Francis12
JF-Expert Member
- Sep 30, 2016
- 7,533
- 22,276
Anaandika Malisa GJ,
Awali ya yote nipongeze juhudi za Rais JPM za kununua ndege kadhaa mojawapo ni Boeing 787 Dreamliner iliyopokelewa wiki jana. Hizi ni juhudi za kupongezwa na kila mtanzania, kwamba sasa serikali inamiliki ndege za usafiri wa umma.
Pamoja na juhudi hizo yapo madai kwamba kuna wapinzani wanapinga ununuzi wa ndege hizo. Haya ni madai yanayotolewa na watu waliozoea kujipendekeza kwa viongozi.
Ukweli ni kwamba hakuna mpinzani anayepinga ndege kununuliwa, wala hakuna anayepinga shirika letu la ndege la ATCL kufufuliwa. Kila mtu anapongeza juhudi hizi, lakini kupongeza hakuzuii watu kuhoji. Askofu Dr.Benson Bagonza (PhD) aliwahi kusema "Kuhoji ni haki ya mtawaliwa inayolindwa kikatiba, na kujibu hoja ni haki ya mtawala. Kumzuia mtawaliwa kuhoji ni kumnyima haki yake, na kumzuia mtawala kuhojiwa ni kumnyima haki yake ya msingi inayolindwa kikatiba"
Kwahiyo watu wanaohoji kuhusu ununuzi wa ndege hizo, sio kwamba wanapinga bali wanahitaji ufafanuzi. Ni muhimu wajibiwe kwa hoja. Lazima tutofautishe kuhoji na kupinga. Mwanaharakati na mpigania uhuru wa zamani wa Rhodesia ya kusini Mchungaji Ndabaningi Thisole aliwahi kusema "Wendawazimu peke yao ndio wasioweza kutofautisha kukosoa na kupinga, na bahati mbaya tuna wendawazimu wengi wenye madaraka na vyeo."
Binafsi nimepitia hoja za wapinzani zinazowafanya waambiwe wanapinga ununuzi wa ndege. Nimepata hoja zifuatazo;
[HASHTAG]#Mosi[/HASHTAG]; Watu wanahoji kwanini tununue ndege kwa fedha taslimu? Hoja hii imetolewa na kaka yangu Sam Ruhuza. Alisema Biashara ya usafiri wa anga mara nyingi ndege hununuliwa kwa mikataba. Mashirika makubwa kama KLM, Quatar Airways etc hayanunui ndege kwa cash. Kwanini sisi tununue cash? Ndege hii imenunuliwa kwa dola milioni 225 ambayo ni sawa na Bilioni 500 za kitanzania. Kwanini tusingelipa nusu, ili pesa nyingine zitumike kwenye shughuli nyingine za maendeleo, halafu nusu inayobaki ilipwe na ndege yenyewe kupitia mapato yake? Hii hoja haijajibiwa. Majibu yanayotolewa ni kwamba wapinzani wanapinga ununuzi wa ndege. Aibu.!
[HASHTAG]#Pili[/HASHTAG]; Watu wanahoji kwanini tununue ndege wakati kuna huduma muhimu za kijamii hatuna? Hoja hii hii imetolewa na Comrade Julius S. Mtatiro. Kuna maeneo nchi hii watu wanakunywa maji kwa kushare na mifugo, kuna vituo vya afya havina watumishi, unakuta mtu ni "Medical Attendant" lakini ana act kama mganga mfawidhi wa kituo. Wanafunzi hawana mikopo wengi wamekatiza masomo, watu wanakufa kwa kukosa madawa, ajira hakuna etc.
Je kulikuwa na umuhimu wa kuacha yote haya na kukimbilia kununua ndege? Vipaumbele vyetu kama taifa ni vipi? Je tupo tayari kuona watu wanakufa kwa kukosa "panadol" lakini tunayo ndege? Je ni kweli kwamba tunathamini zaidi maendeleo ya vitu kuliko maendeleo ya watu? Hoja hii inapaswa kujibiwa kwa hoja, sio kusema wapinzani wanapinga kila kitu.
[HASHTAG]#Tatu[/HASHTAG]; watu wanahoji kwanini ndege zinunuliwe na serikali na sio ATCL kuwezeshwa ili ijiendeshe yenyewe? Rais hajaiwezesha ATCL kujitegemea. Anachofanya ni serikali kununua ndege kisha kuikodishia ATCL. Yani ndege zote 4 zilizonunuliwa hadi sasa, hakuna hata moja inayomilikiwa na ATCL. Zote zinamilikiwa na serikali then ATCL wanakodi kufanyia biashara.
Mfumo huu hauwezi kuwa na tija. Kwa sababu kama ni kukodisha ndege, ATCL wangeweza kukodi mahali pengine, sio lazima wakodi ndege za serikali. Hoja ya watanzania ni ATCL kumiliki ndege zake yenyewe, sio kukodisha ndege. Kwanini serikali inunue ndege then ATCL wakodi? Kwani walishindwa kukodi kwingine?
Kuilazimisha ATCL kukodi ndege za serikali ni kuongeza gharama za uendeshaji, kwa sababu ATCL watalazimika kupandisha bei ili wapate fedha za kuilipa serikali na wabaki na faida. Vinginevyo watajiendesha kwa hasara, kama ambavyo imeanza kujitokeza, ambapo mwaka jana na mwaka juzi wamepata hasara ya zaidi ya bilioni 60 (kwa mujibu wa ripoti ya bunge).
Kwahiyo ili kuondoa hasara hiyo, ingekuwa busara ndege hizo kumilikiwa na ATCL moja kwa moja. Yani serikali ingenunua ndege hizo na kuipa ATCL izimiliki moja kwa moja, au serikali ingewapa fedha ATCL wanunue ndege wenyewe ili waweze kuzimiliki.
Vinginevyo shirika hili litajiendesha kwa hasara maradufu kuliko ilivyokuwa awali. Kwa sababu katika mapato ya ATCL italazimika kupata fedha za kumlipa mmiliki wa ndege (serikali), kukidhi gharama za uendeshaji, kisha ibaki na faida. Hii ni ngumu sana hasa kwa kuwa soko la ATCL bado lina ushindani mkubwa kwa makampuni mengine ya ndege yaliyopo.
[HASHTAG]#Nne[/HASHTAG]; ni kuhusu serikali kufufua shirika la ATCL. Kufufua kitu means kitu kilikuwepo lakini kikafa/kuuawa. Kabla ya kupongeza JPM kufufua ATCL ni muhimu kujiuliza nani aliyeiua? Swali hili ni muhimu kwa sababu litasaidia isife tena.
Ukweli ni kwamba Serikali hii hii (ya CCM) inayosifiwa kufufua ATCL ndio iliyoua shirika hilo. Shirika la ndege la taifa (wakati huo likiitwa ATC) lilianzishwa mwaka 1977 baada ya kuvunjika kwa shirika la ndege la Afrika Mashariki, East African Airways (EAA).
Mpaka kufikia mwaka 1994 ATC ilikuwa na jumla ya ndege 8 kubwa na za kisasa. Ndege tatu kati ya hizo tulizitaifisha kutoka EAA, na nyingine tulinunua. Zilikuwepo ndege 8 aina ya Boeing 737, Boeing 747 SP, Airbus A320, Boeing 737-500 etc. Hizi zilikuwa ndege kubwa, bora na za kisasa.
Katika picha hizi nilizoambatanisha hapa chini utaona ndege mbalimbali za ATC wakati huo zikiwa ktk safari zake. Picha ya kwanza kulia ni nege ya ATC ikiwa imepaki uwanja wa ndege wa Frankfurt nchini Ujerumani mwaka 1994, na picha ya 3 kushoto ni ndege ya ATC aina ya Boeing 737 ikiwa imepaki uwanja wa ndege wa kimataifa wa Oliver Tambo, SA mwaka 2006.
Kwahiyo sio kweli kwamba hatujawahi kuwa na ndege kama wachache wanavyojaribu kupotosha. Tulikuwa nazo nyingi na nzuri na zilifanya safari za kimataifa, lakini serikali hiihii ya CCM inayosifiwa leo ikazifilisi na kuua shirika. Watu walewale waliouwa ATCL ndio haohao wanaosifiwa kufufua shirika hilo leo. Futuhi.!!
Mwaka 2002 serikali iliingia mkataba (wa kijinga) na shirika la ndege la Afrika Kusini (SAA) wa dola milioni 20, na kuiwezesha SAA kumiliki 49% ya mali za ATC zikiwemo ndege. Dola milioni 20 ni kama shilingi bilioni 45 za kitanzania. Kwahiyo kwa Bilioni 45 tu SAA wakamiliki 49% ambayo ni kama nusu ya mali zote za ATC. Hapa ndipo jina lilipobadilishwa kutoka ATC kuwa ATCL.
Lengo la kuingia ubia na SAA ilikuwa kujaribu kuona kama tutapata faida kwa sababu ATC ilikuwa ikijiendesha kwa hasara sana wakati huo. Lakini baada kufunga "ndoa" hiyo hasara ikawa maradufu. Kufikia mwaka 2005 tukawa tumepata hasara ya dola milioni 19 (kama shilingi Bilioni 40 hivi) ndani ya miaka mitatu tu. Yani tuliuza shirika kwa Bilioni 45 halafu baada ya miaka mitatu tukapata hasara ya Bilioni 40. Biashara kichaa.!!
Mwaka 2006 tukashindwa kuendelea na mkataba huo. Tukauvunja. Kilichotokea wengi mnajua. Baadhi ya ndege zetu zilizuiwa na SAA kufidia hasara. Waliosababisha hasara hiyo hawajawahi kuwajibishwa wala kuchukuliwa hatua zozote za kisheria.
Leo taifa zima linashangilia Boeing 1 na kuimba mapambio ya kuabudu kana kwamba hatujawahi kuwa na ndege kabisa, kumbe tulikuwa na Boeing nyingi za kisasa. Serikali ileile iliyoua ATCL na kufilisi ndege zote 8 zilizokuwepo ndio hiohio inayosifiwa kwa kununua ndege moja. Nimekumbuka kauli ya Mwalimu Nyerere aliyowahi kusema ujinga ni kuibiwa madini ukapewa kichupa halafu ukaondoka ukishangilia kama zuzu.
Mwaka 1994 wakati ATCL ikiwa na Boeing 8, shirika la ndege la Kenya Airways ilikuwa na Boeing 4 tu ambapo mbili zilikuwa za kukodi. Lakini leo miaka 24 baadae, Kenya Airways wana Boeing 25 sisi tumenunua Boieng moja taifa zima linasifu na kuabudu. What a shame?? Lazima tujiulize tumefikaje hapa.
Anayestahili kupongezwa katika juhudi hizi ni Rais JPM, sio serikali ya CCM ambayo ilishiriki kuua ATCL. Lakini pamoja na pongezi hizo ni muhimu ashauriwe namna bora ya kufufua shirika hilo ili yasije yakajitokeza yaleyale yaliyosababisha likafa. Nchi hii ni yetu sote, hakuna mwenye haki zaidi kuliko mwingine. Watu wanapohoji wasikejeliwe au kujibiwa kwa mipasho, wajibiwe kwa hoja. Tukosoane, tushauriane, tuelimishane kwa maslahi ya taifa. Kwa pamoja tuijenge nchi yetu.!
Malisa GJ