Ukweli mtupu kuhusu mabadiliko yanayoendelea nchini chini ya uongozi wa Rais Magufuli

ndege JOHN

JF-Expert Member
Aug 5, 2015
19,544
44,690
Yako mambo ambayo watanzania wanayajua wote humu ndani tunatambua yafuatayo kuhusu ukweli wa mabadiliko toka aingie Rais Magufuli. Ila kwa sababu tofauti kila mtu amekuwa na mtazamo wake...

1. Wote humu ndani tunajua toka aingie Rais Magufuli hakuna kesi kubwa za ufisadi kama miaka ile ya nyuma skendo nyingi za ufisadi.Sasa zimepungua tunaendelea kushuhudia vigogo wakibanwa.

Watanzania wa hali ya kawaida walio wengi walikuwa wakikerwa na vitendo vya rushwa huku TAKUKURU imepewa nguvu sasa. Watanzania waliokuwa na uchungu na kupigwa kwa mabilioni wote wamefurahi sana.

2. Watanzania walikuwa hawafurahishwi na safari za vigogo ulaya zisizo na tija.Awamu ya tano imewabana viongozi hakuna tena safari za ovyo.
Watanzania hilo wanalijua na wamefurahi hata kama ni kimya kimya moyoni. Vijana wengi tu wanachama wa upinzani wamefurahi sana pesa haichezewi kwa matumizi ya ovyo


3. Vifo vya ovyo vimepungua sana hasa visa vya ajali kila siku.Kutokana na kuzuiwa viroba.Jamii kubwa ya watu watulivu wanaojielewa wamefurahi sana kuona serikali inajali vijana taifa lilikuwa linapotea siku hizi watu wanafanya maamuzi kwa kufikiria muda wote. Kumbe viroba vilikuwa vinatia mzuka wa ajabu mpaka wanafunzi . Binadamu yeyote wa Tanzania anayependa taifa liwe na maadili amefurahia uamuzi wa Serikali barabarani speed limit madereva wamekuwa na akili

4. Ukweli kuhusu vita ya madawa ya kulevya.Ishu ya Makonda najua wengi mtakuwa wanafiki kuzidi kunipinga lakini ukweli ni nuru na Mungu anafichua yaliyo moyoni. Makonda naweza kusema alikosea au hakukosea lakini alipokuwa anakwenda ni huku. Yale majina ya wauzaji madawa niya kweli lakini serikali imetumia busara sana kuamua.Kuacha kutangaza toka miaka ya mwanzo enzi ya Amina Chifupa itakumbukwa alitaka ajaribu kutaja majina. Ukweli ni kwamba wauzaji ni vigogo wanene lakini hutumia maagent.

Wapo wachungaji,viongozi kote mpaka upinzani.nani hajui kama leaders club lilikuwa chimbo la kuuza madawa.Kuna stori zinasema mpaka club za mpira hutumika.Makonda alikuwa anakwenda kasi sana.Lakini cha ajabu sana sijui nini kimetokea kwenye mioyo ya watanzania wa kawaida. Yaani nikashangazwa na jinsi upepo ilivyobadilishwa ikaonekana siasa.Mara Makonda ana beef na wauzaji, kweli inaingia akilini?

Lakini hayo mambo ya udaku yakawaingia mpaka jamii ya watu wa upinzani wakahisi kwamba kutajwa kwa mbowe kutaua chama kwamba inaua upinzani.

Lakini fact ni kwamba watu wengi wapenzi wa chadema mimi nawajua hata kama kiongozi mwingine akija pale bado watu wanakiamini sana chadema kwa kuwa kilikua na sera nzuri sana lakini sura za viongozi wakati mwingine zinatia mashaka. Mtanzania yeyote anajua siasa ni watu tu kama sisi wanagombania uongozi. Kuna watu humu mna akili na uwezo kuliko hata wanaogombeaga urais lakini mnajitoa ufaham mnawapa sifa kuzidi au mnawachafua mpaka kwa maneno ya uongo tena ya mitandaoni.

Hivi kweli muda ambao Rais anafanya kazi ofisi kuu mnadhani anakuwa na hulka ya ukali. Hapana ile ni ofisi lazima kuna maamuzi na mikataba inahitaj utulivi.magufuli mzee wa data vijana wengi wasomi wamependa sana kuwa na kiongozi msayansi. Rais Magufuli ni makini watanzania wanatembea na historia sote tunajua jinsi alivofanya kwenye mabarabara.

5. Kunufaika na miradi mikubwa.watanzania masikio hayana pazia hata kama utamkosoa kwa maneno elfu lakini serikali yake imeanza kutekeleza kwanza umeme unakuja umeme wa megawati 2000 yaani mara mbili ya huu reli ya kati kwa kiwango SGR.

Haya mambo yanafurahisha sana yaani itakuwa uchumi utakuwa sana kwanini sasa hata majirani zetu wasituonee wivu na wanaijua tanzania jinsi ilivyo kubwa na marasilimali nyingi ndo maana hata sera zetu zime influence sana hata siasa za East Africa. Ndo maana mnaona joto la uchaguzi. Inshort kila mtanzania anajua hili kwamba miaka michache ijayo tunaipiku kenya kwa uchumi.Tutarudi kuongoza huu ukanda. Haya nayosema ni mawazo ya watanzania wengi.

Japo kwa upande wangu habari kama hizi nazichukulia kama sio sifa kwa Magufuli bali ni kwa manufaa ya nchi na huu ndo wajibu wa serikali zile ni pesa zetu za kodi.Watanzania asilimia kubwa wanapenda kuona kila ukienda dukani unapewa risiti lakini hakuna maana mtu huna duka hufanyi biashara ukapenda kuona wafanyabiashara hawalipi kodi. Lakini ukweli ni kwamba watanzania wazalendo hasa vijana wanapenda kila mtu alipe kodi.

6. Hali ya usalama kuwa mbaya chanzo ni vikundi fulani. Kila mtu anayeijua Tanzania anafaham jinsi kulivyo na mitandao ya majambazi wenye silaha. Mfano mauaji ya kibiti. Kuna watu waliijaribu Serikali.sijui kwanini hawajatajwa wala wafadhili wake lakini kila mtu anajua magufuli hawezi kutoa amri ya kwenda kuua kisa sababu za kisiasa. Haingii akilini yaani Serikali nzima ya magufuli eti iamue kumuua lissu. Kwanini kwanza.yaani kwa sababu tu anaibua kashfa. Tuacheni utani kashfa ngapi zimesemwa.

Jamani amkeni pale kuna ishu nyingine ambayo mimi siijui lakini Ukweli uko kifuani waza kwa kutumia milango yote hakuna sababu za kumshtumu Magufuli kwamba anahusika kwanini kwanza kwa skendo ipi kubwa sana.

Naendelea
 
Back
Top Bottom