UKWELI MCHUNGU KUHUSU MAISHA YETU YA KILA SIKU

DIDAS TUMAINI

JF-Expert Member
Nov 11, 2014
230
583
FACTS CHACHE KUHUSU MAISHA.

By Malisa GJ,

1. Watu wengi wanaojitapa kuwa wana fedha nyingi, ukweli ni kwamba hawana fedha. Wenye fedha huwa hawajitapi. Huwezi kumuona Bill Gates akijiita ‘don’ au ‘money maker’. Hata kwa Tanzania huwezi kuwaona matycoon kama kina Mengi Bakhresaa au Manji wakijiita ‘dons’. Lakini jamaa wa Yombo Buzza kwa mama kibonge akipata milioni mbili atajiita majina yote ya kuonehsa ana hela, na msipomuelewa atapiga nazo picha apost mitandaoni.

2. Watu wengi wanaojitapa kuwa wazuri si wazuri. Ukiona mtu anajiita ‘pretty, cute, beautiful’ na majina yanayofanana na hayo ujue hamna kitu hapo. Wazuri huwa hawajitangazi. Ukimuona tu utajua ni mzuri. Historia ya dunia inaamini mwamnamke mzuri kuliko wote aliyewahi kutokea ni Malkia Cleopatra wa Misri.

Wanahistoria wanaamini tangu dunia iwepo hajawahi kutokea mwanamke mzuri kama Cleopatra. Lakini hakuwahi kujiita mzuri. Mara zote alipoambiwa ni mzuri alikataa. Lakini kutana na kibinti cha Mbagala rangi tatu, kimepaka wanja wa jero na poda ya mia mbili hamsini, kanajiita cutelecious, baby beautiful, na majina mengi ya kutaka kuonesha kwamba ni mzuri.

3. Watu wengi wanaopenda kuonesha kuwa wanapendana, mara nyingi hawapendani. Ukiona mtu kila mara anaandika jinsi anavyompenda mkewe, mumewe, mchumba, mchepuko wake wake ujue kuna walakini. Wanaopendana kweli hawapotezi muda kuiambia dunia wanavypendana, bali hutumia muda mwingi kuoneshana wanavyopendana kwa matendo.

Badala ya kupost kila mara kuonesha namna unavyompenda mkeo/mumeo, mfanyie vitu vitakavyomfanya aone kweli unampenda. Hii haimaanishi usimpost kabisa, hasha. Mpost mara chache, lakini tumia muda mwingi kumuonesha physically unavyompenda kuliko unampost lakini ukirudi nyumbani mnalala mzungu wa nne.

4. Watu wengi wanaopenda kuonekana ni wababe au wana nguvu mara nyingi huwa dhaifu. Ukiona mtu kila mara anajisifu kwamba ana nguvu na mbabe, huyo anaweza kupigwa hata na mtoto. Wababe huwa hawapotezi muda kujisifia, wao huonesha ubabe wao kwa vitendo. Wakati Marekani inaivamia Iraq mwaka 2003, aliyekuwa Waziri wa habari Mohammed al-Sahhaf aliitangazia dunia kwamba hakuna mwanajeshi hata mmoja wa Marekani atakayerudi kwao akiwa hai.

Akawauliza wamarekani je kwao hakukuwa na makaburi hadi wajipeleke kwenda kufia Iraq? Lakini kilichotokea sote tunajua. Alidakwa kama kuku, wakati boss wake Saddam Hussein alipoenda kujificha kwenye shimo kama panya buku. Wababe huwa hawasemi, wanafanya.

5. Watu wengi wanaopenda kuonekana wana hekima mara nyingi hawana. Mwanafalsafa Daniel Dennett aliwahi kusema sifa ya kwanza ya kumjua mtu hana hekima ni mtu huyo kujisifia kuwa na hekima. Baba wa Falsafa duniani, Socrates ambaye inaaminika alikuwa na hekima sana, alipoulizwa alikataa. Mfalme Suleimani ambaye inaaminika ndiye kiumbe mwenye hekima zaidi kuwahi kutokea duniani, hakuwahi hata mara moja kujisifu kuwa na hekima.

Hata Malkia wa Sheba alipomtembelea na kumsifu kuwa na hekima, Sulemani alikataa, na kusema hadhani kama anazo sifa hizo. Lakini hapa bongo kijana wa Buguruni malapa akipata nafasi ya kuhutubia mahali na watu wakamsikiliza akitoka hapo anajiita Wiseman, wisegirl, wise woman, wise, wise, wise. None sense.!

6. Watu wengi wanaopenda kuonekana wacha Mungu mara nyingi ni wanafiki. Wacha Mungu wa kweli hawapotezi muda kuionesha dunia jinsi walivyo wacha Mungu, bali hutumia muda wao mwingi kumcha Mungu wao kwa matendo. Ukiona mtu kila mara anasema 'mniombee, mimi ni mpenzi wa Mungu' ujue hapo hakuna kitu.

Nabii Elia alikua mcha Mungu sana na alinyakuliwa kwenda mbinguni bila kuonja mauti, lakini hakuwahi kujitapa kuwa mcha Mungu, bali matendo yake yalimfanya ajulikane kuwa ni mcha Mungu. Lakini leo kuna watu kila wakipewa microphone utawasikia 'mniombee, mimi ni msema kweli, mimi ni mcha Mungu'. Hakuna kitu.!

7. Watu wengi wanaojifanya kuchukizwa na tabia fulani hadharani, mara nyingi wao ndio wenye hizo tabia. Kwenye kile kilichoitwa 'vita ya ushoga' tuliona walewale waliowahi kutuhumiwa kuwa 'hawana marinda' ndio haohao walikuwa mstari wa mbele kupinga ushoga.

8. Watu wengi wanaoandika mitandaoni 'nifollow kusoma makala zangu nzuri" usipoteze mufa wako. Wanaoandika makala nzuri huwa hawaombi watu kuwafollow. Kama mtu unaandika 'chakula kizuri cha ubongo' watu watakufollow tu bila kuombwa.

Tuna waandishi magwiji humu mitandaoni ambao mara nyingi mimi najifunza kwao, kama kaka Fadhy Mtanga, mzee wangu Mohamed Said, mwanahistoria Francis Daudi, Dada zangu Happy Wa Joseph, Laura Pettie, Gwiji Markus Mpangala, Christopher Cyrilo, Thadei Ole Mushi, na wengine wengi. Wanaandika mambo ya msingi sana lakini hata siku moja sijawahi kuona wameomba watu kuwafollow. Sasa wewe hata kupangilia sentensi huwezi unaomba watu wakufollow?

9. Watu wengi wanaopenda kujisifu kuwa na akili nyingi sana mara nyingi hawana. Wenye akili huwa hawajisifu bali huonesha uwezo wa akili zao kwa vitendo, halafu husifiwa na watu wengine. Albert Einstein aliwahi kuulizwa kama yeye ni 'genius' akakataa katakata. Lakini Donald Trump mwaka jana alitamka kuwa yeye ni extra genius. . Bila shaka kati ya hawa wawili tunamjua genius halisi ni nani.

10. Watu wengi wanaojitapa kuwa wazalendo ni wachumia tumbo. Wazalendo huwa hawajitapi bali wanapewa heshima hiyo na wengine. Mwalimu Nyerere aliitwa mzalendo, hakujiita. Wapigania uhuru wengi waliojitoa kwa jasho na damu kufanikisha harakati za ukombozi hawakuwahi kujitapa kuwa wazalendo. Waliitwa hivyo kwa matendo yao. Lakini leo mtu akishakuwa na kadi ya chama chakavu, akashona na shati lake la kijani, refu kama la kuendea kwenye sendoff anajiita mzalendo na anajiona ana haki kuliko raia wengine. Upuuzi.!

Malisa GJ

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dah ukweli wenyewe ndio huu. Japo wataupinga but yes.. hii ndio jamii tunayoishi kwa sasa. Mtu yuko tayari kujitoa ili aonekane tajiri.. lakin hayuko tayari kujitoa awe tajiri.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom