UKWELI MCHUNGU: Tanzania tupo nyuma ya Kenya kimaendeleo

Boss Man

JF-Expert Member
Feb 10, 2022
458
991
Wajuzi wa mambo naomba nielewesheni jambo, ni kwanini sisi tuko nyuma ya Kenya katika mambo ambayo yakufanywa na mtu Binafsi na si serikali.

Mambo ya flyover, mabarabara na Hospitals nk hayo ni mambo ya Serikali so tusiongelee huko, ila nitazungumzia mambo Binafsi ambayo mm na wewe tunaweza kuyafanya.

Tuanzie kwenye Magari, Kenya wenzetu hasa Nairobi wanamchanganyiko wa magari brands tofauti tofauti, kuanzia Benz, Mazda, Mitsubishi, Honda, Subaru. kama hizi Mercedes Benz ambazo wabongo tunaziogopa kule ndio kama IST Sasa Kila Kona zimezagaa.

Na hata kwa hizi Toyota wao machaguo yao ni tofauti na sisi au sijui niseme wao wapo mbele ya muda au ni sisi ndio tupo nyuma ya muda, hizi Toyota IST ambazo huku ndio zinatamba wao walizitumia miaka mitano nyuma, huwezi kukuta IST namba D Kenya, Barabarani zipo chache sana ambazo ni namba B.

(Kwa wale wasiofahamu)....namba plate za Kenya na zetu Tz zinautofauti kidogo japokuwa wote tupo namba D lakini D yetu ipo mwishoni wao ndio kumekucha, mara ya mwisho nipo kule mwezi may namba yao ya mwisho ilikuwa inasoma KDH nadhani Sasa hivi watakuwa kwenye KDJ (not sure) sisi tupo DZQ.

Ukiachana na magari kitu kingine ambacho sio lazima serikali itufanyie au ituambie, ni kwann Bongo hakuna Supermarkets za kutosha? Watu watasema Wabongo hawana utamaduni wa kufanya manunuzi Supermarket lakini pengine ni labda tu hazipo za kutosha, Wenzetu Kenya Supermarkets hadi uswahilini, yaani Uswazi haswa zaidi ya Tandale lakini utakuta Supermarket, lakini Bongo Sasa Supermarket utazikuta town tu na ushuani tena hata Ushuani kwenyewe ni Mini supermarket.

Hata makazi ya kuishi wenzetu wao kuishi kwenye Apartments ni japo la kawaida lakini huku kwetu wanaoishi kwenye Apartments ni Wahindi hapo Kariakoo na Upanga, wabongo ni wakuhesabu.

Hivi ni kwanini tupo nyuma hivyo ndugu zangu, Yani tupo nyuma kweli kweli sababu hayo ni machache tu na siwezi kuongelea mambo yote hapa Uzi hautaisha.

Picsart_22-07-01_13-43-02-358.jpg
 
Ngoja nisemee hilo hi supermarket na min-supermarket. Kwa bongo wafanya biashara wengi wanoendesha hizo shughuri wana ulimbukeni wa kutafta faida kubwa kiasi kwamba had watu wenye hali ya uchumi wa kawaida wanaogopa kufanya manunuzi kwenye min/supermarket zao.

Mfano ulio hai ukiwa kanda ya ziwa ukaingia kununua bidhaa supermarket au mini-supermarket utakuta bei za bidhaa ni ×1.5-2 ya bei halisi mfano kahawa ya 4500-5000 utauziwa 8000-10000 had hapo unakuwa umeisha mjengea mteja mtazamo wa supermarket ni kwaajiri ya matajiri tu.

Nilipoona kuna nafuu ni ukienda kanda ya kasikazini mfano moshi utakuta (mini)supermarket ndio sehemu yenye bei ndogo zaid za bidhaa kulinganisha na madukani kias kias kwamba ata sisi wa uchumi wa chini na kati kataweza mudu.
 
Mfano ulio hai ukiwa kanda ya ziwa ukaingia kununua bidhaa supermarket au mini-supermarket utakuta bei za bidhaa ni ×1.5-2 ya bei halisi mfano kahawa ya 4500-5000 utauziwa 8000-10000 had hapo unakuwa umeisha mjengea mteja mtazamo wa supermarket ni kwaajiri ya matajiri tu. Nilipoona kuna nafuu ni ukienda kanda ya kasikazini mfano moshi utakuta (mini)supermarket ndio sehemu yenye bei ndogo zaid za bidhaa kulinganisha na madukani kias kias kwamba ata sisi wa uchumi wa chini na kati kataweza mudu.
Kweli Mzee, na hapo ulipoongelea Kanda ya Kaskazini ni kama Kenya tu, Kenya bidhaa zinazopatikana Supermarket ni bei rahisi kuliko Dukani au baadhi ya bidhaa utakuta bei zinafanana
 
Ngoja nisemee hilo hi supermarket na min-supermarket.

