Ukweli ni kama ndevu hata ujitahidi vipi kuzinyoa iko siku zitaonekana

CalvinKimaro

JF-Expert Member
Sep 11, 2017
244
312
Kama Peer Reviewer nimebahatika kuipitia report ya Global Political Outlook 2019; report itolewayo kila mwaka na UN.

Katika EXECUTIVE SUMMARY ukurasa wa 2 report inasema hivi: "Tanzania imeendelea kuwa na uimara wa kisiasa kwa nchi za Afrika Kusini mwa jangwa la Sahara. Tanzania haijakumbwa na mitafaruku ya kisiasa kutokana na misingi imara ya kisiasa na kijamii iliyojengwa kwa kipindi cha miaka takribani 20 baada ya kupata Uhuru mwaka 1961. Hakuna dalili zozote kuwa Tanzania itashuhudia machafuko ya kisiasa na mparaganyiko wa kijamii katika kipindi kifupi kijacho".

Katika ukurasa wa 22 report inasema hivi: "bado Tanzania haijafanikiwa kupata vyama vya upinzani vilivyo makini na vyenye kuvutia raia wengi nchini. Aidha vyama vilivyopo vimeshindwa kushawishi jamii ya kimataifa kuviunga mkono kutokana na sababu mbalimbali zikiwepo za matumizi mabaya ya rasilimali, siasa zisizo na tija kimataifa na uimara wa diplomasia ya Serikali ya Tanzania kimataifa. Katika kipindi cha kuandaa report hii misaada toka jamii ya kimataifa ilipungua kwa asilimia zaidi ya 70 kwa taasisi za kisiasa nchini Tanzania". Mwisho wa kunukuu.

Kwa report hii ambayo itawasilishwa rasmi katika kikao kifuatacho cha UNGASS (UN General Assembly) nimeanza kupata picha ni kwa nini CHADEMA(Chama Cha Maendeleo na Demokrasia) imeamua kususa uchaguzi huu. Suala kubwa hapa linaweza kuwa ni kukosa fedha za kuendesha kampeni. Kuna mtu au kikundi cha watu alipanga kuvuruga ili kuepusha aibu na kadhia ya kukosa fedha.

Kama hii ndio sababu kuu basi hata uchaguzi mkuu itakuwa hivihivi.

Ni vyema wenye CDM wakahoji kuhusu mapato na matumizi ya chama. La sivyo wajiandae kususa tena Oktoba 2020
 
Tulizoea Siasa za ulaghai

Amekuja Mzalendo Magufuli yeye ni kutenda Sio kuongea

Badilisheni aina ya siasa mnazofanya
 
Kimaro umekuja kitetea chama chenu cha wanywa mbege ,hivi kila mchaga lazima uwe chadema

State agent
 
CDM wakishiriki uchaguzi shidaa, wakijitoa ndio shidaaaaa zaidi. CCM mnataka nini?
 
Back
Top Bottom