Mkaruka
JF-Expert Member
- Feb 5, 2013
- 19,629
- 34,172
Habarini wanaJF.
Kwanza nikiri kuwa hili suala la viongozi wa dini Tanzania limekuwa likinisumbua sana lakini leo imenibidi niliseme na sehemu kuu ya kusemea ni hapa JF
Viongozi wa dini Tanzania wamekuwa ndio vinara wa KUKOSOA,KULALAMIKA n kulialia Kuwa serikali haileti maendeleo.Ni kweli hata mimi ninakubaliana nao kuhusu hili ya kuwa Raslimali tulizonazo(isipokuwa raslimali watu) tulipaswa kuwa mbali zaidi.Lakini hawa viongozi wa dini ndio wanaoongoza kuturudisha nyuma.Nitaeleza.............
Chanzo kikuu cha mapato ya serikali yoyote ile duniani ni KODI,Hakuna nchi ambayo raia wake hawalipi KODI na KODI siyo suala ambalo ni "Optional" kwamba unaweza kufanya amma usifanye.NI LAZIMA KILA RAIA ALIPE KODI.
Taasisi za dini Tanzania zimekuwa zikipokea MISAMAHA MIKUBWA YA KODI(Jambo ambalo si sahihi kwa mujibu wa imani).Nitatoa takwimu kidogo
3.Tusiwe kwazo la namna yo yote katika jambo lo lote, ili utumishi wetu usilaumiwe; bali katika kila neno tujipatie sifa njema, kama watumishi wa Mungu; ..... (2 KOR. 6:3, 4 SUV).
Naamini hata taasisi nyigine za dini zinaliona hili kuwa ni KOSA kubwa ila bahati hakuna wa kulizungumzia.
Kwa MUKTADHA huu Je, ni sahihi kwa taasisi za DINI KUDAI Maendeleo wakati hawalipi KODI?
Je,SUALA hili ni sawa KIIMANI??
Cc Mzee Mwanakijiji

Ukiangalia takwimu hapo juu utaona gharama kubwa sana.Mimi ni mkristo nitatoa mfano ikiwa TAASISI ZA KIKIRISTO Kupokea MISAMAHA ya KODI ni HALALI.Yesu Kristo mwenyewe alilipa KODI kwa utawala wa enzi zake na hakuna sehemu yoyote katika biblia Yesu amashauri wakristo wasilipe KODI.Mifano ya maandiko...1. BAKWATA na Taasisi zake (Shule, Vyuo, Hospitali, misikiti etc)
-magari 82 ya aina tofauti yenye thamani ya Bil 6.8 (Kodi iliyosamehewa Bil 1.9),
2. Kanisa Katoliki na Taasisi zake (vyuo, shule, hospitali, parokia etc) - Magari 691 yenye thamani ya Bil 59.5 (Kodi iliyosamehewa Bil 19.3),
3. CCT na Taasisi zake (vyuo, shule, hospitali, makanisa etc), magari 527 yenye thamani ya Bil.42.9 (kodi iliyosamehewa Bil.13.8),
4. Makanisa ya Pentecoste na Taasisi zake (vyuo, shule, hospitali, makanisa etc) - magari 2,719 ya aina mbalimbali yenye thamani ya Bil 186.1 (kodi iliyosamehewa Bil 57.4),
5. Taasisi nyingine za dini (Hindu, Budha etc) magari 203 ya aina mbalimbali yenye thamani ya Bil 36.4 (kodi iliyosamehewa Bil 9.01).
JUMLA ya Magari yaliyoingizwa nchini kwa mwavuli wa Taasisi za dini tangu Mwaka 2006 (Magari 4,222).
JUMLA ya Kodi iliyosamehewa BIL 102.41
]
2.Hata walipofika Kapernaumu, wale watozao nusu-shekeli walimwendea Petro, wakasema, Je! Mwalimu wenu hatoi nusu-shekeli? Akasema, Hutoa. Naye alipoingia nyumbani, Yesu alitangulia kumwuliza, akisema, Waonaje, Simoni? Wafalme wa dunia hutwaa kodi ama ushuru kwa watu gani? Kwa wana wao au kwa wageni? Naye aliposema, Kwa wageni, Yesu alimwambia, Basi, kama ni hivyo, wana ni mahuru. Lakini tusije tukawakwaza, enenda baharini ukatupe ndoana, ukatwae samaki yule azukaye kwanza; na ukifumbua mdomo wake utaona shekeli; ichukue hiyo ukawape kwa ajili yangu na kwa ajili yako. (MT. 17:24-27 SUV).1.
" Mpeni Kaisari yaliyo yake Kaisari , na Mungu yaliyo ya Mungu ." (Mathayo 22:21 )