Ukweli ni upi kuhusu hili!!!

Mtu wa Pwani

JF-Expert Member
Dec 26, 2006
4,184
671
Makasha ya risasi yaibwa kambi ya Mzinga Moro
John Nditi, Morogoro
Daily News; Saturday,May 31, 2008 @00:02



Watu sita akiwamo mwanamke mmoja wanashikiliwa na Polisi mkoani Morogoro kwa tuhuma za wizi wa makasha ya risasi baada ya kuvunja ghala la kuhifadhia milipuko ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania ( JWTZ), Kikosi cha Mzinga mkoani hapa.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, Thobias Andengenye alitoa taarifa hiyo jana kwa waandishi wa habari na kusema kati ya hao watatu ni wafanyakazi wa kambi hiyo.

Kwa mujibu wa kamanda huyo, taarifa za wizi huo zilitolewa Mei 19 mwaka huu asubuhi na uongozi wa Jeshi wa Kambi ya Mazao maarufu kama Mzinga iliyopo mkoani hapa katika Kituo Kikuu cha Polisi mjini hapa.

Alisema baada ya kutolewa kwa taarifa hizo, upelelezi ulianza mara moja ambako watu sita akiwemo mwanamke mmoja wamekamatwa na kushikiliwa na Polisi. Hata hivyo, Kamanda huyo hakutaja majina ya watuhumiwa hao kwa kile alichosema kutasababaisha kuvuruga upelelezi unaoendelea kwa wakati huu juu ya kuwapata wahusika wengine.

Akizungumzia mazingira ya wizi huo, Kamanda huyo alisema kwa mujibu wa maelezo ya uongozi wa kambi hiyo, siku hiyo ya tukio waangalizi wa ghala ya milipuko waligundua wizi huo baada ya kufunguliwa mlango wa ghala.

Kwa mujibu wa Kamanda, wahusika walipofungua mlango waligundua makasha ya risasi za aina mbalimbali hususan za bunduki za rifle yameibwa. Andengenye alisema kati ya watuhumiwa hao waliokamatwa na Polisi, watatu ni wafanyakazi wa kambi hiyo ya Mzinga na wengine ni kutoka nje ya kambi hiyo.

Alisema upekuzi wa Polisi uliofanyika nyumbani kwa mmoja wa watuhumiwa hao alikutwa na risasi 1,500 na upekuzi unaendelea kwa watuhumiwa wengine. Hata hivyo, Kamanda huyo alisema uongozi wa kambi hiyo unafanya ukaguzi wa risasi katika maghala yake ya milipuko kuweza kubaini idadi kamili ya risasi zilizoibwa.

http://habarileo.co.tz/kitaifa/?id=9362
 
Wizi kama huu unafanywa na viongozi wa jeshi wenyewe. Kilichotokea hapa ni kwamba deal limeingia nyongo na ndio maana wanaanza kumsaka mchawi. Kesi kama hizi zinamalizwa kiutu uzima bila kusikia watu wamehukumiwa vifungo. Kuna habari kama hizi ziliwahi kutokea miaka ya nyuma pale maeneo ya mto Wami. Kulikuwa na majambazi waporaji nyakati za usiku. Lakini habari tulizonazo ni kwamba uporaji ule ulikuwa unafanywa na askari wa jeshi (nasikia kuna kambi ya jeshi pale jirani sijui inaitwaje) kwa amri kutoka kwa wakuu zao.
 
kama ni hivyo tumekwisha zombe alitumia polisi na huku yanatumika majeshi


raia ndio tumeuwawa hatujui nani wa kutulinda?
 
Hapo sasa anahusika Mkuu wa Majeshi ,vipi atachukua hatua ,maana kama ni kuiteka kambi hiyo basi tayari watekaji wangelikwisha fanikiwa ,mkuu wa kambi hiyo ,walinzi wa ghala ,afisa wa zamu wa siku hiyo , wanaolinda geti la kuingilia kambini.
Naweza kusema mchezo huo pengine upo zamani na siku za mwizi ni arobaini na huenda ilikuwepo biashara nzuri tu na pia huenda ikawa ndio geti kuu la risasi zinazotumika kufanyia ujambazi Daresalama na mikoa mingine.
Risasi alfu moja na mia tano ,hii ni hatari kubwa sana , na ndio zimekutwa kwa mtu mmoja tu ,mkuu wa majeshi umepata kibarua hicho kazi kwako,macho ya wananchi yote yanaelekezwa kwako maana kuona ni hatua gani utakazozichukua na inaonyesha kuna pengo kubwa katika kuhifadhi silaha za jeshi.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom