Ukweli ni kitu gani?

MIXOLOGIST

JF-Expert Member
Mar 1, 2016
12,655
31,422
Habari wana JF

Wakati tunaelekea mwisho wa mwaka kwenye msimu wa sikukuu nimejaribu kutafakari peke yangu hili jambo tajwa hapo juu (ukweli ni kitu gani?) bila mafanikio. Msingi wa tafakari yangu unatokana na maandiko matakatifu (biblia agano jipya) ambapo Yesu aliulizwa na Pilato je ukweli ni kitu gani? Bahati mbaya muandishi hakueleza kama Yesu alijibu na jibu lake lilikua ni lipi? (kwa wale wenye uelewa zaidi ya huu watanijuza pia).

Kwa kutumia uwezo wangu nimejaribu kujiuliza hili swala muda mrefu sana nisipate jibu lake. Mara nyingine utaona watu wanabishana na kila mmoja ana amini anachosema ni cha ukweli, sasa hapo shida ndipo inapoanza ukweli ni upi sasa?

Tafsiri ya kwanza inaweza ikawa, ukweli unaweza ukawa ni maneno au jambo analolisema mtu amabalo analoliamini na yuko tayari kulishuhudia lakini linaweza likawa sahihi au siyo sahihi. Ni nini basi kinachoamua usahiii wa jambo? mara nyingi ni imani (dini au mila), mapokeo, maono (jinsi lilivyoonwa) na mazoea. Hali kadhalika imani, mapokeo, maono na mazoea yanaweza yakawa na tafsiri tofauti kati ya waumini wa imani moja na nyingine, au jamii moja na nyingine au mtazamaji mmoja na mwingine.

Kwa maana hiyo basi jambo moja linaweza likawa na tafsiri zaidi ya moja kulingana na imani, maono, mapokeo na mazoea. Kwa mustakabali huo basi, ukweli ni kitu gani? je kuna ukweli mmoja (universal truth) au kuna various versions of truths? YOUR TRUTH, MY TRUTH AND THE TRUTH, Naomba kujuzwa.
 
Ukweli ni kitu chenye uthibitisho,uhakika,kitu kisicho mashakamashaka(dhahiri).
kwenye swala la imani kuna tatizo hili kuamini kwanza kuelewa baadae!!
unatakiwa uelewe ndo uamini na ndio maana wengi wao wanapelekwa pelekwa
tu.
Kwa tafsiri yako imani zote za dini siyo ukweli, kwa maana zinazungumza mambo mengi yasiyoweza kuthibitishwa, kama vile maisha baada ya kifo, uwepo wa Mungu, na dhana ya dhambi
 
Back
Top Bottom