Wakudadavuwa
JF-Expert Member
- Feb 17, 2016
- 17,506
- 15,999
Amani iwe kwenu wana JF!
Ni ukweli usiopingika Mbatia kaodhoofisha NCCR kwa tamaa ya Ubunge.Ni wakati sasa uachie chama kwa damu mpya ili chama kipate msukumo mpya.Safu kuu ya chama haifanyi kazi na nilishatoa wito kwa Kafulila na Machali kujenga chama na sio kutumia chama wakati wa uchaguzi.
Rafu ambayo inafanywa sasa na CHADEMA ni kuhakikisha chama kinapata idadi ya kura ili kupata ruzuku na ndio maana Anatropia Theonest aligawa kura kumwangusha Mtatiro.Lilikuwa ni agizo lililoratibiwa na John Mrema ambaye ni mkurugenzi wa shughuli za bunge.
Vita hii inachochewa na John Mrema ambaye ndiye aliyekuwa mgombea wa Chadema Vunja ni Lowasa ndiye aliyempa umeneja wa kampeni na kumsihi amwachie mbatia.Kwa upande mwingine kijana Henry Kilewo ameapa kumhujumu Mbatia kwani alisimamisha Mgombea wa NCCR Mwanga,ikumbukwe Kilewo alimrushia Mbatia matusi kipindi cha kampeni.
Hivyo kuelekea 2020 Chadema watasimamisha mgombea hata kama wakikosa ubunge basi wapate kura za ruzuku na viti maalum.Mwaka 2020 ni dhahiri Chadema hawatakuwa na Mgombea uraisi mwenye ushawishi hivyo John Mrema ambaye alibwagwa vibaya 2010 na Augustine Mrema ni lazima wamnyofoe Mbatia ambaye pia kaapa kuendelea kugombea.Minyukano hii ni moja ya sababu UKAWA unasuasua.Ni maeneo mengi yameleta majeraha sugu.
Mbatia hao ndio Chadema wenyewe ruzuku kwanza na utapotea vibaya kwa uamuzi wako wa kuacha siasa za kitaifa na kukumbatia ufisadi.Hakika utapotea.
Nawasilisha.