Ukweli mchungu!! Usalama wa Taifa wanaamini Rais huchaguliwa na kamati ya CCM na si wananchi

Kimsingi hata wagombea wa vyama vyengine wanapaswa kupewa ulinzi... Marekani Trump alianza kupewa ulinzi kutoka Secret service tangu alipochaguliwa na chama chake kuwa mgombea

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Braza weka kumbukumbu sahihi, unadhani wale waliokuwa wanamlinda lowasa wakati wa kampeni wanatoka chadema? Kama huna uelewa ni bora ukae kimya, kamuilize lowasa kuwa amebadirishiwa waliokuwa wanamlinda? Nadhan waliangalia ulazima wa wagombea wale kulindwa kulingana na ushawishi wao na uwezekano wa kufanyiwa hujuma. Maana tayar waliingia kwenye kundi la watu mashuhuri (VIP) ambao vyombo vya ulinzi vilipaswa viwalinde kwa nguvu zote. Sometimes nafikiri tusiwe mashabiki tuulozane wenyeewe kwanza maana hata ukisoma kwenye vitabu vya kiusalama hata mitandaoni vitakuonyesha ni watu wa aina gani wanastahili kulindwa. Hata MO na Bakhresa wakikubali kulindwa watalindwa kwa nafasi zao katika jamii na uchumi wa nchi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Lowassa analindwa mpaka kesho na walinzi toka usalama kutokana na washifa wake aliyowahi kuushika kama waziri mkuu. usalama hawajawahi kufanya hivyo kwa wagombea wengine. na ndio utaratibu wetu hivyo siwadai wafanye hivyo. au nionyeshe mlinzi wa dovutwa au wa Hashimu Rungwe aliyetoka jikoni.

tukubali tuu vyombo vya usalama havina ushirikiano na vyama vya upinzani mengine porojo
 
Wale wapenda mabadiliko ya kweli tunapaswa kubadili mbinu za kupata yale mabadiliko tunayoyataka.

Tukiongelea uchaguzi wa kila baada ya miaka mitano kama ni ucahguzi wa wananchi tunajidanganya na tunawadanya wananchi ambao hawana uelewa mpana wa maswala ya nchi yetu.

Taasisi nyeti ya usalama wa taifa haimini katika mfumo wa vyama vingi wala katika mfumo wa kuchaguana katika sanduku la kura. Hivyo basi huu utaratibu wa kupiga kura ni kuhalalisha tuu kile walichokiamua wao huko vyumbani.

Nitatolea mfano kwa uchaguzi uliopita uliomuweka madarakani mheshimiwa magufuli. Taasisi nyeti ya usalama wa taifa ilianza kumlinda tangu pale alipochaguliwa na kikao cha ccm pale dodoma. Na bila aibu wala wasi wasi mlinzi wake waliomuweka tangu anachaguliwa magufuli dodoma ndio mlinzi wake mpaka leo hii. Wewe unaona mimi naona na wao wanaona na hakuna cha kuwafanya.

Kama wao wanaopaswa kusimamia haki wanamtambua mtu kuwa rais pale tuu anapochaguliwa na kamati za ccm wewe ni nani hata uje upindue maamuzi yao katika sanduku la kura??

Nasema hivi huku kufanya uchaguzi ni kupoteza muda na mali za nchi kwa mfumo tulionao.

Tupiganie kubadili mfumo wetu ndipo tuingie kwenye kushindana. Huwezi kushindana na watu unaotegemea wasimamie ushindani.

Huyu hapa chini mlinzi wa rais toka kwenye kampeni na kwa wakati ule alijifanya greengurd toka ccm na sasa ni mlinzi wa rais toka usalama wa nchi .

Tutafika tuu hata kama kwa shida ila tubadili mbinu za kushindana na hawa watu
proove
 
T

Tanzania haikuridhia wala kuwa tayari kukaribisha mfumo wa vyama vingi tangu mwanzo.

Lakini ilibidi kukubaliana na hali ya hewa ya hewa tu. Na ndio maana hawakubadilisha katiba bali kufanya marekebisho ya Katiba ya 1977 kisha kwa kutumia Taasisi kama TISS, Bunge, Polisi, NEC nk kuhodhi na kuthibiti mfumo huo wa kinafiki. Tubadili mfumo, madaraka yarudi kwa wananchi.
 
kwani hii ni siri?? au nimewatukana?? au huyu mlinzi nimemsingizia?? usalama hawako hivyo mnavyotaka tuamin wao ni makatili. yaan et ukiwazungumzia tuu wewe kwisha habari yako no. mm nitasema pale naona inafaa kusema kwa lugha sahihi isio na matusi. sasa kama wao ukweli ni maudhi kwao hadi kuua mtu hakuna shida waje tuu kufa ni kwa kila mtu
Umemjibu vzr. Anataka kutuaminisha kwamba kitengo ni kikundi cha wauaji, jambo ambalo siyo sahihi sana.
 
