Ukweli mchungu! Waliommiminia risasi 38 na 16 zikatua mwilini mwake wanateseka kuliko yeye aliyemiminiwa hizo risasi!

Mag3

JF-Expert Member
May 31, 2008
11,684
2,000
Naam, walimmiminia risasi thelathini na nane (38) na kumi na sita (16) kati ya hizo zikatua mwilini mwake.

Naam, zilikuwa ni risasi za kumwangusha tembo na waliondoka hapo wakijua kazi waliyotumwa imemalizika.

Waliondoka hapo kwa haraka ya kufikisha habari njema hii kwa waliokuwa wakiwasubiri kwa hamu kubwa.

Walijua ujira na pongezi kubwa zilikuwa zikiwasubiri kwa kutekeleza kwa ufanisi mkubwa jukumu walilopewa.

Hapana shaka wakiwa njiani walijipongeza wakiwa na uhakika wa mapokezi makubwa yanayowasubiri.

Je kwa nini pamoja na yote hayo, waliomimina risasi wanaonekana kuteseka kuliko aliyemiminiwa risasi? Toa maoni...
 
HEKIMA KWANZA

JF-Expert Member
Mar 31, 2015
2,881

Uko sahihi na ndio sababu wanamtibu wao wenyewe.
 
msabillah

JF-Expert Member
Dec 5, 2011
3,813
2,000
Hajaandika neno "ugolo" mahali popote. Ameuliza hivi; Je kwa nini pamoja na yote hayo, waliomimina risasi wanaonekana kuteseka kuliko aliyemiminiwa risasi?
Nikweli wanateseka sana, kuanzia gharama za matibabu hadi kusafirisha kwenda kwa wazungu kuwaonyesha walichomfanya, dah inasikitisha sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
gemmanuel265

JF-Expert Member
Feb 16, 2016
8,500
2,000
Naam, walimmiminia risasi thelathini na nane (38) na kumi na sita (16) kati ya hizo zikatua mwilini mwake.
Naam, zilikuwa ni risasi za kumwangusha tembo na waliondoka hapo wakijua kazi waliyotumwa imemalizika.
Waliondoka hapo kwa haraka ya kufikisha habari njema hii kwa waliokuwa wakiwasubiri kwa hamu kubwa.
Walijua ujira na pongezi kubwa zilikuwa zikiwasubiri kwa kutekeleza kwa ufanisi mkubwa jukumu walilopewa.
Hapana shaka wakiwa njiani walijipongeza wakiwa na uhakika wa mapokezi makubwa yanayowasubiri.

Je kwa nini pamoja na yote hayo, waliomimina risasi wanaonekana kuteseka kuliko aliyemiminiwa risasi? Toa maoni...
Kumwaga damu ya mtu asiye na hatia siyo jambo rahisi ndio maana wanateseka mioyoni mwao huku waliyekuwa wamedhamiria kumuua akiwa na tabasamu muda wote

Sent using Jamii Forums mobile app
 
MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
12,693
2,000
Walitaka kumuua walifanya kitendo kibaya sana kiubinadamu.

Kusema wanateseka ni kujifariji tu kwa sababu kama kazi zao ni kuua kwa nini wateseke. Wao watakuwa wametimiza malengo ya kazi zao.

Ni sawa na kusema wanaotengeneza siraha wanateseka kwa sababu zinatumika kuua! Hiyo ni biashara yao halafu watasekaje!

Tuache kujifariji kwa hisia ambazo hazina mantiki.

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Mwifwa

JF-Expert Member
Apr 3, 2017
35,942
2,000
Ukiwa kwenye chumba cha mtihani ukafanya swali na ukawa na uhakika wa kulipata kwa aslimia zote.

Baada ya kutoka, ukasikia rafiki yako anasema jibu lilikuwa 4 na wala sio -4, lazima utaumia sana kwa kosa hilo dogo.
 
Counsellor Sima

JF-Expert Member
Jun 28, 2016
522
1,000
Who told u? Wapo kazin kama wewe ambavyo upo kazini......na ni kaisari....mnaamua kuandika mnavyoviamini....
 
carter

JF-Expert Member
Jan 23, 2009
3,210
2,000
Walitaka kumuua walifanya kitendo kibaya sana kiubinadamu.

Kusema wanateseka ni kujifariji tu kwa sababu kama kazi zao ni kuua kwa nini wateseke. Wao watakuwa wametimiza malengo ya kazi zao.

Ni sawa na kusema wanaotengeneza siraha wanateseka kwa sababu zinatumika kuua! Hiyo ni biashara yao halafu watasekaje!

Tuache kujifariji kwa hisia ambazo hazina mantiki.

Sent from my iPhone using JamiiForums
Ngoja nipitie bio ya Kalashnikov nijue aliteseka baada ya kuona kazi ya mikono yake inavyolaza watu chini? #AK-47#

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Maneno Meier

JF-Expert Member
May 12, 2013
1,967
2,000
Naam, walimmiminia risasi thelathini na nane (38) na kumi na sita (16) kati ya hizo zikatua mwilini mwake.
Naam, zilikuwa ni risasi za kumwangusha tembo na waliondoka hapo wakijua kazi waliyotumwa imemalizika.
Waliondoka hapo kwa haraka ya kufikisha habari njema hii kwa waliokuwa wakiwasubiri kwa hamu kubwa.
Walijua ujira na pongezi kubwa zilikuwa zikiwasubiri kwa kutekeleza kwa ufanisi mkubwa jukumu walilopewa.
Hapana shaka wakiwa njiani walijipongeza wakiwa na uhakika wa mapokezi makubwa yanayowasubiri.

Je kwa nini pamoja na yote hayo, waliomimina risasi wanaonekana kuteseka kuliko aliyemiminiwa risasi? Toa maoni...
Nyie watanzania aidha nyie ni vichaa au ni wajinga wa kupindukia. JF Kennedy Rais wa Marekani alipigwa kisasi moja tu na ilimfunua fuvu lake na silaha za wakati ule. Nyinyi mnataka kuwamaanisha watanzania na ulimwengu kuwa Lissu kapigwa risasi 16 na silaha za kisasa za leo halafu mguu na mwili uokolewe? Hiyo Story nendeni mkamwambie Bibi yenu kijijini nafikiri ndiye atakaye waamini.Zaidi ya hayo ni serikali gani na askari polisi gani ambao wanaweza kufanya tukio la kinjinga namna hiyo? Mnakubali kweli kilishwa matango poli na ujinga huo? Kama serika ya Magufuli ilitaka kumwua Lissu kweli ingefanyia hilo tukio Dodoma? Kwenye ulinzi mkali? Yaani kwote huko aliko zunguka washindwe wamsubiri kwenye Ngome? Aisee hiyo kali sana.

Kama kweli waliomtendea Lissu kitendo hicho cha kinyama ni serikali na Dodoma, basi imani yangu ya ulinzi na intelligent service ya serikali Ita kuwa ni ya kiovyo sana. Kitu ambacho siamini. Rais Magufuli anavyopenda watu sidhani kama anaweza toa amuri za kinjinga namna hiyo. Watu wa secrety Service hawawezi wakafanya mauaji ya kinjinga namna hiyo. Kuna njia nyingi za kumaliza mit lakini sio hivyo.

Watu wanao kubali uongo huo nadhani hata JKT hawajaenda na wala Kalashnikov hawaja ishika mikononi na hata kisasi hawaja wahi kuifyatua. Ni watu ambao wanalishwa kila kitu na kukubali. Hawana hata ule uwezo wa kujiuliza wenyewe kuwa kitu kama hicho inawezekana au la?

Tunaomba picha na clips za Lissu akiwa hospitalini Kenya tuone majeraha yake na hali ya mguu au mwili wake baada ya kumiminiwa risasi 16, maana tunaona picha za bandage tu. Kwanza maelezo ya dereva wake mwenyewe ni hovyo hata kudanganya kwenyewe hawezi. Akirudi katika kuhojiwa ataumbuka tu.

Nina uhakika serikali ya Tanzania imejipanha vizuri sana na ina ushahidi wa kutosha. Kinacho subiliwa ni huyo mwaini na msaliti wa nchi arudi. CHADEMA, Lissu na wote wanao usupport ujinga huo mtaumbuka kishenzi nyie!

Lissu hatafanyiwa kitu kibaya na serikali akirudi, hiyo nina uhakika, ila serikali na baadhi ya watanzania wako tayari kuwa-face CHADEMA na Lissu na uongo wao. Uongo wenu CHADEMA utawekwa wazi na wataalam na watu wenye uzoefu wa aina tofauti ya silaha. Watanzania tutafahamu ukweli wa mambo sio mda mrefu.

Risasi 16 kwenye mwili wa binadam alafu tuambiwe eti mguu wa kulia ndiyo uliojeruhiwa vibaya, wakati risasi inapita kwenye mwili wa binadamu kama vile kisu cha mkate kwenye siagi? Hiyo siamini.

Ni mategemeo yangu hizo bullet na makombora yake yako kwenye mikonao vyombo vya ulinzi na usalama na ni matarajio yangu makubwa kuwa majaribio mbali mbali ya hiyo silaha kwenye miili ya binadam yatakuwa yamesha patikana tayari kwa kutoa ufafanuzi juu ya Effekt ya silaha risasi hizo kwenye mwili hiyo.

Tutatafuta tu clips kwenye Youtube ya Effekt ya hiyo silaha kwenye misiki ya binadam na kudemonstrate kwa public kuonyesha uongo ulio tumika.

Lissu na CHADEMA Watanzania wanadai pics za majeraha ili tuzione!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mag3

JF-Expert Member
May 31, 2008
11,684
2,000
Nyie watanzania aidha nyie ni vichaa au ni wajinga wa kupindukia. JF Kennedy Rais wa Marekani alipigwa kisasi moja tu na ilimfunua fuvu lake na silaha za wakati ule. Nyinyi mnataka kuwamaanisha watanzania na ulimwengu kuwa Lissu kapigwa risasi 16 na silaha za kisasa za leo halafu mguu na mwili uokolewe? Hiyo Story nendeni mkamwambie Bibi yenu kijijini nafikiri ndiye atakaye waamini.
Tuliza presha, hata waliomimina risasi nao wamepigwa butwaa kama wewe...mateso hutesa. Wapo ambao toka tarehe 7/10/2017 wameshindwa hata kulitamka jina la aliyemiminiwa risasi.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom