Ukweli mchungu kuhusiana na mradi wa Stiegler's Gorge

Hujui thamani ya mazingira mpaka siku uwe na jangwa kama sudani au mali.

Tanzania ina options nyingi za kutengeneza umeme. Kwanini msifikirie Solar? Wind Turbines? Gas? Hizo zote ni sustainable means to get electricity without the expense of environment.

Fanya yote ila usichezee mazingira. Kizazi kinachokuja kitajuta.

Sent using Jamii Forums mobile app
China na marekani wanazalisha hewa chafu inasafishwa huku na south america kwasababu ndiko kwenye miti. Lakini mataifa hayo ndo yenye uchumi imara. Bora na sisi tuchafue mwishowasiku tutajua tunaishi vipi. Hatuwezi kuwa omba omba milele

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kwa hilinnapingana na jiwe huwezi haribu mazingira unakata miti eneo ukubwa kama mkoa wa dar... unazani miaka kumi sijazo tutakuaje?? kwani sini gesi ipo inawezaa tumika hadi miaka 100 ijayo kwanini tusiitumie hiyo au kaona kwenye mradi huo kuna pesa kubwa ataipiga sana... maana kila raisi hukuja na mbinu yake ya miradi ili kupitia miradi hizo apige pesaa waliopita walidili na gesi na yeye kaona adili na hii bwawa... tusifanye mambo kwa kukurupuka tuangalie na athari ya mazingira gesi sini ipo ?? au gesi sio yetu yaani umeme wa gesi unaaminika duniani sisi tunayo lita na lita za matrillion zinazoweza tumika hata miaka 100 ijayo... kweli?? kwa hili hata kama ni mabeberu wapo sawa kusema hili hata kama mkiritafakari kwa upande wa kusema hawaitaji tukajiendeleza kimaendeo hakika tutakuwa tumekosea gesi mtwara ipo tuitumie hiyoo kuliko kuharibu hifadhi ya selous naambatanisha video clip ya zitto kabwe




clip ya nape nnauye akitahadharisha ukataji miti
Bei ya gas unajuwa wewe. Gharama ya kuzalisha umeme na maji Vs Gas Bora maji. Kutumia gas ni kujitengenezea mazingira ya unasikini kwa taifa letu!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
La msingi hapa ni umuhimu wa EIA kabla na baada ya JPM. Kwa spidi ya JPM ya utekelezaji wa mradi huu sidhani kama hilo kwake lilikuwa muhimu.
Hili ndilo tatizo kubwa sana la Magufuli. Kupuuza taratibu na sheria. Hili linamharibia sana hata katika kupanga na kufanya mambo mazuri. Yeye hawezi kuwa mjuaji wa kila kitu. Hili ni tatizo baya sana kwa upande wake.
 
China na marekani wanazalisha hewa chafu inasafishwa huku na south america kwasababu ndiko kwenye miti. Lakini mataifa hayo ndo yenye uchumi imara. Bora na sisi tuchafue mwishowasiku tutajua tunaishi vipi. Hatuwezi kuwa omba omba milele

Sent using Jamii Forums mobile app
Ujerumani, Uingereza, Marekani, Japan, n.k., walichafua sana mazingira halafu wakasafisha. Kwa nini na sisi tusiweze kufanya hata nusu yauchafuaji waliofanya wao ili tujikwamue na hii hali ya umaskini? "Environmental Remediation Technology" sasa hivi imeendelea zaidi ya wakati huo walipokuwa wanachafua. Sisi tutaitumia.
 
Ni watz hawa Hawa waliouvuruga mradi wa gesi hadi usikidhi mahitaji.Leo hii watz hawa msiojua kusimamia mambo mnataka kuteketeza eneo la ukubwa wa Dar ili kuanzisha mradi mpya!
Mimi naomba muanzishe mradi wa kubadili vichwa vyenu kwanza halafu mrudi kwenye gesi mkarekebishe uozo mlioufanya kabla ya kunishawishi kuteketeza mamilioni ya miti na viumbe wanaotegemea ikolojia yake.
I can't buy that!
 
Ni hivi watu wengi wanaandika bila kuujua ukweli.

Ukweli ni kwamba kabla ya mradi wowote mkubwa kutekelezwa lazima kifanyike kitu kinachoitwa Environment Impact Assessment.

Ukweli ni kwamba serikali iliunda team iliyojumuisha maprofesa nguli kufanya Environment Impact Assessment ambapo serikali yetu iliwalipa fedha kufanya kazi hiyo.

Ukweli ni kwamba team hiyo ilifanya kazi hiyo na kuandika ripoti yake ambayo ilieleza kwamba madhara ya kwnye mazingira kama mradi huu ukitekelezwa yatakuwa makubwa sana hivyo wakashauri mradi huu usitekelezwe na wakashauri serikali ijikite kwenye kuzalisha umeme kwa kutumia gesi ambayo inapatikana mtwara kwani uzalishaji wa umeme kwa kutumia umeme hautakuwa na madhara kwenye mazingira kama mradi wa stiglers gorge.

Sasa bana ripoti hii iliwasilishwa kwanza wizara inayohusika na mazingira ya bwana January.

Waziri akakubaliana na ripoti naye akaifoadi ikulu.

Bwana kolichotokea almanusura huyu jamaa apoteze kazi, .

Ukweli ni kwamba jiwe alimuita akamtukana sana kwanini amekubaliana na ushauri wa hao maprofesa na kisha akamtupia ripoti yake .

Isingekuwa aibu ya jiwe akifahamu jinsi January alivyomfanyia figisufigisu ya kutengeneza matokeo yaliyomsaidia kumuweka madarakani pale mlimani city huyu january alikuwa afukuziwe mbali.

