Ukweli ni kwamba pamoja na nia nzuri ya Rais Magufuli, sasa hivi Tanzania ni kama uwanja wa fujo

Kazi kwa mazoea. Hii ni shida. Mpaka tuzoe kufuata sheria. Kilatu tuna kama ni fujo. Kama umnavyoona wewe
 
Good analysis Mkuu. Ndio maana nina wasiwasi sana na anachofanya raisi Magufuli, pamoja na kwamba ana nia nzuri. Hata Hitler alikuwa na nia nzuri na Ujerumani, aka thrive kwenye support aliyopata toka kwa baadhi ya Warumani na kuwapuuza hata kuwaua walioona anakosea - pamoja na nia yake nzuri. Kiongozi mzuri unatakiwa uwe flexible, kuna wakati inabidi urudi kwenye drawing board, sio kuwa persistent na njia yako ambayo akili yako inakuambia ndiyo inayofaa.

Raisi Magufuli anapaswa kuwa humble na kukubali kwamba kuna baadhi ya approach zake katika kuinyosha nchi sio tu hazifai, bali hazileti mafanikio na sana sana zinakuwa na matokeo mabaya kwa ujumla.

Japo hatujui nani alihusika, hakuna mtu mwenye akili ambaye atabisha kwamba kupigwa risasi kwa Tundu Lissu ni matokeo ya kujihusisha kwake na siasa katika awamu ya raisi Magufuli. Na ukweli mchungu ambao watu hawataki kuusema ni kwamba katika awamu zote za uongozi zilizopita isingekuwa raisi kufikia hali ya kupigana risasi waziwazi hivyo kwa ajili tu ya siasa - na hapo sijagusia Kibiti. Hivyo ni wazi kwamba raisi Magufuli anapaswa kujiuliza kama njia zake, hata kama anahisi zitakuwa na positive impact ya muda mrefu, kama negative impact ya sasa ina-justify kuzikomalia. Na tunajuaje impact zinazoonwa kama ni short term hazitakuwa za long term kiasi hata ku-overshadow benefits anazotarajia?

Hebu jiulize, kuna ubaya gani kukomalia kwa kila namna ufisadi, wafanyakazi hewa, vyeti feki, uwajibikaji, huku ukiwa umeruhusu wapinzania kuendelea na siasa zao za mitaani kama kawaida? Au unadhani Watanzania ni wajinga sana kiasi kwamba hawatajua kama wanadanganywa na hotuba za wanasiasa pale wanapoona juhudi halisi za raisi wa nchi na chama chake cha siasa? Kwa namna fulani, kusema unawazuia wanasiasa kwenda kuhubiri uongo kwa wananchi is an insult to the intelligence of Tanzanians, hata kama si wote wana PhD kama wewe.

Tusisahau pia kila wakati una mbinu zake..
Hittler ilimbidi kutumia mbinu zile kwa wakati ule, Wajerumani wamefaidika na mbinu za hittler japo pia zimeacha machungu kwa Wajerumani na wasio Wajerumani lakini at the end Germany is amongest the superpower,

Mbinu za karne ya 19 ukizitumia sasa huwezi kufanikiwa baadala yake utaanguka na usiamke tena mfano Zimbabwe.
Tuna kitu cha kujifunza kutoka Malysia,Indonesia, Thailand, Singapore, NewZealand, Brazil nk, Kwanini waliweza kufika hapo bila ya kutumia mbinu za karne ya 19?...

Ni vizuri kama watanzania tukatanua mawazo na kushauri with posibilities and tangiable evidence ili tuwe na suluhu na tuchague mbinu itakayotuwezesha kwenda mbele huku tukizingatia hii ni karne ya 21..
 
Rais hana nia mbaya na nchi hii,ila ukweli mchungu ni kwamba hakujiandaa kuwa rais,ana uwezo mdogo wa kuongoza nchi,alitakiwa abaki kuwa waziri tu.
Uchumi-ukweli ni kwamba uchumi umedorora,hebu ajiulize kwanini TRA wanaunderperform sana kwa miezi 12 iliyopita,tena mwezi huu nasikia itakuwa balaa nusura ya mkosi importation imepungua sana imesababisha ata biashara za ndani zimedorora.Japo tuna sera mfu ya viwanda ambayo tunajidanganya nchi itakuwa ya viwanda..... kuelekea kuwa nchi ya viwanda ni chakato mrefu ...europe industrial revolution ilichukuwa zaidi ya miaka miaambili ilikuwa mchakato mrefu ulioanzia kwenye utawala,kisasa,kidini na kijamii
utumishi wa umma pia umekuwa kaa la moto litasababisha kuwa na watumishi wasio wabunifu,waoga
Biashara na kilimo ndio mgongo wa nchi hii ,Rais akae na wafanyabiashara asijenge nao uadui
ifikie wakati wa URAIS kuwa Taasisi sio jeshi la mtu mmoja

nchi ni ya kwetu sote hii tabia ya umimi na ubabe aliyonayo mheshimiwa abadilike

Tutafika tu japo wengi wataumia sana na wachache tutafaidi sera mbovu za awamu ya tano
 
Iliwahi kuwa haijatulia huko nyuma, mfano kipindi cha kufunga mikanda kwa miezi 18 baada ya vita vya Kagera. Nchi hii ilivumilia hali ambayo si rahisi watu kuvumilia. Sasa tofauti ya wakati huo na sasa, ni kwamba Nyerere, kwa hekima yake ya uongozi, alihakikisha wananchi wote wako nyuma yake.

Mie nadhani ingekuwa ni busara sana kwa Raisi Magufuli, kama alivyofanya Nyerere wakati huo, kuhakikisha kwamba katika kipindi cha mpito kuelekea kuinyoosha nchi, wanananchi wote wako nyuma yake, kutia ndani vyama vya upinzani. Ni mpango mbaya kuwagawanya wananchi kiitikadi wakati uko kwenye kampeni kubwa ya kuinyoosha nchi.

Hakuna kipindi ambacho Magufuli alipaswa awe karibu sana na wananchi na vyama vya upinzani kama hiki cha kuinyoosha nchi. Hii ni philosophy ndogo sana ya uongozi ambayo nadhani Raisi Magufuli haitambua - creating a common enemy in order to have the support of the masses.

Hupaswi kutengeneza "maadui" au migawanyiko wakati unataka kukabiliana na "common enemy". Common enemy hapa ni ufisadi, kutowajibika, kuibiwa na wawekezaji nk. Sasa haya ndio mambo ambayo Magufuli alipaswa kuya preach na kutaka support ya vyama vya upinzani na wananchi kwa ujumla - na ungekuta hata kina Tundu Lissu wanamkubali na kumsifia, kwa sababu ana-address mambo ambayo ni "common enemy".

Na Raisi Magufuli anasahau strategy muhimu sana katika kujenga nchi - "Rome was not built in one day" Anajipa mambo mengi sana kwa wakati mmoja. Anataka kumla ng'ombe kwa mkupuo, ataweza wapi kama sio kuja kuchanganyikiwa kukuta umeamza kula pembe zikakudhuru tumbo na kisha ukashindwa hata kula maini??

Mara nyingine tukiri kwamba mambo ya public administration na management ni profession. Sio siasa.
You've made a good point chief
 
Kulifikia tatizo na kulitatua kuna njia nyingi sana, na kila mtu anaweza kutumia njia yake kutatua tatizo..
Unaweza kulitatua tatizo ukaacha athari au ukatatua tatizo bila kuacha athari..
Katika kutatua tatizo pia kunaweza kukawa na njia ambazo sio sahihi na zikashindwa kutatua tatizo bila kuacha athari..
Katika kutatua tatizo pia kunaweza kukawa na njia ambazo sio sahihi na zikashindwa kutatua tatizo na kuacha athari kubwa.

Tatizo la Taifa letu la Tanzania ni matatizo mchanganyiko ambayo yanasumbua karibu kila mtanzania, Ila tatizo kuu ni Uchumi mbovu na umasikini kwa watanzania, bila shaka ukitatua tatizo hili unaweza ukawa umetatua matatizo mengi sana.

Ni jukumu letu sasa kuamua ipi ni njia sahihi katika wakati huu wa karne ya 21 katika kutatua matatizo yetu..
Jukumu let kina nani? Je rais anashaurika??
Je watendaji walioko chini yake wanawajibika kwa mapenzi ama n kwa woga?
 
Tutulieni tu kwenye roli mpaka litakapopiga breki ili tushuke, haya mambo ya kuhamasishana turuke mmh unaweza fikia kichwa ikawa mwisho wako, ni kweli speed ni kali na barabara kologesheni kibao na roli halina break, tunakoenda hatukuoni ila mimi nawashauri tutulie tuone hadi mwisho wake.
 
Jukumu let kina nani? Je rais anashaurika??
Je watendaji walioko chini yake wanawajibika kwa mapenzi ama n kwa woga?

Hilo sio jukumu letu bali jukumu letu ni kushauri na kushauri hata kama hakuna anayesikia sisi tushauri na tuweke record ili mwisho wa siku tuweze kumhukumu huyo tunayemshauri na hasikilizi ushauri wetu..

Sasa unataka tufanyeje kama hashauriki? sasa baadala ya kubweka si ni vizuri tukaendelea tu kushauri na kushauri..
 
Nadhani wengi tulimuunga mkono Raisi Magufuli juu ya nia nzuri ya kurekebisha hali ya nchi yetu, katika masuala ya uongozi, uchumi na uwajibikaji. Lakini inafikia mahali tujiulize kama kweli hili ndilo linalofanyika. Inabidi uwe shabiki mbaya wa kisiasa au kipofu wa kifikra kutoona kwamba nchi yetu sasa imekuwa kama uwanja wa fujo karibu kila nyanja;
  • Bungeni - vurugu, mipambano, kukomoana, kunyanyasana na ukamataji wa wabunge kwa sababu zisizo za msingi, ubabe na vitisho kwa wabunge ukosefu wa nguvu za hoja na utumiaji wa nguvu za wingi (partisanship)
  • Siasa - ukosefu wa kuvumiliana na kuheshimiana, uadui unaokua kati ya vyama vya siasa, lugha za kukebehi na kukosa staha ya kiuongozi, utekaji, majaribio ya mauaji, udhibiti wa uhuru wa kuhutubia, vyama vya upinzani kuonekana wazi vikiandamwa na serikali na polisi
  • Uhuru wa vyombo habari - ufungiaji na vitisho kwa magazeti na mitandao ya kijamii, ukamataji wa kiholela wa kauli zinazoonekana kuikosoa serikali
  • Nidhamu ya kazi - nidhamu ya woga kujitokeza kwa kiasi kikubwa kwa hofu ya kutumbuliwa
  • Uwekezaji wa nje - migongano na wawekezaji (confrontation), kutofanya mambo kwa utaratibu wa kisheria
  • Utawala wa mikoani na wilayani - ubabe kama kuwekana ndani masaa 24, migongano kati ya wanasiasa na watendaji, hujuma na ufitini ili kujinufaisha kibinafsi
  • Mipaka ya kimadaraka - muingiliano ya madaraka kati ya watendaji, kutia ndani uingizaji wa siasa katika vyombo vya kijeshi taasisi za kiserikali
  • Utawala wa kisheria - ukiukwaji wa makusudi wa katiba ya nchi, ukiukwaji wa kimakusudi wa maamuzi ya mahakama, uhasama kati ya wananchi na polisi na usalama wa taifa, ubabe wa vyombo vya usalama
  • Hali ya maisha - ugumu wa maisha kwa mwananchi wa kawaida, ukosefu wa ajira, uchungu na athari za maamuzi ya serikali kama bomoa bomoa, uhalifu wenye kuongezeka, hofu na kukosa furaha, mzigo wa faini za barabarani kwa makosa madogomadogo
Kwa namna fulani, naanza kuona kuwa gharama ya "kuinyosha" Tanzania inakuwa kubwa sana, ikiwa na namna fulani ya tishio la kuifanya nchi yetu iingie katika hali isiyoeleweka na kuwa uwanja wa fujo.

Sipendekezi kwamba Raisi Magufuli aache nia yake njema ya kuinyoosha Tanzania, bali swali ambalo ningependa sana raisi Magufuli ajiulize ni kwamba, je njia anazotumia "kuinyoosha" nchi amezitafakari sana kuona faida zake na hasara za muda mrefu? Je ni bora kuwa na nchi iliyonyooka "at any cost, regardless of the socio and psychological consequences"?

Je, sasa si wakati muafaka wa kutafakari namna iliyo bora zaidi ya kuinyoosha nchi kuliko njia zinazotumika kwa sasa? Kuna faida gani kuinyoosha nchi kwa ajili ya wananchi ambao kila siku wanazidi kupandwa na hasira na nmana inayotumika kuinyoosha nchi - kwamba wao wanapaswa kuwa collateral damage?
Pointlessssssss wew chadema mbona ujasema kwanini chadema wamekosa hekima ya kumuheshm raisi na serikal wanatukana ovyo matusi ya nguoni kama wanataka kueshimiwa waanze kuwaeshm wenzao
 
Ubabe ubabe wew unamtukana MTU akikutukana unalia acha mchezo una hasira na wenzio wanayo ukitaka mambo yaende sawa tuliyaa
 
Unaweza wew au utambwela
 
Dawa ya ufisadi ni kuondoa umasikini,ukipiga vita ufisadi huku unaharibu uchumi,unatengeneza njaa,mwenye njaa kuwa fisadi ni rahisi sana

Uchumi ndio dawa ya kila kitu,hata maeneo ya watu masikini ndio yamejaa uhalifu,si masaki,oyersterbay,

Hata vita ya kupambana na ufisadi inahitaji uchumi mzuri ili uwalipe wapambanaji,uimarishe taasisi kwa mifumo ya kiteknolojia

UFISADI NI DALILI TU,kama homa,ugonjwa wenyewe ni UMASIKINI
Masiki uwa hawi fisad masikini ana moyo wakuridhika usimkosoe Mungu aliyesema Nivigumu tajiri kuuona ufalme wa mbingu matajiri ndo hawaridhkag rud hosome vizur
 
Sawa kabisa tushauri na kuweka rekodi.lakin labda nikuulize jambo ww katika mtazamo wako unaona kwamba itakaa litokee nafasi ili sisi tunaoshauti tuweze kusema kuwa tuliwah kumshauri haya?

Who cares kwa hapa tulipofika?nani anatujali juu ya miili inayoopolewa baharini Kila uchwao? Nani anayejali kwamba kuna wasiojulikana ambao huwanyima raha na yamejemgwa hofu kubwa katika jamii?

Hivi unadhan mpaka mtu mwenye madarasa ngazi ya rais kusema kuwa sikutaka kuwa raisi nilijarubu lkn wakanisukumia huo. Huoni kuwa kwa kauli hiyo ni wazi kwamba endeleen kufa mm hata sikutaka kuwa comforter wenu.

Yaan hapa kitu pekee kitakacho tusaidia wala sio katiba mpya pekee bali ni watu kusoma alama.za nyakati kisha kulitendea haki msanduku la kura
Hilo sio jukumu letu bali jukumu letu ni kushauri na kushauri hata kama hakuna anayesikia sisi tushauri na tuweke record ili mwisho wa siku tuweze kumhukumu huyo tunayemshauri na hasikilizi ushauri wetu..

Sasa unataka tufanyeje kama hashauriki? sasa baadala ya kubweka si ni vizuri tukaendelea tu kushauri na kushauri..
 
Anko tunarudisha nidhamu ilopotea ndo maaana unaona vurugu. Watakaa Sawa tu soon!,

Magu songa mbele

Hakuna nidhamu inayorudi bali unapandikizwa woga. Hapa tatizo moja linafunikwa na blanketi la tatizo jingine. Rais wetu ana kitu kimoja tu kwa mujibu wa maelezo yake yaani nia njema. Ila hana mbinu kabisa za uchumi, kibaya zaidi hana busara na ni mlevi wa madaraka. Lakini akumbuke Nyerere alikuwa na nia njema na taifa hili kuliko yeye na bado tulivaa viraka.

Hofu anayojenga na kuahidi mambo mazuri bila nidhamu ya uchumi, sioni akifanikiwa zaidi ya kulazimisha kuongezewa muda ili afikie ndoto yake. Akitaka asomeke ahamishie nguvu yake kwenye mapinduzi ya kilimo, kisha kupitia kilimo automatically viwanda itakuwa rahisi kufuata raw materials.
 
Iliwahi kuwa haijatulia huko nyuma, mfano kipindi cha kufunga mikanda kwa miezi 18 baada ya vita vya Kagera. Nchi hii ilivumilia hali ambayo si rahisi watu kuvumilia. Sasa tofauti ya wakati huo na sasa, ni kwamba Nyerere, kwa hekima yake ya uongozi, alihakikisha wananchi wote wako nyuma yake.

Mie nadhani ingekuwa ni busara sana kwa Raisi Magufuli, kama alivyofanya Nyerere wakati huo, kuhakikisha kwamba katika kipindi cha mpito kuelekea kuinyoosha nchi, wanananchi wote wako nyuma yake, kutia ndani vyama vya upinzani. Ni mpango mbaya kuwagawanya wananchi kiitikadi wakati uko kwenye kampeni kubwa ya kuinyoosha nchi.

Hakuna kipindi ambacho Magufuli alipaswa awe karibu sana na wananchi na vyama vya upinzani kama hiki cha kuinyoosha nchi. Hii ni philosophy ndogo sana ya uongozi ambayo nadhani Raisi Magufuli haitambua - creating a common enemy in order to have the support of the masses.

Hupaswi kutengeneza "maadui" au migawanyiko wakati unataka kukabiliana na "common enemy". Common enemy hapa ni ufisadi, kutowajibika, kuibiwa na wawekezaji nk. Sasa haya ndio mambo ambayo Magufuli alipaswa kuya preach na kutaka support ya vyama vya upinzani na wananchi kwa ujumla - na ungekuta hata kina Tundu Lissu wanamkubali na kumsifia, kwa sababu ana-address mambo ambayo ni "common enemy".

Na Raisi Magufuli anasahau strategy muhimu sana katika kujenga nchi - "Rome was not built in one day" Anajipa mambo mengi sana kwa wakati mmoja. Anataka kumla ng'ombe kwa mkupuo, ataweza wapi kama sio kuja kuchanganyikiwa kukuta umeamza kula pembe zikakudhuru tumbo na kisha ukashindwa hata kula maini??

Mara nyingine tukiri kwamba mambo ya public administration na management ni profession. Sio siasa.
Maluweluwe ya uchaguzi 2015 bado yanamsumbua ndio maana anafanya yote mawili.
Mahusiano ni fani lakini inakuwa bora zaidi kama kama mtu akisoma na anakipaji cha kujenga mahusiano kama kikwete,mwinyi mwalimu nk.
La mwisho kama huna karisma kubari kushauriwa na uwe mwelekevu utaficha udhaifu huo. Mwenzetu anaamini katika matumizi ya mamlaka na nguvu, na wakati huohuo anatengeneza maadui wapya,itakuwa ngumu sana kutoboa.
 
Ndio maaana nikakiri wazi kwamba moja ya sifa muhimu sana kwa kiongozi mzuri ni kuwa humble, mnyenyekevu. Na unyeneyekevu sio udhaifu tofauti na viongozi wengi sana waliopotoka wanavyodhani.
 
Pointlessssssss wew chadema mbona ujasema kwanini chadema wamekosa hekima ya kumuheshm raisi na serikal wanatukana ovyo matusi ya nguoni kama wanataka kueshimiwa waanze kuwaeshm wenzao
Mkuu mbona unajishuku sana. Kwani niliyosema hapo juu nimesema ni ya CCM, ambayo inaonekana unashabikia? Nimeongela kuwapo kwa lugha za kukebehi na kukosa staha ya kiuongozi. Kama Chadema wanatukana haifanyi iwe halali CCM kutukana. Na tatizo ni kuwa na watu wenye mentality kama yako katika ngazi za juu - akili ndogo kuwa na mamlaka makubwa.
 
Haaaaaaa unatska democrasia ujui maana ya democrasia njooo tukufunzeee democrasia upaswi kumkataza MTU kufanya atakacho lakini mfanyie anacho kufanyia akifurahia unahaja yakumchukia hakikasirika jiulize alifanya kwa makusidi flani siyo alikuwa anatafuta haki unaona sasa unatoa povu kidogo nimekugusaaaa pole RFK nilitaka nisikie u amaaanisha mini democrasia au unajambo Nyumba yake
 
Mkuu mbona unajishuku sana. Kwani niliyosema hapo juu nimesema ni ya CCM, ambayo inaonekana unashabikia? Nimeongela kuwapo kwa lugha za kukebehi na kukosa staha ya kiuongozi. Kama Chadema wanatukana haifanyi iwe halali CCM kutukana. Na tatizo ni kuwa na watu wenye mentality kama yako katika ngazi za juu - akili ndogo kuwa na mamlaka makubwa.
Democrasia haiwez kwenda mbinguni maana ukinipiga nakupiga ukinitukana nskutukana ukisema hili nasema lile tunakaaaaa sawa mambo yanaenda hapo vipi
 
nasikia waliopo serikalini sasa hivi wamefunga midomo yao hata kutoa dira ya nini kifanyike wanaogopa.......kwani inaweza ikawa tofauti ukaonekana siyo mzalendo.......wengi wanatamani kustaafu mapema walipwe chao waondokane na dhahama.........
 
Back
Top Bottom