Kwa bongo wafanya biashara wengi wanoendesha hizo shughuri wana ulimbukeni wa kutafta faida kubwa kiasi kwamba had watu wenye hali ya uchumi wa kawaida wanaogopa kufanya manunuzi kwenye min/supermarket zao.

Mfano ulio hai ukiwa kanda ya ziwa ukaingia kununua bidhaa supermarket au mini-supermarket utakuta bei za bidhaa ni ×1.5-2 ya bei halisi mfano kahawa ya 4500-5000 utauziwa 8000-10000 had hapo unakuwa umeisha mjengea mteja mtazamo wa supermarket ni kwaajiri ya matajiri tu.

Nilipoona kuna nafuu ni ukienda kanda ya kasikazini mfano moshi utakuta (mini)supermarket ndio sehemu yenye bei ndogo zaid za bidhaa kulinganisha na madukani kias kias kwamba ata sisi wa uchumi wa chini na kati kataweza mudu.
Mfano kama Mimi ilikuwa nikitaka mkate basi lazima niufate Supermarket coz ni bei poa na wanakuwa na Ofa. Hasa mikate yenye brand ya supermarket kama Naivas au Quick mart na hizo ndizo Supermarkets zenye majina na wateja wengi na kila sehemu zinapatikana
 
wamiliki wa supermarket wa kibongo wengi hawana marketing strategies za kuattract walio wengi
 
Supermarkets na malls si vitu kizuri. Haya magenge na maduka ya mangi ni vitu muhimu sana kwa uchumi wa mtaa na mtu mmojammoja.

Kwenye maendeleo kuna kitu kinaitwa Gini coefficient. Ni tofauti ya walionacho na wasionacho. Kenya ni kubwa ndiyo maana unaona wengine wakifanya ufahari na ishu zingine. Tz tumegawana umaskini kwa usawa kwa kiasi fulani. Lakini pia usisahau kuwa Nairobi ni hub ya kimataifa.
 
Ngoja kwanza!!! Kabla hatujaenda kwenye hoja zako zingine...umesema Kenya ni kubwa?
 
Tafsiri ya mleta mada kuhusu maendeleo ya mtu binafsi haiko sahihi. Ni tafsiri ya kishamba sana. Maisha ya mtu binafsi kimaendeleo yatapimwa kwa uwezo wake wa kupata kipato cha kila siku, Chakula, Mavazi na Makazi.

Kuweka kumbukumbu sahihi, mleta mada unapaswa kufahamu haya kuhusu Kenya au Nairobi.

1. Nairobi sio kipimo cha maendeleo ya wakenya. Zaidi ya 80% ya wakenya hawaishi Nairobi. Na maisha ya Nairobi hayawakilishi maisha halisi ya wakenya.

2. Nairobi ni eneo lenye watu wa maisha mchanganyiko. Watu wenye maisha ya juu (Daraja la juu, hao wenye kumiliki magari ya kisasa nk) kwa Nairobi hawazidi 10%.

3. Nairobi kuna maeneo makubwa yenye maisha duni kupindukia. Mfano halisi ni eneo la Kibera, ambapo wakazi wake wengi hata vyoo vya uhakika hawana.
 
Sawa hata sisi tuna eneo kubwa lenye maisha duni, lakini tukisema tupambanishe hiyo miji miwili mikubwa Dar na Nai Bado sisi tutakuwa nyuma tu
 
Ist bongo zinatumika toka 2015,na brand zote ulizotaja Kenya bongo zipo. Mara ya mwisho nimefuatilia takwimu za magari ya kifahari afrika mashariki, Tanzania ilikua inaongoza
Ivi umekaa Nairobi au unajibu kwa kufuatisha hizo takwimu?...halafu sijasema hizo brand bongo hakuna, ila kwa experience yangu ya miji yote miwili Nairobi imechanganya brands zote kwa wingi kuliko Dar, Yani Dar mfano Benz zipo lakini ni za kuhesabu na kwa hadhi la hili jiji haikutakiwa kuwa hvyo.
 
Kenya wanapanga nyumba kwa kuwa wengi ni maisha ya kati na chini uwezo wa kununua ardhi na kujenga hawana.

Ukilinganisha maendeleo mengine, sisi kwa stendi za mabasi tumewapita sana East Africa nzima. Barabara ndio usiseme. Umeme hapo unamaliza kabisa
 
Back
Top Bottom