Ukweli mchungu: Mwanamke ama Mwanaume kama huna hela wewe ama Wazazi wako utaoa/kuolewa na maskini mwenzako

FRESHMAN

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
8,820
33,455
Habari wadau.

Nipo sehemu moja napata moja moto.. kuna jamaa katusua kapanda cheo kazini huko auditing firm moja kubwa , yupo early 30s anadai muda wa kuoa umefika, anadai lazima aoe mwanamke mwenye kipato kama chake ama amzidi yeye mwanaume kipato.. maana watu wanapenda sana kuvuna wasichopanda.. yeye anaona bora achunwe na mwanamke mwenye hela kuliko kuchunwa na mwanamke maskini.

Pia, nikajaribu kuwaza harusi nazoziona za walionizunguka, unakuta kama bwana harusi ni mtoto wa tajiri kama kimei anafunga ndoa na binti wa tajiri mwenzake kama matemba wa victoria oil.. nawaza dada zangu mimi maskini na ndoto zao za kuolewa na wenye pesa zitatimia kweli? ama wanaume kina sisi wa uswazi kuoa wanawake wenye pesa zitatimia kweli?

Ushauri wa wazi kama unataka maisha mazuri kwenye ndoa yako ni lazima wewe mwenyewe uwe na uwezo wa kujipa hayo maisha mazuri kabla hujaoa ama kuolewa, kwa sababu hakuna anaesaini mkataba husio na win win situation zama hizi kisa mapenzi
 
Mapenzi yasikie tu hakuna cha tajiri wala maskini


Mkate mkate tu unatafunwa na yeyote maskini au tajiri
 
Wanaangalia status zinazoendana.
We pata picha binti was tajiri amtoe kijana tandale uswahilini akamtambulishe kwao masaki..
Pata picha kijana msomi tajiri hadi kwao amtoe binti wa muuza GENGE uswahilini akamtambulishe kwao..

Ni ngumu sana hasa kwa mlengwa ambae ni maskini,labda mambo yaende tofauti tu.but ni ngumu sana
 
Wanaangalia status zinazoendana.
We pata picha binti was tajiri amtoe kijana tandale uswahilini akamtambulishe kwao masaki..
Pata picha kijana msomi tajiri hadi kwao amtoe binti wa muuza GENGE uswahilini akamtambulishe kwao..

Ni ngumu sana hasa kwa mlengwa ambae ni maskini,labda mambo yaende tofauti tu.but ni ngumu sana
Haya mambo inategemeana na mazingira zaidi ndio maana hata videmu vya ushenzini vinaenda GYM za Mikocheni, Kawe ama kujiunga na jogging club za ushuani huko! 😅😅😅 Watu hawachezi mbali na fursa
 
Nakumbuka kuna jamaa alikuwa na maisha mabovu sana akapata mtoto wa kishua harafu yule mtoto familia ikamtenga kisa ameolewa na jamaa ambaye maisha ni mabovu hata mlo hakuna, ila demu alikomaa na mmr wake huyo fukara, Mambo yalivyo kuja badirika baada ya kuzaa mtoto wa kwanza tu jamaa akapata mchongo kwenye kampuni ya wachina Neema ikaingia baada ya mda ameachana na wachina amepata dili UN,
anapiga kazi nje ya nchi, maisha ya wale wazazi wa mke wake yakabadilika kama kuimba ni kupokezana, wamefulia mpaka basi hawana lolote,
Jamaa anamuheshimu mke wake asikwambie mtu na anampenda sana.
sasa wewe endelea kukalili maisha ambayo Mungu anayeyapanga haujawahi kumuona kwa macho
 
Usawa haujawahi kuwepo, alijisemea DR.Kumbuka “Hamna mtu asiyependa kula pazuri jamani”
Hahahaa we uchebe saizi yako shilole..usijitakie kutekwa ukatupwa mtaroni bure.
Mtu unaenda ukweni unaulizwa babako ana proffesion gani unajibu "ah yupoyupo tu"

Na wewe je? "Ah kuna Moshe Moshe flank tu napiga"
Watakuelewaje
 
Hahahaa we uchebe saizi yako shilole..usijitakie kutekwa ukatupwa mtaroni bure.
Mtu unaenda ukweni unaulizwa babako ana proffesion gani unajibu "ah yupoyupo tu"

Na wewe je? "Ah kuna Moshe Moshe flank tu napiga"
Watakuelewaje
Hahahahah cha muhimu mmependana tu jamani! Nyie ndio mnaofanya ndoa ziwe ngumu kwa akili hizi🤣🤣🤣
 
Haya mambo inategemeana na mazingira zaidi ndio maana hata videmu vya ushenzini vinaenda GYM za Mikocheni, Kawe ama kujiunga na jogging club za ushuani huko! Watu hawachezi mbali na fursa
Maandishi yako yanaakisi jina lako hakika unatenda vyenye inatakiwa kutenda
 
9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom