hiki.

Ikafika muda wa kuombewa akanambia nenda mbele nkamwambia hapana mimi nakaa hapa hapa. Oho ajab nyingine nlioona watu wanasimama nyuma ya mtu anayeombewa unaguswa kwa kusukumwa nyuma halaf wale wanakudaka.

Kiukwel nlijionea mengi nkasema hapana ngoja nibaki na dini yangu mama KKKT inanitosha. Nawaangaliaga watu weee
Nasema anyway kila mtu na Imani yake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naweza kukubaliana na wewe japo mie pia ndo wale wanaopiga magoti na kunyoosha mkono kwenye Emmanuel TV.

Ninachoweza kukubaliana nawe ni hivi, miaka kama nane hivi niliwahi onana uso kwa uso na brother mmoja aliyekuwa on the way kwenda huko Sinagogi na nikampa baadhi ya mahitaji yangu kimaandishi. Hakuna kilichobadilika.

Kilichoniacha hoi ni pale lile Sinagogi lilipofunika watu na mambo yakapita kama upepo.

Huwa sielewi.

Kuhusu kuponya, Mungu anaweza kukuponya baada ya kuona imani yako kwake na wakati mwingine Mungu hapendi mtu ahangaike zaidi.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
You are right blaza, yuko mmoja hapa TZ, sijui mzee wa nini vile. Kwanza ni mlevi hatari, kavunja ndoa ya mtu kwa kutumia nguvu za giza na mme akafa kimazingira. Huyo mwanamke sasa ni kama mkewe kabisa japo ni mambo ya (gizani) kiwiziwizi. Mkewe halisi ndo kama zuzu japo ukimuona yuko fresh, akisafiri nje yuko na huyo kimada mama wa watoto 2 wa kiume, ni hatari. Hapo bado kondooo wanaochinjwa kimya kimya.

Mungu tunaomba huruma yako ituimarishe kiroho.
 
Back
Top Bottom