Ukweli mchungu! Waliommiminia risasi 38 na 16 zikatua mwilini mwake wanateseka kuliko yeye aliyemiminiwa hizo risasi!

Naunga mkono hoja, tena mpango wenyewe ni kama ule wa Masiya " ni kwa kupigwa kwake, sisi tuliponywa".
Thanks
Japo najua karma itawashughulikia watesi wake, swali linabaki, jee kwa kupigwa kwake sisi tutaponywa?.

Time Will Tell.
P.
We jamaa una akili sana, ulifaa uwe pale magogoni ukila bata.
 
Walitaka kumuua walifanya kitendo kibaya sana kiubinadamu.

Kusema wanateseka ni kujifariji tu kwa sababu kama kazi zao ni kuua kwa nini wateseke. Wao watakuwa wametimiza malengo ya kazi zao.

Ni sawa na kusema wanaotengeneza siraha wanateseka kwa sababu zinatumika kuua! Hiyo ni biashara yao halafu watasekaje!

Tuache kujifariji kwa hisia ambazo hazina mantiki.


Sent from my iPhone using JamiiForums
Malengo yao yalikuwa ni kuua, je walifanikiwa kumuua? Kama wangefanikiwa ingekuwa nafuu kwao kwa sababu wangepata guilty consciousness mara chache wasomapo habari zake. Lakini mtu bado yupo hai na anaonekana mara kwa mara kwenye media, ni mateso makubwa kwa waliofanya jaribio hata kama wawe na roho ya shetani kiasi gani. Haishangazi kuona watu fulani wanaweweseka na kuropoka mara kwa mara. Kilangila.
 
Naunga mkono hoja, tena mpango wenyewe ni kama ule wa Masiya " ni kwa kupigwa kwake, sisi tuliponywa".
Thanks
Japo najua karma itawashughulikia watesi wake, swali linabaki, jee kwa kupigwa kwake sisi tutaponywa?.

Time Will Tell.
P.
Amini nakwambia "SISI TUMEPONA". Jaribio lile lingefanikiwa wangenyamazishwa "uawa" wengine, lisingeishia kwa Lissu. Kushindikana kwake kuliwafanya wauaji watulie kujipanga upya. Wamwonavyo hai akiwatangaza kwenye media wanaishiwa nguvu kabisa. Ndiyo maana hata wanaojipendekeza kuwatetea, wanashindwa kujibu maswali ya msingi. Kilangila.
 
Mission imefeli wanatakiwa walambwe shaba

#bamia_ndefunene
Katika ulimwengu wa "conspiracy" usikute aliyeshika siraha, naye ameshauawa kitambo. Hii inazuia uwezekano wa aliyefanya jaribio kuanza kuweweseka anapomuona akiwa hai yule aliyetaka kumtoa roho. Guilty consciousness inaweza kusababisha muuaji na washirika wake wajulikane. Dawa yake huwa ni "elimination". Kilangila.
 
Kalamu1 kasema anakudharau...unajuaje hakujui wala hajakuona? Naona unazidi tu kuteseka, pole sana.
Atanijulia wapi na mimi ni nani? Wakati jina nalo tumia ni humu ni fake na hajui mimi niko wapi Australia Europe, Amerika au Afrika. Na Afrika nchi gani Tanzania, Malawi, Kenya au nchi nyingine na mji gani na genda gani na umri wangu?

Kwa maelezo hayo kama uliyaona mahesabu ya Statistics utaona kuwa probality ya yeye kunijua mimi is vanishingly small. Probality yake ni continents × countries × cities × streets of the World. The function curve of the probability graphically converge against zero line.
 
Nyie watanzania aidha nyie ni vichaa au ni wajinga wa kupindukia. JF Kennedy Rais wa Marekani alipigwa kisasi moja tu na ilimfunua fuvu lake na silaha za wakati ule. Nyinyi mnataka kuwamaanisha watanzania na ulimwengu kuwa Lissu kapigwa risasi 16 na silaha za kisasa za leo halafu mguu na mwili uokolewe? Hiyo Story nendeni mkamwambie Bibi yenu kijijini nafikiri ndiye atakaye waamini.





Zaidi ya hayo ni serikali gani na askari polisi gani ambao wanaweza kufanya tukio la kinjinga namna hiyo? Mnakubali kweli kilishwa matango poli na ujinga huo? Kama serika ya Magufuli ilitaka kumwua Lissu kweli ingefanyia hilo tukio Dodoma? Kwenye ulinzi mkali? Yaani kwote huko aliko zunguka washindwe wamsubiri kwenye Ngome? Aisee hiyo kali sana.

