Ukweli mchungu utabiri wa BIBLIA kuhusu nyakati za mwisho wa dunia unazidi kutimia..

Nystatin

JF-Expert Member
Oct 31, 2020
2,402
2,000
Njaa kali na upungufu wa chakula-math 24:7


Vita kwa kadri kubwa
ufunuo 6:4

upendo wa watu wengi kumwelekea mungu ungepoa
math 24:12

Unafiki wa kidini utakua waziwazi
2 Timotheo 3:5

Tauni-magonjwa yanayoenea sana
luka 21:11

Matetemeko
Luka 21:11

Kuvunjika kwa familia-watu watakua hawana upendo wa asili tena...watoto hawata waheshimu wazazi na usaliti utaongezeka
2 timotheo 3:5
 

Mathanzua

JF-Expert Member
Jan 4, 2017
10,585
2,000
Njaa kali na upungufu wa chakula-math 24:7


Vita kwa kadri kubwa
ufunuo 6:4

upendo wa watu wengi kumwelekea mungu ungepoa
math 24:12

Unafiki wa kidini utakua waziwazi
2 Timotheo 3:5

Tauni-magonjwa yanayoenea sana
luka 21:11

Matetemeko
Luka 21:11

Kuvunjika kwa familia-watu watakua hawana upendo wa asili tena...watoto hawata waheshimu wazazi na usaliti utaongezeka
2 timotheo 3:5
Na mengi mengineyo.Ila agents wa Lucifer a.k.a Shetani watakuja kukupinga.
 

avogadro

JF-Expert Member
Apr 30, 2013
4,838
2,000
Tatizo la vijana mliozaliwa juzi mnasema njaa imeongezeka ?

1. Wewe tulishapita kipindi cha kugaiwa kibaba cha unga wa njano wa yanga unasema nini?

2. Tulishakunjwa na kushindia uji wa chunvi, malimao na ubuyu wewe unasema nini? umewahi kula ugali uliochanganywa na chunvi usio na mboga wewe?

3. Uliwahi kunanua vitu duka lakijiji kwa foleni na majina na kama ni robo kilo huruhusiwi kununua zaidi hadi umtafute mnyonge zaidi yako achukue posheni yake akuuzie? wewe acha kabisa wewe kijana uliyesoma medium tuliiiya kabisa
 

Ushindi victory

JF-Expert Member
Dec 11, 2018
767
1,000
icho kitabu mnachokitumia kutabir kitawapeleka chakaa, yaan chakaa vibaya sana

kwann chaka? kwasababu kuna mambo ya muhimu humo yaliongelewa kuhusu matukio yanayotokea leo hii, lkn ktk biblia za kisasa zote huwez kupata haya maandiko tena, sabbu kuna wajanja tyr walishayaondoa hayo maandiko kwa faida zao wenyewe ili watu wabaki vipofu na wasjue jinsi gani watayaepuka yale majanga yatakayoikumba dunia.

wengi walkuwa wanaongelea hata mambo ya covid19 kuwa ni chapa ya666, wengine wapo mpka leo hii wanasema kuwa haya majanga na magonjwa ni Mungu analeta ili kuadhibu wanadamu sabbu ya dhambi, huu ni uongo mkubwa unaopotosha watu.

Matatizo yoote dunian msababishaji ni mwanadamu, hayo magonjwa, vita, njaa, mafuriko, matetemeko na vimbunga mwanadamu ndye msababishaji, kwann nasema hiv, sabbu kuna wahuni wanao control hali za hewa/mazingira jinsi wapendavyo, kupitia technolojia zao.

pia magonjwa yote, kama ukimwi, malaria, covid, kansa na mengineyo msababshaji ni mwanadamu, na hawa ni baazi ya washenz kutoka ktk makundi ya watu wachache wenye mipango ovu duniani.

hiyo biblia&quran mnayotumia kuswal&kusal zilishachezewa sana na mikono ya wajanja wachache kwa kuondoa vifungu vinavyofichua uovu wa dunia na wakaviedit kwa kuweka uongo uongo ambao haujawai na hautowai kuwepo.

nawashangaa sana hata ninyi mnaomsubil huyo yesu wenu feki kuwa ataurud hapo israel feki, na ninyi mnaomsubil masihi dajal mwenye jicho moja, nasemaje mtakesha kusubil hizo tabil zenu za uongo na hazitatokea ng'oo sabab zilibuniwa ili kuwahadaa,

naweza kukuonesha tabil za kwel ambazo zilitokea na znatokea na zitazid kutokea ambazo ndzo zilitakiwa kuwepo ktk vtabu vyenu vya dini.

Dini zote pamoja na imani zote mnazokalilishana ni Uongo by100% ukwel mchungu..
FB_IMG_16376797644151192.jpg
 

Kuchwizzy

JF-Expert Member
Oct 1, 2019
830
1,000
Hayo mambo yote yaliyotajwa kwenye huo unaoita utabiri
yalikuwepo hata kabla ya huo utabiri haujaandikwa

Vita vilikuwepo tangu binadamu amepata ustaarabu

Njaa ilikuwepo tangu binadamu wanaishi kwenye mapango

Magonjwa yalikuwepo kabla ya huo utabiri

Kinyume chake, tunaishi katika kipindi ambacho vita, njaa na magonjwa vimepungua kuliko kipindi chochote kile katika historia

Thanks to Science and Technology
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom