Synthesizer
JF-Expert Member
- Feb 15, 2010
- 11,143
- 18,774
Nadhani wengi tulimuunga mkono Raisi Magufuli juu ya nia nzuri ya kurekebisha hali ya nchi yetu, katika masuala ya uongozi, uchumi na uwajibikaji. Lakini inafikia mahali tujiulize kama kweli hili ndilo linalofanyika. Inabidi uwe shabiki mbaya wa kisiasa au kipofu wa kifikra kutoona kwamba nchi yetu sasa imekuwa kama uwanja wa fujo karibu kila nyanja;
Sipendekezi kwamba Raisi Magufuli aache nia yake njema ya kuinyoosha Tanzania, bali swali ambalo ningependa sana raisi Magufuli ajiulize ni kwamba, je njia anazotumia "kuinyoosha" nchi amezitafakari sana kuona faida zake na hasara za muda mrefu? Je ni bora kuwa na nchi iliyonyooka "at any cost, regardless of the socio and psychological consequences"?
Je, sasa si wakati muafaka wa kutafakari namna iliyo bora zaidi ya kuinyoosha nchi kuliko njia zinazotumika kwa sasa? Kuna faida gani kuinyoosha nchi kwa ajili ya wananchi ambao kila siku wanazidi kupandwa na hasira na nmana inayotumika kuinyoosha nchi - kwamba wao wanapaswa kuwa collateral damage?
Updates:
Kuanzia sasa nitaweka kutoka magazetini habari zinazoonyesha ni jinsi gani nchi yetu Tanzania inakuwa uwanja wa fujo siku hadi siku;
- Bungeni - vurugu, mipambano, kukomoana, kunyanyasana na ukamataji wa wabunge kwa sababu zisizo za msingi, ubabe na vitisho kwa wabunge ukosefu wa nguvu za hoja na utumiaji wa nguvu za wingi (partisanship)
- Siasa - ukosefu wa kuvumiliana na kuheshimiana, malumbano kwenye vyombo vya habari, kujibizana kwa press release, uadui unaokua kati ya vyama vya siasa, lugha za kukebehi na kukosa staha ya kiuongozi, utekaji, majaribio ya mauaji, udhibiti wa uhuru wa kuhutubia, vyama vya upinzani kuonekana wazi vikiandamwa na serikali na polisi
- Uhuru wa vyombo habari - ufungiaji na vitisho kwa magazeti na mitandao ya kijamii, ukamataji wa kiholela wa kauli zinazoonekana kuikosoa serikali
- Nidhamu ya kazi - nidhamu ya woga kujitokeza kwa kiasi kikubwa kwa hofu ya kutumbuliwa
- Uwekezaji wa nje - migongano na wawekezaji (confrontation), kutofanya mambo kwa utaratibu wa kisheria
- Utawala wa mikoani na wilayani - ubabe kama kuwekana ndani masaa 48, migongano kati ya wanasiasa na watendaji, hujuma na ufitini ili kujinufaisha kibinafsi
- Mipaka ya kimadaraka - muingiliano ya madaraka kati ya watendaji, chama na serikali, kutia ndani uingizaji wa siasa katika vyombo vya kijeshi taasisi za kiserikali
- Utawala wa kisheria - ukiukwaji wa makusudi wa katiba ya nchi, ukiukwaji wa kimakusudi wa maamuzi ya mahakama, uhasama kati ya wananchi na polisi na usalama wa taifa, ubabe wa vyombo vya usalama
- Hali ya maisha - ugumu wa maisha kwa mwananchi wa kawaida, ukosefu wa ajira, uchungu na athari za maamuzi ya serikali kama bomoa bomoa, uhalifu wenye kuongezeka, hofu na kukosa furaha, mzigo wa faini za barabarani kwa makosa madogomadogo
Sipendekezi kwamba Raisi Magufuli aache nia yake njema ya kuinyoosha Tanzania, bali swali ambalo ningependa sana raisi Magufuli ajiulize ni kwamba, je njia anazotumia "kuinyoosha" nchi amezitafakari sana kuona faida zake na hasara za muda mrefu? Je ni bora kuwa na nchi iliyonyooka "at any cost, regardless of the socio and psychological consequences"?
Je, sasa si wakati muafaka wa kutafakari namna iliyo bora zaidi ya kuinyoosha nchi kuliko njia zinazotumika kwa sasa? Kuna faida gani kuinyoosha nchi kwa ajili ya wananchi ambao kila siku wanazidi kupandwa na hasira na nmana inayotumika kuinyoosha nchi - kwamba wao wanapaswa kuwa collateral damage?
Updates:
Kuanzia sasa nitaweka kutoka magazetini habari zinazoonyesha ni jinsi gani nchi yetu Tanzania inakuwa uwanja wa fujo siku hadi siku;
- Mbunge Lijuakali ashikiliwa na Polisi - kwa amri ya Mkuu wa Wilaya ya Malinyi Majura Kasika, kosa likiwa ni kuhudhuria kikao cha ndani cha Chadema nje ya jimbo lake (Mwananchi 28/09/2017)
- Wadau wa habari nchini wainyooshea kidole serikali - wakielezea kwamba asasi na vyombo vya habari vinaogopa kutoa taarifa zinazoikosoa Serikali kwa kuhofia usalama na vitisho vinavyotoka kwenye mamlaka (Mwananchi 29/09/2017)
- Msukuma ajiandaa kumlipua Kamanda - Mgogoro wa watendaji wakuu wa mkoa ambapo Mwenyekiti wa CCM Geita anatangaza kuanika uhalifu wa Kamanda wa Polisi wa Geita kwa kulipiza kisasi kitendo cha kamanda huyo kumkamata kama mhalifu kwa kumkunja suruali kiunoni (Nipashe 29/09/2017)