Ukweli mchungu: Ndoa bila watoto sio ndoa

The Businessman

JF-Expert Member
Jan 9, 2014
7,404
9,233
Wakuu salama

Kuna ukweli watu hatutaki kuusema, ndoa bila kuwa na watoto sio ndoa hiyo. Watu wanahangaika usiku na mchana kutafuta watoto ili tu kunusuru ndoa isivunjike.

Wanaume na wanawake ni vema kwanza kabla hamjaanza maandalizi ya ndoa muhakishe mna hata mtoto mmoja.
raha ya ndoa uwe na watoto, kama ujana wako uliuchezea kwa kuchoropoa mimba hovyo hovyo sasa ndio utakuja kuikumbuka.

Wanaume tasa wapo ila mara nyingi wao utasa wao ni wa kibiological kuliko wanawake ambao wao utasa wao mara nyungi ni wa kutengenezwa.
 
Haki ya mama dah! ni kweli mengine tunayataka wenyewe mengine ni majaaliwa ya Mungu jamani
 
Mmmmmh.. wapo wenye vizazi vyao, kila kitu kipo sawa na mtoto bado asipatikane. Hawakukosea kusema mtoto/watoto ni majaaliwa. Kitu kingine, pamoja na mtoto/watoto, mwisho wa siku wanakuwa na kuondoka nyumbani, mnabaki wawili mnatazamana. Kinachotakiwa upendo bwana katka ndoa hiyo, watoto wawepo au wasiwepo
 
Mtoa mada kajipange upya

Kwanza hakuba ukweli katika ukweli wako mchungu unaosema

Itbis only a call of nature kwamba watoto wanapatikana iwe nje au ndani ya ndoa

Kusudio la.kwanza la.ndoa sio watoto bali ni mwanamke na mwanaume waambatane wawe mwili mmoja.....watoto ni zawadi tu

Kwa hiyo kwa wenye ndoa ambao hawana watoto wasikwazike ni kwamba Mungu hajaamua kuwapa zawadi hiyo.

NB nina ndoa na nina watoto
 
Ngoja nijipange.
 
Afadhali hapo mwisho ume-declare interest kwamba umeoa na una watoto. Sijui mwanaume ambaye ameoa na hawajabatika kupata mtoto/watoto atasema nini.

Tukumbuke issue ya ndoa katika mila na desturi zetu za kiafrika ni zaidi ya mume na mke. Pressure ya kutokuwa na mtoto mara nyingi inatoka kwa ndugu, hasa wa mwanaume! Ndipo lile tusi maarufu huja - mwanamke gani anajaza choo tu. Kibaya zaidi, ndugu wa kike wa mwanaume (mama, dada, shangazi) ndio washika bango wakubwa.

Mwishoni shinikizo la ndugu humkumba mwanaume asiye na msimamo.
 
Ndio kuna ndugu nimewaona ndoa zao zipo hatarini kuvunjika kisa hawapati watoto.

Inatokea sana lakini pia huleta faraja kwa wengine. Baada ya kuachana, mwanamke anapata mtoto mbele ya safari na mwanaume anazaa na mwanamke mwingine - sijui hilo linaelezewa vipi?
 
Nenda shule upya ukajifunze maana ya "NDOA" ... naona uliondoka kabla darasa halijakamilika. Hope hujaoa/kuolewa, ukioa/olewa mahari ikatolewa ukavalisha/wa pete, ukaenda kanisani/msikitini ndo utajua kama unaoa kwa ajili ya watoto ama kwa ajili yako mwenyewe ... watoto ni zawadi ya ndoa kutoka kwa MUNGU as well as temporary assignment for your marriage, Ndoa ya zote ni muunganiko wa hiyari wa watu wawili na MUNGU wao, watoto wenyewe watakuona chizi kama unawapenda sana wao kuliko Mama/Baba yao.

Tafuta amani na mwenza wako, mpende Mume/Mke wako unconditionally, pendaneni unconditionally halafu utaona jinsi maisha yalivyo matamu hata kama hamna hao watoto unaowazungumzia.

NB:Nina ndoa bila mtoto, muda ukifika watakuja but kwa sasa nafikiri bado tunahitaji kuwa wawili kwanza.

(Ni mtazamo binafsi)
 
Back
Top Bottom