Ukweli uko dhahiri shahiri, Rais Samia anagombea mwaka 2025

Ojuolegbha

Member
Sep 6, 2020
22
75
KUELEKEA 2025, ROMA LOCUTA, CAUSA FINITA!

Na MariaMungu Charles

KATIKA karne ya tano ilitokea sintofahamu katika Kanisa Katoliki Jimbo la Hippo, eneo hilo leo linaitwa Annaba, nchini Algeria, lililokuwa likiongozwa na Mtakatifu Augustine. Mtafaruku huo umeacha alama na funzo kubwa kwa jamii yetu hata leo.

Katika mafundisho ya Kanisa na kwa mtazamo wa Mt. Augustine, ukamilifu wa mwanadamu unapatikana kwa Neema ya Mungu. Lakini wafuasi wa mtazamo wa mtawa wa Kiingereza Pelagius wakiitwa Pelagians wao walikuwa wakiamini kwamba mwanadamu anaweza kuwa mkamilifu wa umahili na uwezo wake tu bila kuhitaji neema ya Mungu.

Ili kuondokana na mkanganyiko huo mabaraza ya Milevi na Catrthage yalituma shauri hilo Roma, Makao Makuu ya Kanisa Katoliki, ili kupatiwa ufumbuzi wa mkanganyiko huo. Majibu toka Roma yaliporudi Mtakatifu Augustine aliwaeleza wafuasi wake kwamba baada ya shauri hilo kufika kwa Baba Mtakatifu, limeamuliwa kuwa ukamilifu wa mwanadamu haupatikani isipokuwa kwa Neema ya Mungu tu, kwa hiyo hakuna mjadala tena, suala hilo limekwisha.
Ni katika hukumu hiyo toka Roma ndipo ulipozaliwa msemo maarufu alioutumia Mtakatifu Augustine kwa wafuasi wake kwamba Roma locuta, causa finite est, kwamba Roma imesema, shauri limefungwa (Rome has Spoken, the matter is finished).

Ndani ya CCM huwa kawaida kwa rais na mweyekiti wake kutopingwa anapowania kuongoza kipindi cha pili kukamilisha miaka kumi ya ukomo wa urais wa Tanzania kwa mujibu wa Katiba. Ndiyo ilivyokuwa baada ya Uchaguzi Mkuu wa 2020, uliomweka madarakani aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano, Hayati John Magufuli na aliyekuwa Makamu wake Samia Suluhu Hassan.
Ni wazi kwamba wapo watu ndani ya chama walishajiandaa kujitokeza kuomba kuwania Urais wa Tanzania kupitia chama hicho ifikapo 2025, lakini katika maisha yetu Mola ndiye mpangaji wa yote. Machi mwaka huu Rais Samia kwa mujibu wa Katiba akawa ndiye Rais wa Tanzania baada ya kifo cha mtangulizi wake, Hayati Rais Magufuli.

Katiba ya nchi inaelekeza kuwa ikitokea Makamu wa Rais anachukua nafasi ya Rais kwa sababu zozote kwa mujibu wa katiba hiyohiyo, ikiwa imebaki miaka minne kabla ya kufikia uchaguzi mkuu unaofuata, atahesabiwa kuwa ameongoza kwa kipindi kimoja, na hivyo kubakiza awamu moja kama atataka kuendelea, ikiwa atashika nafasi ya rais chini ya miaka mitatu, ataruhusiwa kugombea kwa mihula miwili mizima ya miaka mitano mitano. Rais Samia bado anayo nafasi ya kuomba tena kipindi cha pili cha miaka mitano.

Kulizuka taarifa mkanganyiko za watu kuendelea na mikakati ya kuelekea 2025 bila kujali utamaduni kiliojiwekea Chama Cha Mapinduzi kwamba Rais anayekuwa madarakani ikiwa hajakamilisha kipindi chake cha awamu ya pili hapingwi ndani ya chama. Vuguvugu lilishaanza kushika kasi, tetesi na uzushi ukawa mwingi kiasi cha kuanza kuwachanganya wananchi na wananchama wa CCM.

Hatimaye katika madhimisho ya siku ya Demokrasia Rais Samia amevunja ukimya na kuweka bayana kuwa kwa majaaliwa ya Allah, yuko kiringeni 2025. Waliokuwa na mashaka, waliokuwa wanatamani iwe na waliokuwa kinyume chake huu sasa si wakati wa hisia na tetesi, ukweli uko dhahiri shahiri, Rais Samia anagombea mwaka 2025. Na kama ulivyo utamaduni mzuri wa ndani ya CCM inatarajiwa wana CCM wote wamauunge mkono kwa nguvu zote, mjadala nani ni nani sasa umefungwa rasmi, kilichobaki sasa ni namna gani ushindi wa tufani unapatikana ifikapo 2025.

Tanzania Kimataifa
Samia Kuelekea 2025
 

Kalamu1

JF-Expert Member
Jul 7, 2018
11,307
2,000
Siyo kwamba Samia atagombea, nadhani ulipaswa kusema rais atajipa ushindi wa urais 2025
Kuna mengi yanayopashwa kutokea kati ya sasa na hiyo 2025 ambayo yote yanapinga hilo la "rais atajipa ushindi wa urais 2025".

Ndani ya CCM kwenyewe yapo mengi yatakayompa ugumu; na hata akifanikiwa huko, atakutana na visiki kadhaa nje ya CCM.

Hata arembue kiasi gani, safari hii mambo ni tofauti kabisa.
 

tang'ana

JF-Expert Member
Apr 3, 2015
10,860
2,000
Huyo bibi sijui nani anamdanganya kuwa tunampenda.keshafundishwa roho ya kikatili na akina Sirro ,kawaje sijui.
 

Shocker

JF-Expert Member
Sep 15, 2012
1,363
2,000
Si kweli ndani ya CCM huwepo upinzani katika kugombea nafasi ya Uraisi na shida ni kuzidiana mbinu tu na zaidi maslahi na ujanja ujanja,sasa hapo ndipo anapopigwa mtu na chini,kwa sasa ndani ya CCM nafasi ya uraisi ipo wazi tena nyepezi kwa wale waliokuwa wakishindana misuli na akina Magufuli Kikwete na Mkapa ambao kwa sasa wote ni marehemu labda mmoja tu ambae nae anaelekea huko kwani Dhulma waliyoifanyia Zanzibar inawatafuna bila ye wenyewe kujua.

kwa upande wa Da Sami fukuto na mawimbi ya kugombea nafasi ndani ya CCM hio hana ubavu nalo,inajulikana vuke lipo na linatembea chini kwa chini ,wanasema wanajipanga ili kuitwaa nafasi hio.

Kama Da Sami anataka kuwini chance hio ni lazima kuanzia sasa aweke Tume huru ya Uchaguzi tena aichague na kuipanga vilivyo na aiweke huru kiuhakika kabisa bila ya kuwa na shaka ndani yake na hapo CCM waleee watakuwa na hofu ya kwamba hata wakifanikiwa mtihani upo kwenye kuivuka Tume ambayo mhusika mkuu bado ni Raisi.
 

Shocker

JF-Expert Member
Sep 15, 2012
1,363
2,000
Ndoto hizo, wazanzibari ni waarabu wa pemba wanajuana kwa vilemba ,Auntie Sami hagombei tena anawawachia zigo lenu wenyewe machogo si mnao akina Mdee huko wanawatosha .
 

G4N

JF-Expert Member
Apr 6, 2014
763
1,000
Kuna mengi yanayopashwa kutokea kati ya sasa na hiyo 2025 ambayo yote yanapinga hilo la "rais atajipa ushindi wa urais 2025".

Ndani ya CCM kwenyewe yapo mengi yatakayompa ugumu; na hata akifanikiwa huko, atakutana na visiki kadhaa nje ya CCM.

Hata arembue kiasi gani, safari hii mambo ni tofauti kabisa.
Ndani ya chama hakuna shida yoyote. Yeye ndiye mwenyekiti, safu nzima ya uongozi wa chama ni yake, na wajumbe wa CC ni wake. Nani wa kuleta fyoko?

Nje ya ccm yeye ni rais, vyombo vyote vya ulinzi na usalama bila kusahau katiba ya nchi viko chini yake. Nani wa kuleta fyoko??

Urais 2025 ni wa mama
 

Kalamu1

JF-Expert Member
Jul 7, 2018
11,307
2,000
Ndani ya chama hakuna shida yoyote. Yeye ndiye mwenyekiti, safu nzima ya uongozi wa chama ni yake, na wajumbe wa CC ni wake. Nani wa kuleta fyoko?

Nje ya ccm yeye ni rais, vyombo vyote vya ulinzi na usalama bila kusahau katiba ya nchi viko chini yake. Nani wa kuleta fyoko??

Urais 2025 ni wa mama
Hapa unamzungumzia Magufuli, ambaye tayari hatunae!

Naona wewe unakwenda kwa mwendo wa kinyonga mkuu!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom