Ukweli ni lazima tuuseme hadharani: Rais Magufuli alikuwa anaona kitu ambacho wengi hatukuwa tunaona; Je, ni Mungu aliyesema naye?

Mtini

JF-Expert Member
Apr 28, 2011
1,487
2,344
Utendaji kazi wa Mungu ni waajabu sana, ili umsikie Mungu akisema ni lazima uwe kwenye nafasi husika. Mfano kama wewe ni mwenyekiti wa mtaa Mungu atasema na wewe kuhusu mtaa wako ni mara chache atakuambia kuhusu mitaa mingine au nchi yote kwa ujumla ila uwe na uhakika mara nyingi atasema na wewe kuhusu mtaa wako kama ukimtafuta.

Hivi hadi leo tungekuwa lockdown? Hali zetu zingefananaje? Hata hao waliokuwa lockdown wanajichomoa kimya kimya maana hali zimeanza kuwa tete. Msimamo na ujasiri aliokuwa nao Rais Magufuli aliupata wapi licha ya pressure kuwa kubwa sana hadi akawa apokei baadhi ya simu ya marafiki zake? Je, ni Mungu alimsemesha kitu ambacho hakutusemesha wengine?

Aina ya ujasiri na msimamo aliokuwa nao juu ya Corona naamini kabisa ni Mungu alimsemesha. Na yawezekana kuamua kwenda likizo ndefu vile ni ili kujitenga na pressure ya watu ili asije timiza matakwa yao bali mapenzi ya Mungu maana alijua Mungu amesema na yeye kuhusu Taifa la Tanzania hajasema na wengine.

Ni wakati muafaka watu kama sisi tuliokuwa kinyume nae tena kwa ukali kabisa wa kumsema vibaya, kina Mbowe and the like, wote tutoke mafichoni, tufanye press kama tulivyofanya tupongeze na kumshukuru Mungu kuwa tumevuka salama
 
Na ambao hawaamini Mungu unawaweka wapi?Taifa la Tanzania Ni la Watanzania Wala halima uhusiano na Mungu, Taifa la Tanzania halimtambui Mungu yeyote.

Watanzania Kila mtu mmojammoja ana Mungu wake, Kama unaona umeguswa na utendaji wa Magufuli wewe pekeako mwombee kwa Mungu au Mungu wako unayemjua. Taifa la Tanzania likiamua jambo, haliamui kwa kuogopa Mungu au kupenda Mungu Bali kwa Yale ambayo Watanzania wanapenda yafanyike kwa kufuata katiba.

Halafu Kama unaongelea Mungu wa waKristo Basi Mungu huyo huwa sio wa Kuwanangia Wengine na kuonesha kuwa wengine ni zaidi wengine sio. Mungu Ndio anahukumu na sio mwanadamu. Huwezi kuja na utashi wako hapa eti watu Waite press conference sijui wafanyaje kwa mambo ya Imani za kufikirika tu.

Let's be realistic.
 
Na ambao hawaamini Mungu unawaweka wapi?Taifa la Tanzania Ni la Watanzania Wala halima uhusiano na Mungu,Taifa la Tanzania halimtambui Mungu yeyote.

Watanzania Kila mtu mmojammoja ana Mungu wake, Kama unaona umeguswa na utendaji wa Magufuli wewe pekeako mwombee kwa Mungu au Mungu wako unayemjua.Taifa la Tanzania likiamua jambo,haliamui kwa kuogopa Mungu au kupenda Mungu Bali kwa Yale ambayo Watanzania wanapenda yafanyike kwa kufuata katiba...
Kama hawaweza mshukuru Mungu basi wamsifu mtu mwenye msimamo dhabit
 
Mtoa mada umekula maharage ya wapi? Naona unatamani kumfananisha magufuli na MUNGU,eti mungu amemsemesha magufuli!!! Nyie malofa mna kufuru kwelikweli
Mungu husemaesha kila mtu katika nafasi yake hiyo siyo kufuru we elimu yako ya dini mbona ndogo hivyo? Au we mpagani nini?
 
Mbona unachagua ya kusikia? Aliyesema tufunge siku tatu ni nani?
Nikiwa na kumbukumbu nzuri, hiyo kauli ilikuja kwa ajili ya kuondoa Korona. Haikuhusiana na ku-lock au kuto-lock Dar.

Naamini mlengo wa hoja yako umejikita kwenye ku-lock Dar.

Kadhalika, Mh. Rais mwenyewe alishuhudia kuwa hata mwanae mwenyewe aliugua Korona tu kwamba alipona kwa kujifukiza. Hiyo ndo ikaleta chachu ya 'kujiuguza' majumbani. Hata leo hii, sidhani kama kuna aliye tayari kujipeleka hospitali.
 
Corona inauwa kimya kimya na haisemwi, kwani wewe umewahi kusikia ikisemwa kama yale mandege tuliyonunua yanaleta faida au hasara? Zijue siasa vizuri utamjua magu.
 
Utendaji kazi wa Mungu ni waajabu sana, ili umsikie Mungu akisema ni lazima uwe kwenye nafasi husika. Je, ni Mungu alimsemesha kitu ambacho hakutusemesha wengine?

Aina ya ujasiri na msimamo aliokuwa nao juu ya Corona naamini kabisa ni Mungu alimsemesha ili atimiza mapenzi ya Mungu maana Mungu amesema na yeye kuhusu Taifa la Tanzania.

Ni wakati muafaka watu kama sisi tuliokuwa kinyume nae tena kwa ukali kabisa wa kumsema vibaya, wote tutoke mafichoni, tufanye press kama tupongeze na kumshukuru Mungu.
Naunga mkono hoja
P
 
50% nakubaliana nae ila 50% napingana nae ila namshukuru tu ya kwamba kidogo ameweza kurejesha Nidhamu ya Kiutendaji na Nchi inakwenda.
 
Back
Top Bottom