Ukweli siku zote unauma iwe ni ndani ya ccm au nje yake pia! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ukweli siku zote unauma iwe ni ndani ya ccm au nje yake pia!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Twaa, Mar 28, 2012.

 1. T

  Twaa Member

  #1
  Mar 28, 2012
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 46
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wanajamvi hamjambo? Mie napenda kusema ukweli hata kama nikiusema huo ukweli nitauawa! Dunia ni tambara bovu huwa haina mwenyeji hata kidogo! Ila kwa CCM kama chama tawala sii rahisi kwao kuamini kwamba watakua kama KANU ya Kenya iliyoasisiwa na KENYATTA Ila CCM wapende wasipende watafika huko KANU ilikoenda!
  Pia ni lazima na wao wabadilike kama hawapendi kua kama KANU ya Kenya! Wabadilike kivipi? Ni lazima wabadilike kwa kutoa haki za msingi za raia wa Tanzania kabla uvumilivu haujawashinda zaidi ya hapa walipo!
  Ikumbukwe kule Zambia na pia Senegal watu wake waliichoka serikali iliyopo madarakani na kuamua kuiondoa kwa njia ya sanduku la kura ila kwa CCM ni vigumu wao kuukubali ukweli wa matokeo ya sanduku la kura! Ila sasa CCM itakataa kuukubali ukweli ila siku ya mwisho kabisa viongozi wake na waandamizi wake wote wanaweza kua kama BAGBO wa Ivory Cost au GADDAFI wa libya! Chondechonde kwa CCM muwe tayari kukubaliana na ukweli wa mambo la sivyo Tanzania inawezekana ikawa tanzania nyingine na sio hii ya sasa!
  Kama chama kinatawala nchi , kina wabunge wengi bungeni halafu mnatuambia eti nchi yetu ni maskini bila sababu ya msingi kwanini ni maskini halafu kwa upande mwingine hampo tayari kukubaliana na ukweli wa sanduku la kura sisi tuendelee kuwavumilia?
  Ujumbe kwa watanzania ''NI HERI KUFA UKIPIGANIA HAKI KULIKO KUISHI BILA MATUMAINI!'' ikumbukwe hawa viongozi wetu wa serikali yaani CCM wanatumia udhaifu wetu wa kutodai haki zetu wanajifaidisha na ndio maana wanatuita sisi maskini, je taifa lingekua maskini lingewasomesha wao na mpaka sasa wanakua na maono ya kutambua kuwa sisi watz ni maskini! Ila siku zote hazilingani ipo siku itakayokua na historia mbaya kwa hawa CCM.
  PIA WANAJAMVI IKUMBUKWE BILA KUFA WA WATZ KADHAA HAKI HAITAPATIKANA HATA KIDOGO, TUCHUKULIE MFANO MZURI WA NCHI YA KENYA KTK UCHAGUZI WA MWAKA 2007; BAADA YA MATOKEO KUTANGAZWA NA WAKENYA KUHISI HAWAJATENDEWA HAKI WALICHUKUA HATUA THEN FAIDA YAKE SASA NI KWAMBA WAKENYA HAO SASA WANA KATIBA AMBAYO INAMLINDA RAIA NA SIO KIONGOZI , KWA MFANO NAIBU JAJI WA MAHAKAMA KUUKUBALI KENYA KWA JINA ''NANZ BARAZA'' ALIMTISHIA MLINZI WA SUPERMARKET MOJA NA MLINZI HUYO ALIPORIPOTI KISA HICHO HUYO NAIBU JAJI ALIAMBIWA AJIUZULU NA AKAJIUZULU ! Sasa hiyo ni mojawapo ya faida ya kupoteza wachache ktk nchi inayokombolewa kutoka ktk mikono ya wahujumu uchumi na mafisadi! Wachache hao naweza kua mimi au wewe, tuwe tayari kwa mabadiliko tusikubali kuudhalilisha utu wetu wa Mtz kwa kuwakumbatia na kuwaheshimu mafisadi! Nawasilisha!!!!!!!
   
 2. chitambikwa

  chitambikwa JF-Expert Member

  #2
  Mar 28, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 3,940
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Uliyosema ni kweli tunahitaji kichaa kama Mtikila
   
 3. LOWE89

  LOWE89 Senior Member

  #3
  Mar 28, 2012
  Joined: Nov 18, 2011
  Messages: 149
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Si mtu mmoja ila watu wengi wakielewa na kuchukua hatua italeta mabadiliko. leo nilibahatika kuona mahojiano ya wazee wa ccm chanel ten kwenye kipindi cha makwaia ambao ni Butiku, Kitine na Kaduma. wazee hao wamesema mengi sana lakini wakamalizia kuwa nchi hii inaelekea kukolapse (utatafsiri mwenyewe) maana matatizo mengi yanafunikwa hayatatuliwi. misingi mikuu ya uongozi hakuna hata mmoja anayeifuata isipokuwa pesa ndiyo inaongea. nimewapenda!!
   
 4. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #4
  Mar 28, 2012
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  ccm iliasisi kazi za tanu mwaka 1973 ambazo lengo lake lilikuwa ni uhuru ambao ulishapatikana 1961.
  kuanzia wakati huo haikuwa na kazi kwani wakati inarithi tayari lengo lilishatimia.

  ni wakati wakuipumzisha gia ya mlima kwani sasa tupo tambarare,jia ya mlima inakufa kwa sababu ya kufanya kazi si yake.
   
 5. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #5
  Mar 29, 2012
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,598
  Likes Received: 3,888
  Trophy Points: 280

  nashangaa bado watu mnamkumbuka Mtikila...ombwe la uongozi lipo! ombwe la upinzani ni kubwa zaidi!
   
 6. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #6
  Mar 29, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,801
  Trophy Points: 280
  Ombwe la uongozi, Ombwe la upinzani either way ccm haikwepi lawama!!!!!!!
   
 7. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #7
  Mar 29, 2012
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160

  Na nakwambia ya kwmb hili gear ikifa hakuna hata spear madukani!

  Hili la sisiem hakika imekwenda kushoto na nikimaanisha ya kwmb bado kitambo kidogo sana hata ccm haitasikika bali itabaki kuwa ilikuwepo chama iliyo na jina kama hii!

  Hakika bado kitambo kidogo sana!!!!
   
Loading...