Kama kweli waliomtendea Lissu kitendo hicho cha kinyama ni serikali na Dodoma, basi imani yangu ya ulinzi na intelligent service ya serikali Ita kuwa ni ya kiovyo sana. Kitu ambacho siamini. Rais Magufuli anavyopenda watu sidhani kama anaweza toa amuri za kinjinga namna hiyo. Watu wa secrety Service hawawezi wakafanya mauaji ya kinjinga namna hiyo. Kuna njia nyingi za kumaliza mit lakini sio hivyo.

Watu wanao kubali uongo huo nadhani hata JKT hawajaenda na wala Kalashnikov hawaja ishika mikononi na hata kisasi hawaja wahi kuifyatua. Ni watu ambao wanalishwa kila kitu na kukubali. Hawana hata ule uwezo wa kujiuliza wenyewe kuwa kitu kama hicho inawezekana au la?

Tunaomba picha na clips za Lissu akiwa hospitalini Kenya tuone majeraha yake na hali ya mguu au mwili wake baada ya kumiminiwa risasi 16, maana tunaona picha za bandage tu. Kwanza maelezo ya dereva wake mwenyewe ni hovyo hata kudanganya kwenyewe hawezi. Akirudi katika kuhojiwa ataumbuka tu.

Nina uhakika serikali ya Tanzania imejipanha vizuri sana na ina ushahidi wa kutosha. Kinacho subiliwa ni huyo mwaini na msaliti wa nchi arudi. CHADEMA, Lissu na wote wanao usupport ujinga huo mtaumbuka kishenzi nyie!

Lissu hatafanyiwa kitu kibaya na serikali akirudi, hiyo nina uhakika, ila serikali na baadhi ya watanzania wako tayari kuwa-face CHADEMA na Lissu na uongo wao. Uongo wenu CHADEMA utawekwa wazi na wataalam na watu wenye uzoefu wa aina tofauti ya silaha. Watanzania tutafahamu ukweli wa mambo sio mda mrefu.

Risasi 16 kwenye mwili wa binadam alafu tuambiwe eti mguu wa kulia ndiyo uliojeruhiwa vibaya, wakati risasi inapita kwenye mwili wa binadamu kama vile kisu cha mkate kwenye siagi? Hiyo siamini.

Ni mategemeo yangu hizo bullet na makombora yake yako kwenye mikonao vyombo vya ulinzi na usalama na ni matarajio yangu makubwa kuwa majaribio mbali mbali ya hiyo silaha kwenye miili ya binadam yatakuwa yamesha patikana tayari kwa kutoa ufafanuzi juu ya Effekt ya silaha risasi hizo kwenye mwili hiyo.

Tutatafuta tu clips kwenye Youtube ya Effekt ya hiyo silaha kwenye misiki ya binadam na kudemonstrate kwa public kuonyesha uongo ulio tumika.

Lissu na CHADEMA Watanzania wanadai pics za majeraha ili tuzione!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa Lissu kuwa hai katika mazingira hayo uliyoyaeleza unapaswa kuanzia leo ujue kuwa Mungu yupo na uanze kuiamini story ya kwenye biblia kuwa Mungu alimuokoa Daniel kwenye shimo lililojaa Simba wenye njaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naam, walimmiminia risasi thelathini na nane (38) na kumi na sita (16) kati ya hizo zikatua mwilini mwake.

Naam, zilikuwa ni risasi za kumwangusha tembo na waliondoka hapo wakijua kazi waliyotumwa imemalizika.

Waliondoka hapo kwa haraka ya kufikisha habari njema hii kwa waliokuwa wakiwasubiri kwa hamu kubwa.

Walijua ujira na pongezi kubwa zilikuwa zikiwasubiri kwa kutekeleza kwa ufanisi mkubwa jukumu walilopewa.

Hapana shaka wakiwa njiani walijipongeza wakiwa na uhakika wa mapokezi makubwa yanayowasubiri.

Je kwa nini pamoja na yote hayo, waliomimina risasi wanaonekana kuteseka kuliko aliyemiminiwa risasi? Toa maoni...
Hasa mtu fake Paulo Makonda
 
Niliwahi soma pahala, kama si yeye mmoja wapo wa wavumbuzi wa siraha alitaabika sana alipokuwa anapata taarifa juu ya ufanisi wa siraha yake katika kuua watu. Kilangila.
Ndio mwenyewe Lt. Gen. Kalashnikov mwaka 2012 aliandikia barua kwa mkuu wa kanisa la orthodox akijutia silaha aliyogundua inavyomaliza uhai wa watu huko somalia na Afghanistan.

Japo mwanzo alikuwa anajitetea alitengeneza kwa ajili ya ulinzi sio kuuana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom