Ukweli ni huu (kuusuta uwongo) utukufu na neema ya Zanzibar

aleesha

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
776
1,121
Mwenyezi Mungu amevipa visiwa hivi viwili yaani Unguja na Pemba bahati ya utukufu kwa kila jambo lake. Hayo yaliendelea tokea karne na karne mpaka pale ulipotendwa ufisadi wa taarikh 12 Januari 1964, ndipo neema na utukufu wa Zanzibar ulipoanza kutoweka.

Hapo tena, badala ya zumari kuwa likipulizwa Zanzibar, watu wa maziwani (Bara) walikuwa wakihemkwa, ikawa linapulizwa Bara, tuliopo visiwani tunahemkwa!

ZANZIBAR NA UBAGUZI KABLA YA MAVAMIZI
Nathubutu kusema bila ya wasiwasi wowote kuwa Zanzibar hakukuwepo ubaguzi wa namna yoyote kwa maana khasa na ya wazi ya neno UBAGUZI. Kwanza Wazanzibari ni watu waliochanganya sana damu hata sio rahisi kuweza kumtambua mtu kuwa ni mwenye kutokana na asili ya kabila fulani kwa kuangalia rangi yake au pua yake au masikio yake au kimo chake au kwa jina lake.

Jee, watu hao watabaguana namna gani? Malipo ya wafanyakazi serikalini yalikuwa hayakupangwa kiukabila. Wala serikali haikuwa na sehemu maalumu katika maskuli wala katika mahospitali kuwa zimetengwa kwa ajili ya watu wa makabila fulani.

Katika nchi za jirani zetu, Tanganyika, Kenya na Uganda kote huko kulikuwepo na ubaguzi uliyokuwa ukiongozwa na serikali za nchi hizo. Malipo ya mishahara ya wafanyakazi yalikuwa yakilipwa kutokana na makabila yao wala si kutokana na ujuzi wao wa kazi. Kulikuwepo "African Scale, Asian Scale na European Scale".

Madaktari, Mainjinia, Waalimu na wowote nawawe wana elimu na ujuzi na maarifa ya namna moja, yaani wote sawa sawa kwa elimu na ujuzi wa kazi zao, lakini mishahara yao ilikuwa tafauti kutokana na makabila yao.
Waafrika ndio wenye kulipwa malipo ya chini kabisa kuliko wote.

Wazungu walikuwa ndio wenye kulipwa mishahara minono (hata baadhi yao walikuwa hawana elimu yoyote isipokuwa huwo Uzungu wao), waliowafuatia ni Waasia. Vyoo vya njiani (Public Toilets) na sehemu za kungojelea usafiri wa reli navyo vile vile vilikuwa vikitumika kwa ubaguzi wa kikabila. Waafrika waliekewa vyoo vyao na sehemu zao za kungojelea usafiri.

Wazungu walikuwa na sehemu zao na Waasia walikuwa na sehemu zao, wote mbali mbali. Lilikuwa ni kosa na kuvunja sheria ikiwa imetokea kwa yoyote kuingia katika sehemu isiyo kuwa amekhusika nayo. Khasa Muafrika awe ameingia au amekaa katika sehemu za Waasia au za Wazungu.

Katika Tanganyika, Kenya na Uganda kote huko kulikuwa na Kodi ya Kichwa. Kodi hiyo ilikuwa ikilipwa na kila mtu aliyekwishafika balegh katika umri wake.
Nayo pia ikitekelezwa kwa njia za ubaguzi wa kikabila. Waasia na Wazungu, wao hata ikiwa wamechelewa kulipa kodi zao, basi walikuwa hawakamatwi majiani wala hawaendewi majumbani mwao kukamatwa. Lakini, Waafrika walikuwa wakisakwa majiani na wakiendewa majumbani mwao mnamo pinga pinga za usiku.

Na wakikamatwa, basi walikuwa wakifungwa kamba za viunoni au hufungwa ncha ya shati la huyu na la huyu kisha walikuwa wakiongozwa mmoja nyuma ya mmoja na huku wakipigwa mateke na kusukumwa mpaka wakifikishwa Bomani. Huko ikiwa hawatokuwa na cha kulipa basi walikuwa wakihukumiwa na kufungwa.

Kutokana na hali kama hizo, ndipo wengi kati ya wananchi wa nchi hizo, khasa kutoka Tanganyika walikimbia kutoka makwao na kuhamia Zanzibar kwa sababu ya kufuata hali njema za kimaisha. Zanzibar hakukuwepo kodi za kichwa wala ubaguzi wa vyooni wala malipo ya mishahara wala wa namna yo yote. Ilikuwa njema atakae naaje.

Pichani ni muarabu masikini kazi yake ni kinyozi, hapa anaonekana akimnyoa nywele muafrika angalau apate pesa chache ya chakula. picha hii imepigwa na A. C. Gomes kabla ya 1964.

itaendelea.....
 
Hao tuliokhabarishwa kuwa kulikuwa na mabwenyenye wa kiarabu waliokuwa wakimiliki biashara za watumwa na masetler wa mashamba makubwa ni kina nani hao?
Mabwana na watwana niulize tena, ni nani hasa hao? Washirazi na waarabu ngozi nyeupe, walikuwa wanaishi kwa hadhi gani enzi za utawala wa kisultan na biashara ya watumwa hadi mapinduzi ya 64?
Ukumbuke historia haichongwi.
Enzi za utawala wa awamu ya kwanza walichonga sana kupotosha historia za waasisi wa mapinduzi Zanzibar kutokana na siasa zao enzi hizo.
Jaribu kusoma kitabu kiitwacho "revolution in Zanzibar" uje na angalizo la kitabu hicho ili kuipa nyamanyama kidogo simulizi yako hii.
Vinginevyo nitakuona kama "team sultan".
 
Back
Top Bottom