Ukweli ulio mchungu: Kuna mstari mwembamba sana unaotenganisha kati ya utajiri wa mali na neno 'ubinafsi'

FAJES

JF-Expert Member
Oct 29, 2017
715
627
Wanabodi heshima kwenu.

Naomba nijielekeze moja kwa moja kwenye mada.

Kwanza kabisa niwashukuru sana wadau wote waliochangia kwenye uzi wangu huu uliopita, ukipenda unaweza kusoma hapa. Baada ya kusoma comments zote za wadau kwenye uzi huu na kufanya tafakuri ya kina, nimebaini na kujifunza mambo machache yafuatayo .

Kuna mstari mwembaba sana unaotofautisha kati ya utajiri wa mali na ubinafsi. Neno utajiri wa mali sina haja ya kulitolea ufafanuzi wake maana ni kitu kinachofahamika kwa walio wengi. Ila naomba niazime tafsiri ya neno 'Ubinafsi' kutoka kwenye mtandao wa wikipedia. Wanasema, Ubinafsi ni 'tabia ya kujipendea mno hata kutojali wengine na shida zao'. Unaweza kusoma mwenyewe kwa link hii (Ubinafsi). Comments za wadau zimedhihirisha pasi na shaka kwamba, ili uweze kutoboa kwenye haya maisha, yaani kwamba uweze kumiliki mali nyingi inabidi kwanza uwe mbinafsi. Maana yake ni kuwa ujijali zaidi wewe mwenyewe ikiwemo labda wazazi na mke/mme na watoto pekee bila kutazama shida za watu wengine wanaokuzunguka.

Kwa ufafanuzi zaidi ni kuwa, haijalishi jirani au ndugu yako ana shida kiasi gani, ila usijaribu kabisa kuendekeza shida za watu wengine maana utaishia kuwa maskini kwakuwa shida za watu hutazimaliza hapa duniani. Kama ni kusaidia labda usaidie kwa watu wachache sana na mara chache mno. Kiufupi usiendekeze kabisa shida za watu wengine kwenye maisha yako. Na awengine wakaenda mbali zaidi kwa kusema ikiwezekana kwenye masuala ya kiutafutaji usiishi karibu na ndugu zako. Uende ukaishi eneo lingine mbali ili kupunguza kabisa mazoea ya kuombana misaada.

Jambo hili limenisukuma kudhani ya kuwa hali hii ya kujipenda mwenyewe kwa sisi Wafuasi wa Ukristo huenda ikawa tofauti na imani hii maana kwenye Ukristo tunafundishwa kumpenda jirani yako kama unavyoipenda nafsi yako. Najua wadau wengine wanaweza kusema mie ndio sifahamu tafsiri ya maandiko hayo ila katika hali ya kawaida maandiko hayo yanamanisha kumpenda jirani ama mtu mwingine aliye karibu yako kama unavyojipenda wewe mwenyewe. Ikimaanisha kuwa ukimpenda jirani yako hutamuacha alale njaa na wala hutamuacha afariki kwa kukosa matibabu kwa kisingizio cha utafutaji wa mali na kujikusanyia mali nyingi hapa Duniani.

Kwa upande mwingiine, ni ukweli usiopingika kuwa watu wengi waliofanikiwa kwenye utafutaji waliamua 'ubahili' na kujijali wao zaidi iwe sehemu ya maisha yao. Ukiwa mtoaji sana kwenye utafutaji utaishia kuwa mtu wa kawaida na huenda ikapelekea kufilisika na hao uliowasaidia wasikukumbuke utakapokuwa umeanguka chini.

Any way, naomba nisieleweke kuwa huenda hoja yangu imejikita kwenye masuala ya imani, ila kwa kuhitimisha ni kuwa, ili utoboe kwenye haya maisha kiufupi, inabidi uwe mbinafsi sana. Sasa kama ubinafsi ni hali inayoenda kinyume na imani zetu hilo ni jambo lingine ambalo linahitaji jicho la kitaalamu kiimani ila naomba kuishia hapo kwa sasa.
 
Japo umeandika ubinafsi ila siyo ubinafsi kama ubinafsi ni ubepari au watu kujizoeza kuandaa njia za kutatua matatizo yao wenyewe bila kutegemea wengine, unajua wengi wanaamini ujamaa na wakautumia kama kisingizio cha kutaka watu wengine wawajibike kwaajili yao, imagine mtu anashindwa kuweka mpango wa mbele wa maisha yake na mwingine akaweka mpango wa mbele wa maisha yake kiasi cha kujinyima mambo mengi Ili mambo yake yafanikiwe lakini yule asiyejinyima na huku anapenda mwingine amubebea majukumu yake au ajinyime kwa ajili yake ndo huyo anapenda vya Bure au kupewapewa tu na kuishi kwa kutegemea jasho la mwingine au vitu vya watu wengine ikitokea yule anategemewa kugawa hovyo vitu vyake akawa mjanja na kukwepa huo mtego mara nyingi huwa kunaleta mafanikio.
 
Ni daraja, narudia tena ni DARAJA.

Kwenye uzurulaji wako kama ushawahi kutana na kitu kinaitwa Philanthropy, hii inahusisha hali ya kutoa kilichozidi kwa wengine, hapa ndio tunakutana na foundations kama za kina Mo au TonyElumelu au akina Billy and Melinda (Kwenye hili daraja hapa hakuna uzi hata huo mwembaba mkuu).

Halafu kuna hili daraja la kina (Mtoto wa kike apate pedi bure ili asikatishe masomo yake) , (Upasuaji kwa watoto waliozaliwa na mgongo wazi na mdomo sungura) na (Kimbia marathon kuchangia bima ya afya kwa watoto waishio mtaani) utoaji huu unawagusa pia hata ambao nao walipewa toka kwa wale wa kule juu

Halafu kuna wale ambao wanatengeneza sh.2000 (ELUFU MBILI TASLIMU) kwa siku ila wana familia inayotumia sh.2100 (ELUFU MBILI NA MIA MOJA) kwa siku na wala huwa hawanyimi , anapata wapi hiyo sh.100 ni yeye ndo anajua.

Anyway nilichotaka kusema ni kwamba kuna wanaojitoa kama mishumaa na wanaojitoa kama boya juu ya maji (kamwe hawazami).
 
Kwa maoni yangu, ishu kubwa kwenye kua tajiri au kutokua tajiri, haipo kwenye kiasi unachotoa, bali kwenye kiasi unacho ingiza.

Kama wewe kipato chako ni cha kuunga unga, hata usipompa mtu yoyote chochote, bado hautakua tajiri! Ila kama una mifereji ya maana inayomimina fedha, hata ungetoa pesa zako zote ukasaidia masikini, bado utakua tajiri tu.
 
Kwa maoni yangu, ishu kubwa kwenye kua tajiri au kutokua tajiri, haipo kwenye kiasi unachotoa, bali kwenye kiasi unacho ingiza.

Kama wewe kipato chako ni cha kuunga unga, hata usipompa mtu yoyote chochote, bado hautakua tajiri! Ila kama una mifereji ya maana inayomimina fedha, hata ungetoa pesa zako zote ukasaidia masikini, bado utakua tajiri tu.
Kweli mkuu. Nadhani mada hii itafaa zaidi kwa tulioko kwenye transition kutoka kwenye kipato cha kuunga unga kwenda kwenye sustainable and reliable cash flow..
 
Waliotuletea hiyo mistari ni Wabinfsi kuliko mistari yenyewe nadhani walileta kwa malengo yao binafsi hawakuumanisha walichokiandika.
 

Similar Discussions

5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom