David Ben Gurion
JF-Expert Member
- Nov 1, 2018
- 856
- 1,359
Mkuu umenena Kweli tupu... Kwa wengine hapa Kuna kitu tumejifunzaLiko tatizo moja kubwa hapa. Ndoa ya kweli ni ipi hasa? Mwanaadamu ameuacha msingi wa ndoa tangu kuumbwa ulimwengu na kujifanyia utaratibu wake. Hata yanayojiita makanisa hivi leo yameanguka kwenye mtego huo pia.
Iko amri moja kuu inayosimamia maisha ya mwanadamu hapa duniani:
Mathayo 22
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
³⁷ Akamwambia, Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote.
³⁸ Hii ndiyo amri iliyo kuu, tena ni ya kwanza.
³⁹ Na ya pili yafanana nayo, nayo ni hii, Mpende jirani yako kama nafsi yako.
⁴⁰ Katika amri hizi mbili hutegemea torati yote na manabii.
Sasa mtu anaoa ama kuolewa na mtu ambaye amempenda yeye kuliko kumpenda Mungu, halafu wanajidanganya wamefanana. Huu ujinga unaenezwa mpaka kwenye majumba ya ibada. Ndoa ya kweli ya kati ya wenza wanaompenda Mungu zaidi ya chochote, kwamba hakuna anayeweza kubadili msimamo wa mwingine kuhusu mungutkusudi tu wafunge ndoa. Umegundya kwamba tangu awali ndoa nyingi ni FAKE!?
Ndoa ni tendo la rohoni, kuoana kwa sababu ya sifa za nje pekee ni kumkana aliyeanzisha ndoa. Mke aliye na hofu ya Mungu, anawezaje kuruhusu mawazo ya uzinzi yatawale mwili wake? Ndiyo ilivyo kwa mume pia.
Matthew 22 (KJV)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
³⁷ Jesus said unto him, Thou shalt love the Lord thy God with all thy heart, and with all thy soul, and with all thy mind.
Mpende Mungu wako kwa vitu vitatu:
1. Heart
2. Soul (nafsi - sio roho kama ilivyotafsiri Kiswahili)
3. Mind
Hii ni amri ya kiroho, sio kwa jinsi ya mwili kama Mungu alivyo Roho. Inalenga kujenga mahusiano yetu na Mungu. Ndio maana haiongelei kumpenda KWA MWILI WAKO WOTE. Maeneo hayo matatu yakiwa chini ya mamlaka ya Mungu nani awezaye kukushawishi utende zinaa? Akutongozaye amtongoza Mungu, si wewe!!
³⁸ This is the first and great commandment.
³⁹ And the second is like unto it, Thou shalt love thy neighbour as thyself.
⁴⁰ On these two commandments hang all the law and the prophets.
Amri ya pili ni kujenga mahusiano yetu na wanadamu TUNAOWAONA KWA MWILI. Ni ya jinsi ya mwili:
Mpende jirani yako kama WEWE MWENYEWE UNAJIVYOJIPENDA! Hii inajenga mahusiano na wanadamu wenzetu. Sasa kama mke au mume naye ni mwanadamu basi anaangukia kwenye amri hiyo. Wako watu wajinga kweli kweli ambao wamebadili amri hii na sasa wanapenda wake zao ama wayme zao kuliko Mungu kiasi cha kuwakabidhi mioyo yao.
Ndipo sasa tunakuja kwenye NDOA YA KWELI. Mume anampenda Mungu kuliko mke na mke naye anampenda Mungu kuliko mume. Wote wawili wana hogu ya Mungu, wanaishi katika neno lake. Wajapoooana wanaunganishwa na mapenzi yao kwa Mungu, sio hips wala upuuzi mwingine. Hapa ndipo tunaweza kusema, ALICHOKIUNGANISHA MUNGU, MWANADAMU ASIKITENGANISHE!! Ndipo immeandikwa mke bora atoka kwa Bwana na ni heri kume ampataye mwanamke huyo. Matamko na maagano ya madhabahuni sio kusudio la Mungu, huo ni mpango wa wanadamu tu kama ilivyo madhehebu na uchafuzi mwingine wa aina hiyo.
Study the word of God to be approved.
Amen