Ukweli ni kwamba watu wanene na wafupi vazi la suti halikubuniwa kwa ajili yenu, mnalazimisha kulivaa.

Mukulu wa Bakulu

JF-Expert Member
Aug 12, 2014
4,052
12,904
Ukweli ni kua vazi la suti ni vazi la heshima na linampendezesha mtu na kumuonyesha wa tofauti kidogo. Watu wengi hupendelea kuvaa suti kwenye matukio muhimu kama harusi na matukio makubwa makubwa ili kuyapa uzito.

Habari ambayo sio nzuri kwa baadhi ya watu ni kwamba vazi la suti halikubuniwa kwa ajili wa watu wafupi na wanene. Watu wafupi na wanene kuvaa suti ni kulazimisha maana kwanza hawapendezi, pili ni kudhalilisha vazi lenyewe. Hili vazi lilibuniwa kwa ajili ya watu warefu na wasio na vitambi. Sasa kukuta mtu mfupi alafu ana kitambi amevaa suti inakua ni kichekesho, inakua kama gunia la korosho linalotembea.

Watu wanene na wafupi hupendeza zaidi kama wakivaa kanzu au msuli na nyanya puza na mavazi ya namna hiyo.

Ukweli ni kwamba tuvae mavazi yanayoendana na miili yetu na maumbile yetu. Tusipende kuvamiana kulazimisha kuvaa mavazi ambayo yalibuniwa kwa ajili ya watu wa maumbile flani.
 
Mbona mimi ni Big Hila nikipiga Suti wewe na ndugu zako mnakuja stand kunisalimia
 
images (9).jpeg

Haya huyo sasa Mzee Baba.
 
Back
Top Bottom