Ukweli mchungu: Ndoa za sasa zinaishi kimwili wakati kiroho zilishakufa

Its Pancho

JF-Expert Member
Sep 21, 2018
7,671
2,000
Huu ni ukweli, ukweli utakaowaumiza wengi mliopo na mnaotarajia kuwepo kwenye ndoa.

Ndoa za sasa asilimia kubwa zinaishi kimwili tu na kiroho zilishakufa zamani. Mlikubali kuwa mwili mmoja kanisani. Na roho moja iishi kati yenu

Lakini sasa mnaishi kimwili tu ,roho kila mmoja kaihamisha kwa MTU mwingine. Mwanaume kaihamisha roho yake kwa mwajuma. Mkewe kahamisha kwa chidi boda boda.

Hata mkisema muachane unakuta tayari mna watoto na watapata tabu tu ya bure kulelewa na wazazi wa kambo. Unaona bora muishi hivyo kimwili ni wanandoa ,kiroho mlikwishatengana miaka mitano nyuma. Kila mmoja anaitafuta furaha nje ya ndoa kwengineko apate tulizo.

Funzo: Ukimnunulia mchepuko deli la ice cream, mkeo mletee fridge.
 

DeepPond

JF-Expert Member
Nov 18, 2017
12,503
2,000
Kama ndoa zenyewe ndo hizi unategemea Nini sasa
JamiiForums475699683.jpg
 

Woruu

Member
Aug 14, 2013
35
125
Kuna idadi kubwa sana ya wanandoa wanaishi kwa mateso sana ndani ya nafsi zao. Furaha ya kweli ndani ya mioyo yao HAKUNA.
Nawapa pole sana, msingi imara wa ndoa ni sala, upendo, uvumilivu, ukweli, kujali, subira, amani, kusameheana, kutatua changamoto kwa pamoja, Kusaidiana, kukubali mapungufu kwa kila mmoja, utii kwa pande zote mbili, wazazi na ndugu pia, uwajibikaji wa kutekeleza majukumu. (me,ke)
uwaminifu.

Hakuna usomi kwenye ndoa, walengwa wanapaswa watambue lengo mahususi la ndoa, wanaingia kufanya nn, matarajio baada ya ndoa, Ukuzi na malezi, watoto watasomaje, wataishije lazima walengwa wazingatie,

Familia bora hutokana na malezi bora ya wazazi.

ndoa ni muunganiko wa watu wa wiwili kwa hiari yao wenyewe wanaoridhia kushi kwa pamoja kwa maisha yao yote.
 

Dorrlyn

JF-Expert Member
Jan 10, 2017
1,094
2,000
Mapinduzi ya wanawake kutakiwa(kutaka) kutawala yamechangia pakubwa, kibaya zaidi wanaume nao wameamua kwa makusudi kabisa kukimbia majukumu ya ubaba. Mungu atusaidie😔

Waanzilishi wa yote haya ni wanaume kama wanaume wangefuata vile Mungu amewapa majukumu yao hayo mapinduzi tusiyengasikia kokote pale.
 

Date20210317

JF-Expert Member
Nov 7, 2018
3,860
2,000
Vitu vingine mnaviongea hata sio level zenu.et KIROHO!! Do u really know/ understand what this stuff is!!?
Au ulikua una maanisha kitu kingine?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom