Ukweli ni kwamba Clouds Media na project zao matumbo yanawaka moto na vichwa kuwauma kwa ujio wa Wasafi Media

Media ni content na sio kelele kelele..
Inategemea na wasikilizaji wanataka nini. Tanzania wasikilizaji wanataka vituko vituko. Yaani vitu ambavyo wewe utaviona vya kijinga wao ndo wanavyotaka.
 
Upande wa yamoto aliyekuwa anajulikana ni aslay pekee ila baada ya mboso kujiunga na wasafi nyota yake imewaka na Hadi sasa kumfunika aslay.Nafikiri jamaa atakuwa si mfuatiliaji wa mziki vizuri we mvumilie tu.
If u ask me mbosso na aslay aslay bora ila mbosso kafanikiwa technically .same goes with mond vs kiba
 
Yaani a 2 year old media ipambane na 21 years old media?

Haiwezekani
Wakuu amani iwe pamoja nanyi!!

I hope wote tuwazima wa afya tele!!

Kama heading inavyojieleza hapo juu
Tanzania imejaariwa kuwa na media nyingi sana,na kuna baadhi ya media house zili-dominate katika kipindi fulani.

Mfano kipindi hicho sahara media group,Ipp media na Tbc enzi hizo,
Media House hizo ziliishika Tanzania kwa nyakati hizo,kulingana na mahitaji ya wasikilizaji(aina ya wasikilizaji ikizingatiwa.

Baadae zikaja media nyingine kama Cloud's fm ambayo imejijenga vyema kwa kipindi cha miaka 20 na kufanikiwa ku-cover tz yote na kudominate,na hata kuanza kufungua branches abroad mf Rwanda.

Kwa muda sasa Cloud's imetawala on top kama Super brand,na wanastahili hio heshima maana wamepigana sana kufika hapo,tofauti na media nyingine za zamani zilizoanza na mitaji mikubwa.

Na ili media itawale kwa kipindi fulani inategemeana na Aina ya wasikilizaji,mahitaji ya jamii hiyo kwa wakati huo,ubora,ubunifu,kujituma na kuipenda kazi zao kwa upande wa watangazaji,ikiwepo maslahi bora,uwekezaji mzuri upande wa facilities mfano,technology ,studio nk.

Sasa Cloud's wanadominate lakini mpaka sasa alarm kwenye vichwa vyao inawafanya wapagawe kwa kasi ya ukuaji wa wasafi media,maana ikiwa bado wasafi media hasa redio haijacover tz nzima lakini ni radio au media inayozungumziwa sana hapa bongo sambamba na clouds.

Wasafi media imetake over social media hapa bongo pamoja na ndugu zao wa wcb wasafi na si social media tu hata you tube ndio media yenye subscribers wengi hapa tz ikiziacha nyingine mbali ,na hata mwaka haijamaliza,je ikifikisha miaka 3 na kucover atleast nusu ya tz itakuwaje?

Ni kweli hata E-fm walianza nao kwa speed lakini hawakufikia hapa walipo wasafi na hata mikoani walikuwa hawajulikani kabla ya kulaunch masafa yao,lakini wasafi vijana wengi wana-wish iwafikie mkoani kwao mapema.

Ukija upande wa matamasha ya burudani,Efm walijaribu kuwachallenge Cloud's wameshindwa na saizi naona wameungana na clouds,ila naona wasafi wako serious na utaona ndani ya muda mfupi washafanikiwa kuwaumiza vichwa Cloud's fm,na wasafi festival ndio tamasha ambalo limekuwa na sponsor's wengi hapa tz kwa mwaka wa pili mfululizo,hiyo ina maanisha ni brand inayokubalika kwa watu.

Na kwasasa Wasanii hawana tena pressure ya kusubiri fiesta tu au kuwanyenyekea Cloud's tu naona hilo linaenda kuisha na unaweza kuona wasafi festival dar es salaam,list ya wasanii ni kama haijaacha msanii,maana karibu wasanii wote wako kwenye list,hii inafanya fiesta itakapofanyika dar es salaam either watafute wasanii wengine au wawarudie watakaoperform wasafi festival,(na naona wanazidi kupunguza entrance fee kwenye show zao kutoka 10000 hadi 5000?),jambo ambalo linaweza kupunguza mvuto wa tamasha lao na hili linawatisha.

Naamini baada ya miaka 5 endapo wasafi festival,media na wcb wakiwa bado wana trend na clouds kubaki na pace hii ya sasa ya kurukiarukia vitu Mfano,harmonize issue basi Cloud's wajiandae kuachia nafasi pale juu,maana now ndio kwanza ngoma mbichi na wasafi haijaanza kufika mikoani hila uko social media speed yao ni 120 na youtube washapiga bao.

Upande wa Wasafi TV nadhani iko wazi kuwa now ndio channel pendwa kwa vijana wengi,ukitembelea sehemu nyingi na hata maeneo ya starehe jamaa wanatawala,na sasa wanapatikana katika ving'amuzi vyote ikiwepo dstv across Africa.

Mimi kama mdau wa burudani na competition nimetulia tuli najihesabia point katika hii fight then nitakuwa nakuja na matokeo kila baada ya round.
 
Wasaf nachowapendea hawabagui na pia wanakumbuka wakongwe sema pana baadhi ya wasanii wanaogopa kushiriki wasaf festival wakiona clouds ndio ilowatoa wakishiriki itakua wanasaliti
 
Wasaf nachowapendea hawabagui na pia wanakumbuka wakongwe sema pana baadhi ya wasanii wanaogopa kushiriki wasaf festival wakiona clouds ndio ilowatoa wakishiriki itakua wanasaliti
Bas hao wasanii watakuwa ni wajinga na wasiojitambua Kuna msemo mmoja unasema uoga wako ndio umasikini wako mbona jux kafanya show wasafi festival na baada ya hapo akafanya show ya fiesta Tena atafanya pia wasafi festival ya tarehe 9.
 
Wewe Acha kufananisha mbosso wa yamoto na wa wcb wasafi,
Kule alikuwa underground sana tu
Bora aslay.
Ndio nyie mnaosema harmonize alitolewa na bongo star Search.
Utajua wewe lakini mbosso kapita kwenye mikono ya clouds hiyo ndio point ya msingi alikuwa maarufu hakuwa maarufu Mimi hiyo hainihisu
 
Wasaf nachowapendea hawabagui na pia wanakumbuka wakongwe sema pana baadhi ya wasanii wanaogopa kushiriki wasaf festival wakiona clouds ndio ilowatoa wakishiriki itakua wanasaliti
Sio kwamba wanakumbuka sana wakongwe hapana wasanii wanaohit kwa sasa hawawezi kwenda wasafi kwasababu wanaogopa kubaniwa na clouds pili nguvu na ushawwishi alionao diamond in mkubwa so hata wakimchukua dudubaya na hadija kopa watu watakuja tu kwasababu ya diamond so mind hahitaji wakina marioo ili ajaze uwanja
 
Back
Top Bottom