Ukweli ni kwamba hali ya usalama wa nchi imezorota. Pengine tulificha maana matukio ya kikatili

Francis12

JF-Expert Member
Sep 30, 2016
7,533
22,278
Anaandika Malisa Godlisten
Juzi Kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni Mhe.Freeman Mbowe aliwasilisha hoja kujadili hali ya usalama wa nchi kuzorota, kufuatia matukio ya utekaji, utesaji na mauaji yanayoendelea sehemu mbalimbali nchini. Lakini hoja yake ikazimwa kwa kile serikali ilichosema HALI YA USALAMA NCHINI NI KURIDHISHA NA HAKUNA TISHIO LOLOTE LA AMANI.

Vijana wa CCM wakashangilia kama ilivyo desturi yao. Pengine kwa kuwa wengi wanaouawa, kutekwa au kupotea ni wanachama wa vyama vya upinzani. Kwahiyo huenda CCM waliona hakuna cha kujadili. Kwao chama kwanza, utu baadae. Ndio maana walishangilia kusikia hoja ya Mbowe kujadili hali ya usalama wa nchi imetupwa.

Lakini kwa tukio la leo huko Kibiti la Polisi wetu 7 kuuawa kikatili, nadhani serikali inapaswa kumuomba radhi Mhe.Mbowe na imuombe awasilishe tena hoja yake bungeni ijadiliwe. Ukweli ni kwamba hali ya usalama wa nchi imezorota. Pengine tulificha maana matukio ya kikatili yalikua yanatokea kwa raia, sasa yametokea kwa askari wetu hatupaswi kuficha tena. Lazima tukiri kuwa hali ya usalama imezorota na tuchukue hatua. Mungu ibariki Tanzania. Poleni familia za wafiwa.!
 
Mimi kinachonishangaza zaidi ukiongelea maswala ya kiusalama unaambiwa acha mambo ya kisiasa na ongelea mambo ya maendeleo,je kuna maendeleo bila usalama?
Uncle Magu na wana ccm wenzako badilikeni....
 
Usalama wa nchi sio wa kujadili bungeni ni kupeleka vikosi vya kutosha maeneo husika na majeshi yote kuendesha operation ya kudumu ya kusaka wahalifu wote na kuwafikisha mahakamani weka siasa kando
 
Kila na ahakikishe anajilinda mwenyewe kikamilifu msipuuze hili.

Kwa wale wenye angalau ahueni ya kimaisha hakikisheni mnafunga CCTV camera majumbani.
 
Back
Top Bottom