VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,135
- 17,802
Umekuwa msimamo wangu popote ninaposema au kuandika kuwa mwaka 2020 hakukuwa na uchaguzi mkuu. Kulikuwa na uchafuzi mkuu wa Tanzania. Kulikuwa tu na kutimiza lengo la kuwaondoa 'kivyovyote vile' wapinzani Bungeni. Lengo kuu lilikuwa ni kunyamazisha sauti za upinzani ndani ya Bunge kwa nguvu na maarifa yoyote yale. Hakukuwa na uchaguzi wowote huru au usio huru. Kulikuwa na uchafuzi na uteuzi.
Katika kufanikisha hilo lengo kuu, watu waliteswa;walijeruhiwa;waliminywa na hata wengine kuikimbia nchi. Wananchi walibanwa kwenye kona ya kuona CCM tu wakitamba kama dume la simba bila upinzani wowote. Safu kandamizi ilisukwa kuanzia NEC hadi chini kabisa vituoni. CCM tukashinda kwa kishindo kuliko cha nyundo na kushangilia huku wapinzani wetu wakilia. Mungu akatuona. Akaanza kutuadhibu.
Adhabu kutokana na machozi, jasho na damu ya watanzania uchaguzini. Adhabu kuhusu kuuharibu uchaguzi mkuu makusudi kwa kutimiza lengo la kuufuta upinzani nchini Tanzania. Adhabu ilipoanza, tukaanza kuweweseka. Kwanza, tukalazimisha uwepo upinzani Bungeni ule ule ambao tulitaka usiwepo. Tukalazimisha Wabunge 19 waitwe wa CHADEMA na wa ACT waingie Bungeni kwa mbwembwe.
Haikuishia hapo. Sasa Wabunge wetu wanaparurana kilaana wenyewe kwa wenyewe. Eti, wanawapambanisha na kuwatofautisha Mwendazake Magufuli na Rais Samia. Eti, Wabunge wanademka na kuchemka kumponda mmoja na kumpenda mwingine. Eti Wabunge wetu wa CCM wanaunda kambi kalikali kama mbilimbi. Wanaunda pande kama kande. Wabunge wetu wanaweweseka na kuhangaika kwa laana ya 2020.
Amini nawaambia, hakuna Mbunge wa sasa anayeufurahia ubunge wake. Wabunge wetu hawana amani kama zamani. Wanateswa na dhamira zao na majuto yamekuwa akilini mwao. Wabunge wetu wanatamani kusema Bunge livunjwe lakini hawawezi. Wanatamani tuanza upya kama Taifa kidemokrasia lakini hawathubutu. Wanaishia kupambana wenyewe kwa wenyewe. Karma is real!
Mama, waache Wabunge wademke hadi hamu yao iwatoke!
Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Masasi, Mtwara)