Sasa twende kwenye hoja, kwa nini serikali yetu inakataa repoti ya timu ya iliyoiunda na kuilipa ifanye kazi na wao wakafanya na wakashauri.

Mbona Serikali hiii hii haitoi vibali vya kuendeleza miradi ambayo environment impact assessment zimeshauri kwamb arhari za mradi ni hasi.

Kuna msemo wa kiingereza unaoheshimika sana unaosema "no research no right to speak"

Research imefanyika imeeleza mradi ni mbaya kwenye mazingira watu bila hata kufanya research nyingine wanakurupuka kuukataa ushauri wa wataalamu.

Tusiwalaumu sijui bunge la ujerumani , mimi binafsi siungi mkono kupangiwa mambo yetu na hao wajerunani.

Ukweli ni kwamba mradi huu ulikataliwa kwanza na timu yetu sisi wenyewe watanzania iliyohusisha maprofesa wataalamu ambao mwisho wa siku kama kawaida ya jiwe ukitoa mapendekezo tofauti na mtazamo wake unaitwa sio mzalendo au sijui umetumwa na mabepari.
Aina hii ya uongozi ya kukataa mapendekezo ya wataalamu ni mojawapo ya element za utawala wa kidikteta.
 
Mimi nimeosoma ripoti ya WWF kuhusu mradi huu, kama katiba tuu imeweza kukanyangwa na tuko ok kabisa, what is EIA compared?.

Kwenye hili mimi naungana na serikali yetu kuwa Tanzania is a sovereign state, tutaamua mambo yetu wenyewe bila kuingiliwa au kupangiwa na mataifa ya nje.

Natolea mfano wa mradi wa Kamba Samaki, shrimp farming kwenye Rufiji Delta, ulipitishwa vizuri tuu, lakini kabla ya utekelezaji, mashirika ya kimataifa ya mazingira yakaja na EIA nyingine, tukapigwa stop mradi ukafa. Hoja ya wanamazingira ni kilimo kile kingeathiri uoto wa asili wa mikoko.

Ukiangalia cost benefits na value benefits za mradi na faida za mikoko, mikoko are nothing compared.

Kama ulifuatilia issue ya Kihansi Hydro Electric Project, mradi ulichelewa sana kwa hoja ya vyura wa Kihansi hadi Marekani walipokubali kuwa relocate wakahamishwa, mradi ulipokamilika wakarudishwa. Ukiangalia faida za nchi inayohitaji umeme na faida ya vyura ni nothing compared.

Sasa kwenye Stieglers ni vile vile wanataka kutupangia, kule nyuma waliweza kwa sababu fedha walikuwa wanatoa wao. Kwa Stieglers, watakwama kwa sababu this time around fedha ni zetu.
Hili jambo niliisha lizungumza sana humu

Uzalendo wa kweli wa nchi yako ni pamoja na kusupport mipango kamambe
ya maendeleo ya nchi yako hata kama mipango hiyo itasababisha maumivu kwa walio wengi as long as itakuwa na faida kubwa kitaifa huko baadae.
P
Pascal,

Ebu fanya research ni kwa nini viwanda vya korosho vilivyojengwa wakati wa Hayati Mwalimu Nyerere kule Mtwara, Lindi n.k. vilishindwa kufanya kazi wakati tunavianzisha kama taifa. Na unajua ni kwanini nchi yetu ilifutiwa madeni wakati wa Mkapa? Kalagabao!
 
Mradi huu unasemekana unaharibu Mazingira kuharibu mazingira na kuharibu Viumbe hai.

Mradi huu UNESCO wamezungumzia na wanajua unaharibu sana, ndiyo maana hata tenda ya ujenzi makampuni makubwa yalihofu sana, yakashindwa na mwishowe kampuni ya ARAB COntractors ambayo ni WASTAAFU WA JESHI huko Misri wakaamua kuchukua,.

hii kazi itawagharimu sana, Na huyu mkuu wetu wa nchi anatupeleka shimoni
 
Acha kupotosha watu wewe. Uharibifu gani wa mazingira uliofanywa pale.
Kemea hao ndugu zako wanaokata magogo hapo kijijini kwako kwa kuchoma mkaaa.
Kwa kifupi hakuna best project anayoifanya Magu Kama hiyo. Kati ya zote hiyo kwangu it's number one
 
Tatizo wabongo wengi mnadandia Mambo kwa miheuko.
Wakati dunia inaubwa sehemu kubwa ya makazi yetu yalikuwa ni misitu waishiyo wanyama. Hao uko majuu washamaliza mapori yote, wanaongoza kwa air pollution. Wamefyeka misitu kikubwa ili waweke makazi ya watu. Leo hii sisi kufanya hili la kimaendeleo limekuwa nongwa?
 
Huo mradi kwa taarifa yako utawasaidia sana hata hao wanyama waishiyo hapo. Kutajengwa bwawa kubwa ambalo maji hayatakuwa yanaisha na ule uhaba wa maji kwa wanyama kipindi Cha kiangazi kikali utakuwa haupo.
 
Unajua kuwa mto Rufiji ulisababisha mafuriko huko LINDI kwa sababu ya deforestation iliyofanyika kwenye hiyo project.
Acha kupotosha watu wewe. Uharibifu gani wa mazingira uliofanywa pale.
Kemea hao ndugu zako wanaokata magogo hapo kijijini kwako kwa kuchoma mkaaa.
Kwa kifupi hakuna best project anayoifanya Magu Kama hiyo. Kati ya zote hiyo kwangu it's number one
WANAOJUA ZAIDI KARIBUNI KWA MJADALA

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom