Ukweli mchungu Ripoti ya CAG: Wanasubiri tupoe waendelee na mambo yao (business as usual)

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
46,985
144,312
Niwaambie tu, hawa CCM na serikali yao, japo kwa sasa wanaonekana kugawanyika, ila ukweli ni kwamba wote ni wale wale tu (wapigaji), hivyo msitarajie jipya kutoka kwao zaidi ya maigizo ya kuwahadaa kwa muda na kisha waendelee kulindana.

Ripoti za CAG tangu enzi za Kikwete ni madudu matupu, na kwakuwa hakuna hatua serious zinazochukuliwa, ndio maana madudu haya yanaendelea kujirudia kama yalivyojirudia safari hii na kama yatavyojirudia mwakani.

Zinabadilika tawala tu ila ukweli shehe ni yule yule isopokuwa kanzu ndio mpya- chama kile kile na watu ni wale wale na tabia na hulka zao ni zile zile.

Hata yule bosi wa Bandari aliesimamishwa kazi, mwisho wa siku atahamishiwa na kupangiwa kazi nyingine, au hata kurudishwa kwenye nafasi yake.

Mjue tu hawa watu wameshatuona sisi ni vilaza na wajinga tulioshindwa kuungana na kuwa kitu kimoja kuwataka wote wajiuzulu tutafute watu au chama kingine kuongoza hii nchi.

Kwahiyo, kwa sasa wanasubiri tupoe baada ya hizi kelele zinazoendelea kwani wanajua kelele zetu hizi ni maji ya moto ambayo mwisho wa siku ni lazima yatapoa tu.

Huko CCM hakuna wa kumfunga paka kengele kwani wote ni wale wale, na kama unabisha, jiulize ni nani au ni wangapi wamewahi kwenda jela kutokana na ripoti za CAG tangu enzi za Kikwete na hata Magufuli.

Tumekuwa tukitumia nguvu kubwa ku-deal na matokeo badala ya chanzo cha matatizo halafu tunatarajia mambo yatabadilika( insanity)!

Insanity is doing the same thing over and over again and expecting different results- Albert Einstein.

Wazee wa pamba za mabakamabaka mtusaidie kwa kufanya kinachohitajika vinginevyo nchi hii itabaki mifupa mitupu tu

Poleni wadanganyika.
 
Mkuu wewe hauna 'proposals'? Ni wakati wa kupiga maheraa! 🤣😂😂

Ila ki ukweli sisi Watanzania sijui tulirogwa kwa kafara ya aina gani! Yaani pamoja na kashfa hizi zote, mtaani ni kama hakuna lililotokea!
 
Huko CCM hakuna wa kumfunga paka kengele kwani wote ni wale wale, na kama unabisha, jiulize ni nani au ni wangapi wamewahi kwenda jela kutokana na ripoti za CAG tangu enzi za Kikwete na hata Magufuli.
CAG sio mwendesha-mashtaka wala TAKUKURU..uko na mengi sana ya kujifunza kabla ya kujitia umaalim
 
Tatizo kubwa la viongozi wa kiafrika ni uwajibikaji. Huwezi kupewa dhamana halafu ukafanya madudu na bado ukaendelea tu kung'ang'ania ofisi.

Kwanza unatakiwa ujiwajibishe mwenyewe kwa kujiuzulu halafu pili uwajibishwe na jamuhuri kwa makosa uliyofanya.
 
Mkuu wewe hauna

Mkuu wewe hauna 'proposals'? Ni wakati wa kupiga maheraa! 🤣😂😂

Ila ki ukweli sisi Watanzania sijui tulirogwa kwa kafara ya aina gani! Yaani pamoja na kashfa hizi zote, mtaani ni kama hakuna lililotokea!
Tumefundishwa upole wa kipumbavu sn
 
Tatizo kubwa la viongozi wa kiafrika ni uwajibikaji. Huwezi kupewa dhamana halafu ukafanya madudu na bado ukaendelea tu kung'ang'ania ofisi.

Kwanza unatakiwa ujiwajibishe mwenyewe kwa kujiuzulu halafu pili uwajibishwe na jamuhuri kwa makosa uliyofanya.
Ndiyo maana viongozi Africa wanajiwekea kinga kutoshitakiwa.
 
Imarisheni chama chenu mchukue dola 2025.

it is now or never.

mkishindwa kuchukua dola kwenye uchaguzi mkuu 2025 your are done for good
 
Kazi kweli kweli
IMG_20210408_210709.jpg
 
Ndiyo maana CCM hawataki katiba mpya
Huwa nawashangaa mnaofikiria katiba mpya ni suluhisho, katiba mpya itasimamiwa na watanzania kutoka sayari nyingine!?.. hii iliyopo mbona huwa inavunjwa na wananchi wapo kimya!?.. mtu mweusi ni mbinafsi sana hata ubadilishe katiba au uwaweke CHADEMA madarakani wote ni wezi tu.
 
Mbona Kenya wameweza mkuu?
 
Back
Top Bottom