Ukweli ni kwamba pamoja na nia nzuri ya Rais Magufuli, sasa hivi Tanzania ni kama uwanja wa fujo

Basi kama ana nia nzuri ni mtu mjinga sana.

Huwezi kuwa na nia nzuri halafu ukaiingiza nchi katika madeni ya ajabu kwa maamuzi ya jazba.

Huwezi kuwa na nia nzuri ukashindwa hata kuwa na breki ya mdomo kujua ukiwaita mawaziri uliowateua wewe mwenyewe wapumbavu, umejiita wewe uliyewateua mpumbavu zaidi.Una undermine authority yako mwenyewe.

Huwezi kuwa na nia nzuri, ukasema wewe ni rais wa wanyonge, halafu ukaachia wanyonge wanavunjiwa nyumba zao licha ya kuwa na amri ya mahakama kuzuia hilo.

Magufuli haondoi ufisadi. Magufuli ni fisadi. Kauza nyumba za umma. Kamuuzia mpaka mdogo wake na hawara wake.

Magufuli atawaingiza kwenye madeni makubwa sana ya kijinga kwa pupa zake mnazoziita kupigania rasilimali. Sasa hivi ana kesi kibao na wawekezaji na ataziongeza zaidi.

Kutumbua wafanyakazi wazembe ni gia ya kupunguza watu kwa sababu serikali haina hela. Wazembe kibao wapo wanadunda na wasio wazembe wametumbuliwa. Serikaki haina mpango.

Kilichoongezwa serikalini si uwajibikaji. Ni nidhamu ya woga. Lawrence Mafuru alimshauri rais kwamba akiingilia mzunguko wa fedha bila mpango wa kueleweka, ataharibu uchumi. Magufuli akamtumbua. Sasa hivi alichotabiri Mafuru kinatokea. Magufuli angekuwa na nia nzuri angesikiliza ushauri wa wataalam.

Magufuli hawezi kusema anabana matumizi wakati kila mwezi anatuingiza katika kesi na wawekezaji, kesi tutakazolipa hela ndefu sana.

Hana nia nzuri. Anataka kuonekana ana nia nzuri.

Duh, Mkuu, I read you. Kuanzia sasa nitakuwa ninaweka vichwa vya habari kutoka magazetini vinavyoonyesha kweli Tanzania tunakuwa uwanja wa fujo. Nitafanya hiyo update kila siku.
 
Updates:
Kuanzia sasa nitaweka kutoka magazetini habari zinazoonyesha ni jinsi gani nchi yetu Tanzania inakuwa uwanja wa fujo siku hadi siku;

  1. Mbunge Lijuakali ashikiliwa na Polisi - kwa amri ya Mkuu wa Wilaya ya Malinyi Majura Kasika, kosa likiwa ni kuhudhuria kikao cha ndani cha Chadema nje ya jimbo lake (Mwananchi 28/09/2017)
  2. Wadau wa habari nchini wainyooshea kidole serikali - wakielezea kwamba asasi na vyombo vya habari vinaogopa kutoa taarifa zinazoikosoa Serikali kwa kuhofia usalama na vitisho vinavyotoka kwenye mamlaka (Mwananchi 29/09/2017)
  3. Msukuma ajiandaa kumlipua Kamanda - Mgogoro wa watendaji wakuu wa mkoa ambapo Mwenyekiti wa CCM Geita anatangaza kuanika uhalifu wa Kamanda wa Polisi wa Geita kwa kulipiza kisasi kitendo cha kamanda huyo kumkamata kama mhalifu kwa kumkunja suruali kiunoni
 
Back
Top Bottom