Ukweli ni kwamba wanaohamia ccm leo wanaunga mkono kila lililofanywa na awamu hii , Ukiwemo Muswada kandamizi wa vyama vya siasa

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,557
217,844
Unapohamia ccm leo ufahamu kwamba unaunga mkono juhudi zote za kuficha taarifa za Shambulizi la mauaji ya Tundu Lissu , yaani unaunga mkono Lissu kunyimwa matibabu ili afe kwa kukosa huduma baada ya kushambuliwa , Ni kweli kwamba kila mmoja anayo haki ya kuhamia chama akipendacho , bali ni lazima tukumbuke kwamba ukipenda jongoo basi usisahau kuupenda na mti wake , ni lazima ukubali utaratibu mpya wa kutoruhusiwa kusalimia mgonjwa wa upinzani , ni lazima ukubali kwamba wapinzani ndio maadui wa nchi hii na hawaruhusiwi kufanya siasa za majukwaa , na wakithubutu watandikwe mabomu au risasi za moto

Kwahiyo basi wote wanaohamia ccm leo wamekubali kufichwa kwa CCTV CAMERA ya majengo ya waheshimiwa kule Dodoma ili kuficha taarifa , wamekubali Alphonce Mawazo asizikwe kwa vile Geita kuna kipindupindu , wamekubali kwamba upinzani ni uhaini , na ni lazima wakubali pia kwamba Mbowe na genge lake ndio walimuua Akwilina , ni lazima pia wakubali kwamba unyama wote wanaotendewa wapinzani ni halali yao maana wanatumwa na mabeberu .

Hivyo basi ndugu wananchi mnapaswa sasa kuwatambua wahusika kutokana na matendo yao ya sasa , na si yale yaliyopita maana wakati tunaoishi ni huu na ujao , hatutaishi tena jana wala juzi.

Mungu ibariki Tanzania
 
CCM imewahujumu watanzania toka Uhuru lakini bado haijaridhika .ila ipo siku (nasema siku inakuja) watanzania watashidwa kuvumilia na wataamua kujikomboa kutokana udhalimu huu unaoendelea ..chenye mwanzo hakikosi mwisho
 
Unapohamia ccm leo ufahamu kwamba unaunga mkono juhudi zote za kuficha taarifa za Shambulizi la mauaji ya Tundu Lissu , yaani unaunga mkono Lissu kunyimwa matibabu ili afe kwa kukosa huduma baada ya kushambuliwa , Ni kweli kwamba kila mmoja anayo haki ya kuhamia chama akipendacho , bali ni lazima tukumbuke kwamba ukipenda jongoo basi usisahau kuupenda na mti wake , ni lazima ukubali utaratibu mpya wa kutoruhusiwa kusalimia mgonjwa wa upinzani , ni lazima ukubali kwamba wapinzani ndio maadui wa nchi hii na hawaruhusiwi kufanya siasa za majukwaa , na wakithubutu watandikwe mabomu au risasi za moto

Kwahiyo basi wote wanaohamia ccm leo wamekubali kufichwa kwa CCTV CAMERA ya majengo ya waheshimiwa kule Dodoma ili kuficha taarifa , wamekubali Alphonce Mawazo asizikwe kwa vile Geita kuna kipindupindu , wamekubali kwamba upinzani ni uhaini , na ni lazima wakubali pia kwamba Mbowe na genge lake ndio walimuua Akwilina , ni lazima pia wakubali kwamba unyama wote wanaotendewa wapinzani ni halali yao maana wanatumwa na mabeberu .

Hivyo basi ndugu wananchi mnapaswa sasa kuwatambua wahusika kutokana na matendo yao ya sasa , na si yale yaliyopita maana wakati tunaoishi ni huu na ujao , hatutaishi tena jana wala juzi.

Mungu ibariki Tanzania
Swali moja mnakwepa kujiuliza au kuuambia umma ni WHO IS NEXT?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom