Ukweli ni kitu gani?

katika swala zima la ukweli ni umbo lenye pande Sita three dimension sasa hatuwezi kuwe sawa ingawa wote tutakua wakweli Aliyeona juu hatajua chini Kuna nn na aliuona chini hatajua mbele na vitu mfano Wa hivyo usishangae leo hii watu wanne walioshuhudia tukio moja kila mtu akija na stori yake na inawezekana wanabishana na ngumi zikapigwa
Ngumi Tena 😂😂😂🤣🤣🤣hapo sasa
 
Hakuna ukwel wala uongo , mambo yote yapo kma yalivyo ni wewe tu ufanye uamuzi ufate lipi uache lipi na hizi ni kanuni za maumbile.
 
Ukweli ni Kujua na kutambua hali halisi na kutoa utata wa sintofahamu. Knowing, casying the shadow of doubt, replacing belief with knowledge.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kweli kinyume cha Uwongo. Biblia imesema Mungu ni Kweli na Shetani ni Baba wa Uwongo. Yesu alisema yatupaswa kumuabudu Mungu kwa Njia ya Roho na Kweli. Kuijua kweli lazima tupate picha halisi ya Uwongo kwani kinyume chake cha Uwongo ndio Kweli. Kwa mfano nikikuuliza jee unajua rangi ya Kinyonga? Hakuna anaeijua Rangi halisi ya Kinyonga kwani inabadilika kila inapotokea hali ya mabadiliko ya mazingira yanayo mzunguka.

Kutokuwa halis, na kubadilika ndio tunaita hali ya uwongo. Haijalishi madailiko hayo ni ya muda mfupi au mrefu ilimradi kuna uwezekano wa kutokea mabadiliko ya aina yeyote ile au mabadiliko ya msimamo basi huo ni uwongo.

So long jiwe linaweza kubasilika na kuwa kokoto likilipuliwa na baruti basi nalo sio halisi ni uwongo, au chuma hakikuwa kilivyo kimebadilika kutoka Iron ore basi sio halisi ni uwongo, mbao ilikuwa mti, ambao ulikuwa kambegu kaliko jipanda aridhini na kuvyoza virutubisho udongo hivyo sio halisi ni uwongo.

Kwa utambuzi wetu twaona kuwa vitu vyingi vina hali ya kweli wakati sio. Mfano hali ya maji, maji yana hali ya kimiminika, lakimi ukiyaweka kwenue jokofu yanaganda na kuwa barafu, ukiyachemsha yanapata moto, na joto likipanda ya kuwa mvuke na kukauka. Kama rangi ya kinyonga maji hali ya maji hubadirika hivyo ni hali ya uwongo.

Ukweli ni ile hali kuwa bila mabadiliko ya aina yeyote katika hali yeyote, kwa jua, kwa mvua, au kwa muda, au mahali uliopo ni hali ya milele. Ukweli uko kama ulivyo sasa, kabla ya sasa, na baadae, Ukweli ni hali ya umilele.

Kweli ni Uhai na Uwongo na Maumbile yake.

Binadamu ana nafsi mbili, ananafsi ya kweli ambayi ni Roho na nafsi ya uwongo ambayo ni Mwili. Roho haina mwanzo wala mwisho, lakini mwili una mwazo na mwisho, unakua na kuzeeka, unazaliwa na kufa.

Ndio maana YESU anataka tumwabusu Mungu kwa Njia ya Kweli yaani Kwa Roho zetu kwa Mungu Roho.

Kila unachokiona, unachokitamani kukipata, kula, kunywa, kuzini au kufurahi nacho ni vyo uwongo. Hivyo vinakinaisha, havikidhi matarajio, haviridhishi.
 
Japo hiyo quotation yako kutoka Bible ni tata, haina uthibitisho kupitia kifungu, ila

Ukweli ni hali ya nafsi kujirizisha pasipo na shaka.
 
Ukweli ni uhalisia wa jambo jinsi lilivyo bila kuongeza wala kupunguza. Ni habari au taarifa ya kitu au jambo lilivyo tendeka.
Kila kitu au jambo uliloona, kusikia na hata kuadithiwa linaukwe halisi.
Ukweli halisi na ikiwa uhalisia wa jambo haupo, huo si ukweli ni uongo.
Kwa hali ya kusikitisha, wengi tunashindwa kuelewa tofauti kati ya UKWELI na IMANI.
UKWELI ni mambo ambayo tayari yamefanyika na kuthibitishwa.
IMANI ni mambo ambayo hutarajia kufanyika.
Lakini ikumbukwe kwamba Imani inajengwa na mambo ambayo tayari yamefanyika. Ni lazima mambo yaliyo fanyika na kuthibitishwa (UKWELI) yatangulie ili upate uhakika wa a mambo yajayo (IMANI).
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom