Ukweli uko dhahiri shahiri, Rais Samia anagombea mwaka 2025

G4N

JF-Expert Member
Apr 6, 2014
763
1,000
Hapa unamzungumzia Magufuli, ambaye tayari hatunae!

Naona wewe unakwenda kwa mwendo wa kinyonga mkuu!
Hapana mkuu namzungumzia mama. Huyu mama kidemokrasia ni mbaya kuliko Magufuli.

Ameruhusu na kuachia mambo kadhaa qmbayo yatampa umaarufu na kukubalika zaidi. Lkn kimsingi anaminya Mambo muhimu ya kidemokrasia.

Hata Magufuli hakuwahi kumpa kesi ya ugaidi mpinzani wake. Huu tayari ni mkakati madhubuti wa kuawatisha wapinzani wake wa nje na ndani ya chama chake.
 
Daisam

JF-Expert Member
May 23, 2016
1,659
2,000
Mimi nadhani umefika wakati wale wasaidizi wake wa karibu wamwambie ukweli. Wasiendelee kumdanganya. Hali huku mtaani ni mbaya sana. Zaidi ya 95% ya Watanzania wakubwa kwa wadogo hawana imani naye hata kidogo.
JPM aliweka misingi imara sana na watu walimkubali mno.
Leo hii Watanzania wanapoona UOZO uliokuwepo kabla ya JPM na akaumaliza, UOZO ule ule umerudi kwa kasi ya ajabu. Watanzania wana hasira sana.
Ushauri wangu kwake ni kwamba, amalize miaka hii 4 iliyobaki, 2025 atafutwe mwingine. CCM wasifanye makosa kwenye hilo, watajuta.
 
Kalamu1

JF-Expert Member
Jul 7, 2018
11,307
2,000
Hapana mkuu namzungumzia mama. Huyu mama kidemokrasia ni mbaya kuliko Magufuli.

Ameruhusu na kuachia mambo kadhaa qmbayo yatampa umaarufu na kukubalika zaidi. Lkn kimsingi anaminya Mambo muhimu ya kidemokrasia.

Hata Magufuli hakuwahi kumpa kesi ya ugaidi mpinzani wake. Huu tayari ni mkakati madhubuti wa kuawatisha wapinzani wake wa nje na ndani ya chama chake.
Hii kesi inayomkabili Mbowe ni ya Magufuli; mama kaiokota na kuitumia bila kujua matokeo yake yatakuwa vipi, au akidhani ataitumia kujijengea sifa.
Badala yake mwisho wa kesi hii mama atabaki mikono mitupu na lawama juu yake.
Mama hawezi tena kuvitumia vyombo vya dola kama alivyovitumia Magufuli, hilo litampa hali ngumu zaidi ndani ya chama na nje wakati wa kinyang'anyiro 2025.
Naona kwa mara ya kwanza kabisa, 2025 uchaguzi ukifanyika katika hali tofauti sana na tuliyoizoea. Ujanja ujanja wa CCM hautakuwa na nafasi tena kama vyama vya upinzani watakuwa wamejipanga vizuri.

Mama akishinda uchaguzi huo, hakika nami nitampongeza kwa kufanya kazi nzuri ya kuwapa matumaini waTanzania juu ya uongozi wake. Kwa jinsi ninavyomwona hadi sasa, sioni hizo sifa za uongozi za kugeuza mioyo ya waTanzania ielekee upande wake.
 
G4N

JF-Expert Member
Apr 6, 2014
763
1,000
kama vyama vya upinzani watakuwa wamejipanga vizuri.
Unaposema "kujipanga vizuri" unamaanisha nini? Chaguzi zote nchi hii huvurugwa na tume, polisi na tiss. Sasa wapinzani wajipange ktk lipi?
 
Kalamu1

JF-Expert Member
Jul 7, 2018
11,307
2,000
Unaposema "kujipanga vizuri" unamaanisha nini? Chaguzi zote nchi hii huvurugwa na tume, polisi na tiss. Sasa wapinzani wajipange ktk lipi?
Hiyo ni historia mkuu, hakuna atakayeshiriki kwenye chaguzi katika mazingira hayo tena. Hivi huamini ninapokwambia hivyo?
 
Cheef Baroka

JF-Expert Member
Mar 24, 2020
491
1,000
Ndo kwanza ana miezi6 tu kwenye miaka 5 ashaanza kampeni!. Duh! Mwanamke Mwanamke tu. Naanza kuwaelewa marekani walokubari kumpa nchi mwehu kuliko mwanamke
 
Junior Nicky

JF-Expert Member
Jul 31, 2016
575
500
Hii kesi inayomkabili Mbowe ni ya Magufuli; mama kaiokota na kuitumia bila kujua matokeo yake yatakuwa vipi, au akidhani ataitumia kujijengea sifa.
Badala yake mwisho wa kesi hii mama atabaki mikono mitupu na lawama juu yake.
Mama hawezi tena kuvitumia vyombo vya dola kama alivyovitumia Magufuli, hilo litampa hali ngumu zaidi ndani ya chama na nje wakati wa kinyang'anyiro 2025.
Naona kwa mara ya kwanza kabisa, 2025 uchaguzi ukifanyika katika hali tofauti sana na tuliyoizoea. Ujanja ujanja wa CCM hautakuwa na nafasi tena kama vyama vya upinzani watakuwa wamejipanga vizuri.

Mama akishinda uchaguzi huo, hakika nami nitampongeza kwa kufanya kazi nzuri ya kuwapa matumaini waTanzania juu ya uongozi wake. Kwa jinsi ninavyomwona hadi sasa, sioni hizo sifa za uongozi za kugeuza mioyo ya waTanzania ielekee upande wake.
Mkuu vipi 2025 Katiba mpya na tume huru ya uchaguzi itakuwa imeshapatikana?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom