Ukweli ni Kitu Gani?

Ukweli ni kitu gani? Ukweli uko wapi?

Je, ukweli ni hiki tunachokiona au tunachokisikia?
Je, ukweli ni kile tunachokihisi au tunachokigusa au kinusa? Ukweli ni kitu gani? Ukweli uko wapi?

Je, ukweli ni mafundisho au ni elimu? Au je, ukweli ni taarifa au ni habari? Ukweli ni kitu gani? Ukweli uko wapi?

Je, ukweli ni imani au ni matumaini? Au je, ukweli ni upendo au ni huruma? Ukweli ni kitu gani? Ukweli uko wapi?

Ukweli ni kuzaliwa au ni kuishi? Au je, ukweli ni kuugua au ni kufa? Ukweli ni kitu gani? Ukweli uko wapi?

Ukweli ni kujua au ni kufahamu? Au je, ukweli ni kuelewa au ni kujifunza? Ukweli ni kitu gani? Ukweli uko wapi?

Ukweli ni kuongea au ni kusema? Au je, ukweli ni kusimulia au ni kuhadithia? Ukweli ni kitu gani? Ukweli uko wapi?

Ukweli ni kuvumbua au ni kugundua? Au je, ukweli ni fikara au ni tafakuri? Ukweli ni kitu ganii? Ukweli uko wapi?

Ukweli ni Kanisa au ukweli ni madhehebu? ukweli ni kitu gani? Ukweli uko wapi?

Ukweli ni vikao au ukweli ni maazimio? Au je, ukweli ni taratibu, au ni sheria au ni kanuni? Ukweli ni kitu gani? Ukweli uko wapi?

Ukweli ni kipi; ni kile kinachothibitika au ni kile kinachodhihirika? Ukweli ni kitu gani? Ukweli uko wapi?

Je, ukweli ni nadharia au ukweli ni vitendo? Au je, ukweli ni mawazo au ni maoni? Ukweli ni kitu gani? Ukweli uko wapi?

Ukweli ni upi; ni usanifu, ni ujuzi, ni utalaamu, ni ubunifu, ni uzoefu, ni taaluma au ni maarifa? Au je, ukweli ni maisha au ni kuishi? Ukweli ni kitu gani? Ukweli uko wapi?

Ukweli ni mwili unaonekana au ni akili isio onekana; wala kushikika? Au je, ukweli ni nguvu au ni nishati? Ukweli ni kitu gani? Ukweli uko wapi?

Ukweli ni upi, ni ndoa au ni tendo la ndoa? Au je, ukweli ni mapenzi au ni ngono? Ukweli ni kitu gani? Ukweli uko wapi?

Ukweli ni upi; ni ulimwengu au ni mbingu? Au ukweli ni asili au ni uhalisia? Ukweli ni kitu gani? Ukweli uko wapi?

Ukweli ni upi; ni wema au ni uzuri? Au je, ukweli ni maadili au ni miiko? Ukweli ni kitu gani? Ukweli uko wapi?

Ukweli ni upi: ni mlango wa kushoto au ni mlango wa kulia? Ukweli ni kitu gani? Ukweli uko wapi?

Ukweli ni upi: ni mabadiliko au ni mageuzi? Ukweli ni kitu gani? Ukweli uko wapi?

Ukweli ni upi: ni ufanisi au ni unafuu? Au ukweli ni ubora? Ukweli ni kitu gani? Ukweli uko wapi?

Ukweli uko wapi; uko nyumbani, au uko shuleni? Au je, ukweli uko Kanisani au uko msikitini; au uko kwenye jamii? Ukweli ni kitu gani? Ukweli uko wapi?

Ukweli uko wapi: uko kwenye ubongo au uko kwenye milango mitano ya fahamu: masikio, pua, macho, ulimi au ngozi? Au je, ukweli uko kwenye viungo vingine vya mwili? Ukweli ni kitu gani? Ukweli uko wapi?

Ukweli uko wapi: uko kwa watawala au viongozi; au uko kwa watawaliwa? Ukweli ni kitu gani? Ukweli uko wapi?

Ukweli ni roho au ukweli ni nafsi? Roho iko wapi? Nafsi iko wapi? Ukweli ni kitu gani?

Ukweli ni furaha au ni amani? Au je, ukweli ni utulivu au ni usikivu; au ni unyenyekevu? Ukweli ni kitu gani? Ukweli uko wapi?

Ukweli ni upi; ni kile kisichosababisha uchungu au ni kile kisichosababisha uharibifu? Ukweli ni kitu gani? Ukweli uko wapi?

Ukweli ni kitu gani? Ni usawa au ni haki? Ni wajibu au ni majukumu? Ukweli uko wapi?

Ukweli ni upi: ni maendeleo au ni mafanikio? Ukweli ni kitu gani? Ukweli uko wapi?

Ukweli ni makubaliano yaliyopo kati ya vitu vitatu:

1. -- kitu tunachokifikiria
2. -- wazo juu ya kitu tunachokifikiria
3. -- maneno tunayotumia kuongea juu ya kitu tunachokifikiria

Hii ni pembetatu ya kisemantiki.

Kitu kinachoongelewa na kufikiriwa aghalabu kiko nje ya kichwa cha mtu anayefikiri.

Wazo liko katik kichwa cha mtu anayefikiri

Na maneno yako mdomoni mwa mtu anayeongea.

Nimejibu kulingana na nadharia ya kiepistemolojia iitwayo nadharia ya makubaliano ya kisemantiki.

Yaani 'correspondence theory of truth'

1618355514091.png
 
Ukweli ni kitu gani? Ukweli uko wapi?

Je, ukweli ni hiki tunachokiona au tunachokisikia?
Je, ukweli ni kile tunachokihisi au tunachokigusa au kinusa? Ukweli ni kitu gani? Ukweli uko wapi?

Je, ukweli ni mafundisho au ni elimu? Au je, ukweli ni taarifa au ni habari? Ukweli ni kitu gani? Ukweli uko wapi?

Je, ukweli ni imani au ni matumaini? Au je, ukweli ni upendo au ni huruma? Ukweli ni kitu gani? Ukweli uko wapi?

Ukweli ni kuzaliwa au ni kuishi? Au je, ukweli ni kuugua au ni kufa? Ukweli ni kitu gani? Ukweli uko wapi?

Ukweli ni kujua au ni kufahamu? Au je, ukweli ni kuelewa au ni kujifunza? Ukweli ni kitu gani? Ukweli uko wapi?

Ukweli ni kuongea au ni kusema? Au je, ukweli ni kusimulia au ni kuhadithia? Ukweli ni kitu gani? Ukweli uko wapi?

Ukweli ni kuvumbua au ni kugundua? Au je, ukweli ni fikara au ni tafakuri? Ukweli ni kitu ganii? Ukweli uko wapi?

Ukweli ni Kanisa au ukweli ni madhehebu? ukweli ni kitu gani? Ukweli uko wapi?

Ukweli ni vikao au ukweli ni maazimio? Au je, ukweli ni taratibu, au ni sheria au ni kanuni? Ukweli ni kitu gani? Ukweli uko wapi?

Ukweli ni kipi; ni kile kinachothibitika au ni kile kinachodhihirika? Ukweli ni kitu gani? Ukweli uko wapi?

Je, ukweli ni nadharia au ukweli ni vitendo? Au je, ukweli ni mawazo au ni maoni? Ukweli ni kitu gani? Ukweli uko wapi?

Ukweli ni upi; ni usanifu, ni ujuzi, ni utalaamu, ni ubunifu, ni uzoefu, ni taaluma au ni maarifa? Au je, ukweli ni maisha au ni kuishi? Ukweli ni kitu gani? Ukweli uko wapi?

Ukweli ni mwili unaonekana au ni akili isio onekana; wala kushikika? Au je, ukweli ni nguvu au ni nishati? Ukweli ni kitu gani? Ukweli uko wapi?

Ukweli ni upi, ni ndoa au ni tendo la ndoa? Au je, ukweli ni mapenzi au ni ngono? Ukweli ni kitu gani? Ukweli uko wapi?

Ukweli ni upi; ni ulimwengu au ni mbingu? Au ukweli ni asili au ni uhalisia? Ukweli ni kitu gani? Ukweli uko wapi?

Ukweli ni upi; ni wema au ni uzuri? Au je, ukweli ni maadili au ni miiko? Ukweli ni kitu gani? Ukweli uko wapi?

Ukweli ni upi: ni mlango wa kushoto au ni mlango wa kulia? Ukweli ni kitu gani? Ukweli uko wapi?

Ukweli ni upi: ni mabadiliko au ni mageuzi? Ukweli ni kitu gani? Ukweli uko wapi?

Ukweli ni upi: ni ufanisi au ni unafuu? Au ukweli ni ubora? Ukweli ni kitu gani? Ukweli uko wapi?

Ukweli uko wapi; uko nyumbani, au uko shuleni? Au je, ukweli uko Kanisani au uko msikitini; au uko kwenye jamii? Ukweli ni kitu gani? Ukweli uko wapi?

Ukweli uko wapi: uko kwenye ubongo au uko kwenye milango mitano ya fahamu: masikio, pua, macho, ulimi au ngozi? Au je, ukweli uko kwenye viungo vingine vya mwili? Ukweli ni kitu gani? Ukweli uko wapi?

Ukweli uko wapi: uko kwa watawala au viongozi; au uko kwa watawaliwa? Ukweli ni kitu gani? Ukweli uko wapi?

Ukweli ni roho au ukweli ni nafsi? Roho iko wapi? Nafsi iko wapi? Ukweli ni kitu gani?

Ukweli ni furaha au ni amani? Au je, ukweli ni utulivu au ni usikivu; au ni unyenyekevu? Ukweli ni kitu gani? Ukweli uko wapi?

Ukweli ni upi; ni kile kisichosababisha uchungu au ni kile kisichosababisha uharibifu? Ukweli ni kitu gani? Ukweli uko wapi?

Ukweli ni kitu gani? Ni usawa au ni haki? Ni wajibu au ni majukumu? Ukweli uko wapi?

Ukweli ni upi: ni maendeleo au ni mafanikio? Ukweli ni kitu gani? Ukweli uko wapi?
Ukweli ni maelezo yanayoelezea tukio lililotokea au lililowahi kutokea sawasawa kabisa na namna lilivyokea. Kwa mfano, kama juzi niliwahi kupita shambani kwa Mzee Ibrahim Chande halafu nikaiba maembe shambani humo, halafu kesho yake tena nikakutana na rafiki yangu Mzee Kizito nikamweleza kuwa "Jana nilipita shambani kwa Mzee Ibrahim Chande na niliiba maembe", huo ndiyo ukweli, na maelezo mengine yoyote yale kinyume na taarifa hizi ndiyo uongo
 
Ukweli ni makubaliano yaliyopo kati ya vitu vitatu:

1. -- kitu tunachokifikiria
2. -- wazo juu ya kitu tunachokifikiria
3. -- maneno tunayotumia kuongea juu ya kitu tunachokifikiria
Nikiri, katika kufuatilia mambo kwenye hili jukwa, wewe ni mtu unaefuatilia mambo msingi.

Maandishi yako yanafundisha na kufanya ye yote anaetafuta kujifunza atazame upya katika yale anayoyaelekea.

I appreciate you!
 
Naomba niongezee kwenye hizi hoja za Mama Amon kama ifuatavyo
1. -- kitu tunachokifikiria- na kukisema kwa wengine sawasawa na vile tunavyokifikira
2. -- wazo juu ya kitu tunachokifikiria
3. -- maneno tunayotumia kuongea juu ya kitu tunachokifikiria

Na kukisema (kitu), na kuyasema (mawazo/ maneno) kwa wengine sawsawa na vile tunavyokifikira kichwani mwetu
 
ni neno la Kiarabu linalotokea katika Quran, kihalisi linamaanisha "ubinafsi", na limetafsiriwa kama "psyche"
Wasiwasi wangu ni tafsiri hii "psyche".

"Nafsi" ni neno la kiarabu lilotafsiriwa kutoka neno la kilatini "persona."
 
Ukweli ni hali ya kuishi au kutenda mambo au jambo kwa uwazi, uaminifu na imani kadiri ya taratibu na sheria za utu binafsi,mazingira na/ au jamii iliyokuzunguka.
 
Usipende kujipa mzigo wa kitu kidogo kuumiza watu ufahamu au kujitesa wewe kiufahamu kwanini usiulize uwongo ni nini kabla ya ukweli uwezi ukafanya kitu kwa usawa pasipo kupitisha katika pande mbili zoelefu mbali na ya tatu kwa mapana ukweli unahusika atika vitu na visivyo vitu penye hewa na pasipo na hewa penye kiza na palipo na mwanga hakuna ukweli pasipo na uongo na hakuna uongo pasipo na ukweli ili ukweli upatikane lazima uongo uwepo na ili uongo upatikane lazima pawepo na ukweli uwezi uliza ukweli ni nini wakati hujahusisha uongo nenda kadadisi mengine ndipo ujuzwe vizuri.
Ninaona katika maelezo yako "kuchanganya" mambo.

Kuna maumbile. Kwa mfano, usiku na mchana, giza na mwanga. Hii ni asili; asili imefanya hivyo.

Swali. Kwa mujibu wa maelezo yako, unaona "asili" amefanya uwongo na ukweli?
 
Back
Top Bottom