Hata wao wanabahatisha tu,Kama kunakipindi watanzania tumeishi maisha ya mateso hofu na unyonge basi ni hii miaka sita iliyopita,kama kweli wao wanaona tusioyaona sisi basi safari hii hawakuona.
Hakuna usalama ambae Hana ndugu wafanyakazi,wafanyabiashara,wakulima,wanavyuo.
Kama yeye usalama analipwa vizuri basi mmoja wa ndugu zake hao amepitia machungu.
Kwa hiyo hawa wapendwa wetu TISS Ni wabinafsi na hawana uchungu na Watanzania wenzao.
Kwanini wasitumie uwezo wao wakabadili mfumo huo wa kishetani wa kumpata Raisi kutoka CCM tu? Na kuwaacha wananchi wakipoteza muda fedha na maisha kushiriki uchaguzi ambao hautoi mtu aliechaguliwa na wengi?
Mungu anawaona.
Mungu anawaona.
Mungu anawaona.
 
mkuu haya mambo yapo hata marekani, wazee wa kazi wakishaamua yupi ndiyo anafaa, hakuna namna, democracy is an imagination of beholders,

Huwezi kuachia nchi itawaliwe na yeyote anayejisikia, lazima achujwe na athibitishwe hasa kulingana na mwelekeo wa chama kwa uzito wake na ushawishi.

Unaposikia fulani kakatwa ndiyo mipango yenyewe, raia wengi hughubikwa na ushabiki kiasi kwamba wakiachwa waamue peke yao, athari nyingi zitatokea, Usalama wanawajua wagombea vizuri kuliko tunavyowajua sisi raia watiifu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Nakupinga kwa nguvu Sana afande wangu,najua utachukia kwa sababu nyinyi huwa hampendi kukosolewa.
Umedanganya mchana kweupe.
Vyombo vya usalama vya USA Vinautaratibu mzuri kabisa.
Vyombo vya Marekani huwa wanashauri vyama vyote bila upendeleo na Kisha Kama wanaona mgombea wa chama Fulani hafai wanawaambia mapema kabisa na chama kinamuondoa.
Wagombe wa vyama vyote wakikubaliwa na majasusi ndipo wanaletwa kwenye uchaguzi mkuu huru kabisa.
Sasa huku kwetu Ni kinyume kabisa,Ni full uonevu na kuvidukua vyama vya upinzani na kuinufaisha CCM.
We we na uafande wako hujashituka,ukija kushituka utajuta kuwa kumbe ile CCm halisi kama chama Cha Nyerere ilishagajiondokea hawa wa Sasa hivi Ni genge tu Kama Mafia.Na nyie mnawalinda bila kujua,mnaumiza watanzania wenzenu kwa ajili ya genge tu linatawala nchi kwa Jina la CCM.
Utakuja kuyakumbuka haya maneno yangu wakati huo machozi ya uchungu yakikutoka.
Wewe unaamini kweli kabisa uchaguzi huu ukiopita wapinzani wamekosa hata jimbo moja kweli?
Mungu hadhihakiwi bwana nadhani uneona majibu yake,na bado.
Mchungaji keshapigwa kondoo watatawanyika.
Huu Ni mwanzo
Kama hatutaki vyama vingi TISS shaurini muufute turudi single party system.
Kwani tunamwogopa Nani bana,kwa Nini kupoteza rasilimali na fedha?
 
Usalama wa Taifa ndiyo wadhibiti wa siasa na uchumi wa taifa letu, wanaona mbali kuliko ushabiki wetu wa kisiasa, walifanya kazi yao kikamilifu!

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwamba viongozi wooote wenye akili wanapatikana CCM,kwamba wataalam mahili wa uchumi wanapatikana CCM.
Lol!
Haya mawazo ya kijima kabisa haya.
Haya mawazo ndio waliyokuwa nayo wakoloni na makaburu kuwa mtu mweusi Hana akili hawezi kufanya lolote,hawezi kuongoza,hawezi kuwa dokta,hawezi kuendesha ndege.
Ksumba hii akawa nayo kiongozi mmoja mwafrika wa Kenya kwamba hakuna. Mwafrika awezae kuendesha ndege,siku aliposhuka kwenye ndege akaambiwa alipanda ndege iliuoendeshwa na mwafrika mwenzie hakuamini Hadi alivyoenda kumuona.
Upande wa upinzani Kuna watu mahili kabisa wanaoweza kuja na mawazo mbadala na wakaipeleka nchi mbali kabisa.by the way watanzania Ni wale wale tofauti nivyama tu.
Wamesoma shule za hapahapa pamoja,wamekwenda JK pamoja,wametoka vijijini kumoja,Sasa sijui labda wenzetu CCM wana miji yao na mambo yao .
 
Tanzania inasikitisha Sana ..ndio maana mimi sijawahi hata kushiriki upigaji wa kura ..kwa sababu akili yangu ilisha yanusa hayo mapema

Hii nchi bila ya mabeberu kutia fitina zao na kuitoa ccm madarakani " tujiandae kuendelea kuupokea unyang'anyi huu wa democracy milele

Sent using Jamii Forums mobile app
Aisee Hearly unakosea Sana kutokupiga kura.
Mimi najua kabisabkua huwa yanaiba ila malengo yangu Ni:-
Kuhakikisha kwamba nimeyakataa,kwa macho ya duniani huwezi ona Ila kwa Mungu tayari imeandikwa kuwa nimeyakataa,yaani sikuyachagua maCCM.
Lengo langu Ni yakiiba kura yangu yapate dhambi na laana.sasa kadri yakiiba kura nyingi ndio dhambi na laana zinakua nyingi hivyo Mungu huingilia kati na kushusha fimbo yake.Nadhani uneona safari hii Mungu kafanya yake.

Laana Ni mbaya Sana ndugu yangu,kilio Cha wengi Ni sauti ya Mungu.
Laana inaharibu Kila jema utakalolifanya ndio maana mtaani utasikia da jamaa Ana laana ya wazazi wake Kila afanyalo halifanikiwi.
Laana inadumu vizazi Saba.
Sasa hivi walioiba uchaguzi wamelaaniwa wao na watoto wao vizazi Saba.
Kuna mtu sijui Kama mtoto wake atakuja pata nafasi ya juu ya uongozi wa nchi hii siku za hivi karibuni,sababu ya laana ya kuiba uchaguzi.
Kuiba uchaguzi hata Mungu hukasirika kwa sababu unapoiba unakua umekataa maoni ya wengi Mungu lazima akushukie tu hata ulindwe na Ma spesho fosi wabobevu namna gani,magari yenye vifaa vya aliens Mungu atakuondoa tu.
Hai Ma spesho fosi walikua wanakesha bure tu.

Kwa hiyo wewe nenda kapige kura ili kuyalazimisha yatende zambi halafu yaendelee kuteseka.Dhambi inatesa bana hasa ya dhulumati.

Lengo jingine yajijue yasivyopendwa.
 
Wale wapenda mabadiliko ya kweli tunapaswa kubadili mbinu za kupata yale mabadiliko tunayoyataka.

Tukiongelea uchaguzi wa kila baada ya miaka mitano kama ni ucahguzi wa wananchi tunajidanganya na tunawadanya wananchi ambao hawana uelewa mpana wa maswala ya nchi yetu.

Taasisi nyeti ya usalama wa taifa haimini katika mfumo wa vyama vingi wala katika mfumo wa kuchaguana katika sanduku la kura. Hivyo basi huu utaratibu wa kupiga kura ni kuhalalisha tuu kile walichokiamua wao huko vyumbani.

Nitatolea mfano kwa uchaguzi uliopita uliomuweka madarakani mheshimiwa magufuli. Taasisi nyeti ya usalama wa taifa ilianza kumlinda tangu pale alipochaguliwa na kikao cha ccm pale dodoma. Na bila aibu wala wasi wasi mlinzi wake waliomuweka tangu anachaguliwa magufuli dodoma ndio mlinzi wake mpaka leo hii. Wewe unaona mimi naona na wao wanaona na hakuna cha kuwafanya.

Kama wao wanaopaswa kusimamia haki wanamtambua mtu kuwa rais pale tuu anapochaguliwa na kamati za ccm wewe ni nani hata uje upindue maamuzi yao katika sanduku la kura??

Nasema hivi huku kufanya uchaguzi ni kupoteza muda na mali za nchi kwa mfumo tulionao.

Tupiganie kubadili mfumo wetu ndipo tuingie kwenye kushindana. Huwezi kushindana na watu unaotegemea wasimamie ushindani.

Huyu hapa chini mlinzi wa rais toka kwenye kampeni na kwa wakati ule alijifanya greengurd toka ccm na sasa ni mlinzi wa rais toka usalama wa nchi .

Tutafika tuu hata kama kwa shida ila tubadili mbinu za kushindana na hawa watu
Umenikumbusha wale waliokuwa na mabegi yaliyo jaa,duu ulikuwa siyo uchaguzi Bali uchafuzi
 
Back
Top Bottom