SoC01 Ukweli mchungu juu ya Nukta 3 za Kiuchambuzi kuhusu Mapinduzi ya Viwanda Tanzania

Stories of Change - 2021 Competition

The Festival

Member
Aug 30, 2021
27
98
UTANGULIZI
Kila sifa njema anastahiki Mwenyezi. Ama baada, ningependa kuzibainisha nukta 03 zitakazo chambuliwa katika mnakasha huu.

01) Mapinduzi ya Viwanda kwa ujumla wake.
02) Hali ya Mapinduzi ya Viwanda Nchini Tanzania.
03) Mtazamo Juu ya Nini Kifanyike.

01) MAPINDUZI YA VIWANDA KWA UJUMLA WAKE
Mapinduzi ya Viwanda ni mchakato wa mabadiliko unao tawaliwa na viwanda na matumizi ya mashine katika uzalishaji (Adam Zeidan na Wenzake, 2021). Mapinduzi ya Viwanda mpka hivi sasa yamepita katika awamu kuu 04.

AWAMU YA KWANZA YA MAPINDUZI YA VIWANDA:
Mabadiliko makubwa yalitokea mwishoni mwa karne ya 18 (mwaka 1760). Matumizi ya mashine yalikua ndio kichocheo kikubwa kwa mapinduzi haya ambayo yalipelekea viwanda kuwa uti wa mgongo wa uchumi badala ya kilimo. Kulishuhudiwa uvumbuzi wa matumizi wa makaa ya mawe, nishati ya maji, na injini mvuke (steam engine).

AWAMU YA PILI YA MAPINDUZI YA VIWANDA:
Ilianza mnamo karne ya 19 mwishoni hadi karne ya 20 mwanzoni (Mwaka 1870-1914). Uzalishaji mkubwa wa bidhaa ulishuhudiwa. Vilevile vyanzo vya nishati vilivumbuliwa, ikiwemo umeme, gesi, na mafuta.

AWAMU YA TATU YA MAPINDUZI YA VIWANDA:
Ilianza ndani ya nusu ya pili ya karne ya 20 (Mwaka 1950). Mapinduzi haya yalileta uvumbuzi wa vifaa vya umeme (Electronics), mawasiliano ya simu (Telecommunication), na Tarakilishi (Computers).

AWAMU YA NNE YA MAPINDUZI YA VIWANDA:
Leo hii tumo ndani ya awamu ya nne. Dunia inashuhudia maendeleo makubwa ya teknolojia, miongoni mwao ni uvumbuzi na maendeleo ya matumizi ya Roboti, akili bandia (Artificial Intelligence), Internet of Things (IoI), Big Data, Blockchains, Cloud Computing, Autonomous Vehicles, 5G Networks, na kadhalika.

02) HALI YA MAPINDUZI YA VIWANDA NCHINI TANZANIA
Nukta hii ni kuntu katika kuelezea kwanini kichwa cha habari cha mnakasha huu kimeitwa "Ukweli Mchungu juu ya nukta tatu kuhusu Mapinduzi ya Viwanda Tanzania".

Awali ya yote, tukitizama elementi zilizopo kwenye awamu ya kwanza ya Mapinduzi ya Viwanda, matumizi ya makaa ya mawe, nishati ya maji na injini mvuke, Tanzania inajitahidi kutekeleza. Lakini kwenye matumizi ya mashine, Tanzania bado kuna unautata.

Kiasi kwamba bado kilimo kinabaki kua uti wa mgongo wa uchumi wa taifa hili badala ya viwanda. Sensa iliyofanywa mwaka 2012 inaonesha zaidi ya 65% ya watanzania ni wakulima na wengi wao wanatumia jembe la mkono na kutegemea mvua za msimu katika kilimo (IPP Media, 2019). Hii si dalili nzuri, kwani shida hizi za matumizi madogo ya mashine ni shida za miaka ya 1760, lakini sisi Tanzania leo karne ya 21 tunapambana kutatua changamoto za karne ya 18.

1517080_received_1354667647949552~2.jpeg

(Picha: Mtandaoni)

Mbali na hayo, tukiangazia baadhi ya elementi ambazo zipo katika awamu ya pili. Uzalishaji wa bidhaa bado Tanzania ni mdogo sana. Hii ni kutokana na sababu mbali mbali ikiwemo kiwango duni cha elimu, matumizi madogo ya umeme, ubora wa bidhaa kwa ajili ya kuuzwa nje (export), pamoja na kiwango cha riba (Karger na Dante, 1977). Vilevile sababu nyengine ni hali ya soko la ajira, na umadhubuti wa exchange rate (Samouel na Aram, 2016).

Elementi nyengine zilizopo katika awamu ya pili ni kugundulika kwa vyanzo vya nishati kama umeme, gesi, mafuta. Vyanzo hivi kwa nchi zilizo endelea vinatumika kwa kiwango kikubwa. Bila kupepesa macho ipo wazi kuwa umeme wa Tanzania ni wa kusua sua. Mbali na migao ya umeme ya hapa na pale lakini pia ukiambiwa kunguru walicheza wakakata umeme, wala hupaswi kushangaa. Hali hii pia si ishara nzuri kwa maendeleo yetu kwani haya ni matatizo yaliyokuwa yakitatuliwa katika miaka ya 1870-1914, lakini sisi mpka leo 2021 bado ni changamoto kubwa.

Tukiendelea kusonga mbele, tutizame elementi zilizopo katika awamu ya tatu ambazo baadhi yao ni uvumbuzi wa vifaa vya umeme (electronics), mawasiliano ya simu (telecommunications), na Tarakilishi (computers). Mambo yote haya yalianza kuvumbuliwa katika karne ya 20 kuanzia mwaka 1950. Maajabu yaliyoje Tanzania ya leo ina sheria na tozo nyingi juu ya matumizi ya vifaa vya umeme kama simu na tarakilishi (computers), badala ya kuwa na sera na jitihada nyingi za kuchochea maendeleo na matumizi ya vifaa hivyo.

Hivi sasa dunia shuhudia awamu ya nne ya Mapinduzi ya Viwanda, huku mabadiliko yakiwa ni katika uvumbuzi na matumizi makubwa ya internet na vitu vilivyounganishwa na internet (Internet of Things), 5G Network, teknolojia ya 7D, na mengine mengi. Lakini ndani ya nchi yetu pendwa tunakumbana na mfumo ambao huzungumzwa maneno yanayo onesha nia ya kutaka kuendana ya awamu hii ya nne ya Mapinduzi ya Viwanda, lakini kwenye utekelezaji hapo ndipo kisanga kilipo. Twende na mifano hai;

MFANO WA KWANZA:
Serikali ya Tanzania kupitia TCRA inampango wa kueka sheria ya mafundi wa kukarabati simu kuwa ni wale tu walio na leseni, waliosoma Veta na DIT (jamiiforums, 2020). Sasa tujiulize kwa mfumo huu na utaratibu huu je wale mafundi wenye weledi ambao hawakupitia DIT wala Veta wafanye kazi gani. Hapa tunaona kua vyeti vimepewa thamani kubwa zaidi ya ujuzi na stadi ya kazi. Vile vile hapa tunaona sera itakayo chochea ukosefu wa ajira. Mbali na hilo hapa tunaona mpango utakao wafanya vijana wenye vipawa na ujuzi walioupata kwa njia zisizo rasmi wakivunjwa moyo kutokua wabunifu zaidi. Je, ni taifa gani lenye maendeleo pasi na ubunifu na uvumbuzi? Viongozi na watendaji wa serikali wana nia gani kwa sera kama hizi?

Screenshot_20210831-025226_Instagram~2.jpg

(Picha: Jamiiforums)

MFANO WA PILI:
Matumizi ya ndege ndogo zisizo na rubani (drones).
images (1).jpeg

(Picha: Jamiiforums)


Kuendesha drone nchini Tanzania hata kama ni kwa ajili ya kupiga picha za kawaida au za kikazi basi ni bora uwe na gongo refu sana utundike kamera kisha ndio upige picha. Kwasababu mlolongo wake ni mzito; usomee, upate kibali, kibali sio bure, ufanye hiki na kile mpka una paisha drone Tanzania, ndugu yangu jasho limekutoka. Kwa muenendo huu, vijana wabunifu wataogopa hata kupaisha vishada. Lakini nchi za wenzetu, wadau wanavumbua vitu vipya kwa ajili ya nchi zao kila asubuhi.
Screenshot_20210831-025216_Instagram~2.jpg

(Picha: Mtandaoni)
(Hili ni jeshi la marekani likifanya kazi na mbwa roboti, ambae anaweza kufika eneo la tukio kubaini kama kuna maadui au la.)



(Video: BBC)
Tukiwa katika mazingira ambayo sheria zinatungwa kujilinda zaidi kisiasa, basi tutakua tunakataa mabadiliko chanya zaidi kuliko kuchochea maendelea. Leo imekuja drone tu sheria kibao, kiasi kwamba hata kama ukapewa zawadi ya drone na rafiki yako au ndugu alie nje ya nchi kwa lengo upige hatua bado utakutana na vikwazo nchini, kiasi kwamba hiyo drone unaweza iuza kwa hasara ununue kamera ya kawaida upige picha za vibarazani. Nchi hii drone tu imekua kikwazo, na bado vitu vya teknolojia zaidi ya drone vinaendelea kuvumbuliwa.

Swali; Je, unadhani kuna uwezekano wa kijana mtaalamu wakitanzania kuhamasika na kufanikisha uvumbuzi kama huu? Jibu ni ndio inawezekana kwa nini isiwezekane, lakini jibu linaweza kua ni hapana haiwezekani kutokana na mfumo na mazingira tuliyokua nayo nchini kwetu. Naamini kabisa, wapo watanzania ambao kama wangeishi nje ya hapa, basi wangeweza kua wavumbuzi wakubwa na wenye mafanikio makubwa kutokana na kuthaminiwa kwa wavumbuzi na watumiaji wa teknolojia katika nchi zilizoendelea.

MFANO WA TATU:
Matumizi ya blogs na online channels kwa Tanzania ni madogo kiasi kwamba hayakufaa kulipiwa. Kwanini? Kwasababu mtu akihitajika kulipia kwanza leseni na michakato mengine ndio aweze kuendesha online Channel au blog basi watafungua wenye pesa. Vipi kuhusu wale wasio na pesa, wasiokua na ajira, wasio jiweza, na wanyonge? Hapa hawarambi kitu. Hii inamana ya kwamba, kufungua blogs na online channels kusiwe kwa malipo, ili wale ambao wanavipaji vya utangazaji, kufundisha, uigizaji na kadhalika watumie majukwaa hayo kusimamisha miradi yao, watakapo pata faida walipe kodi za biashara, na si kulipa kwanza bila kuingiza chochote.

MFANO WA NNE:
Gharama za internet ni kubwa mno kwa mtanzania wa kawaida. Huu ni ukweli mchungu, hizi gharama ni "mwana ukome", na kweli tumekoma. Kwa hali hii tutapata wapi akina Mark Zuckerberg? Si rahisi. Mbali na hayo, ukubwa wa gharama hizi inawafanya watanzania wengi kushindwa kusoma mtandaoni (online), hili ni pigo kubwa sana, kwani mambo mengi yaliyo muhimu yanafundishwa mtandaoni.

Vile vile, internet sasa inasonga kwenye 5G, lakini internet yetu nchini inasikitisha, na siasa ikiingia kati inazimwa.

MFANO WA TANO:
Hapa tutaangazia vitu vichache ambavyo vipo kwenye awamu ya nne ya Mapinduzi ya Viwanda lakini sisi hatuna.


(Picha: Mtandaoni. Hii ni hoverbike)


(Video: Mtandaoni. Hii ni 7D Hologram Technology)

03) MTAZAMO JUU YA NINI KIFANYIKE
Bishara; hapa tusiwe viongozi wa kusema tutaweka mazingira bora ya biashara, bali tuwe watendaji wa kweli katika kuweka mazingira ya biashara yawe kweli kwa ajili ya kurahisisha na kuinua biashara. Tuzingatie, masuala mazima ya kodi, miundombinu, siasa, sheria, teknolojia, na kadhalika.

Tudumishe amani katika nchi yetu, kila mmoja kwa nafasi yake.

Kuwe na utawala wa sheria. Asiwepo mtu wakukaa juu ya sheria iliyopo kukandamiza wengine. Hii itajenga imani, umoja na mshikamano katika kutatua changamoto zilizopo.

Sera za nchi za kuchochea maendeleo ziendane na matamko ya viongozi, na pia ziendane na sheria zinazotungwa. Isiwe sera na maneno matamu ya kisiasa yanasema hivi lakini matamko na sheria baada ya vyeo yanasema vyengine.

Uwajibikaji. Tusiwe na mfumo wa viongozi wa nchi kutengeza matatizo, kisha kuyatafutia ufumbuzi ili kuonekana mashujaa. Bali tuwajibike na kuwa mashujaa wa kweli kwa kutafuta ufumbuzi wa matatizo yaliyopo bila kutengeneza matatizo mengine.

Tuendeleze kilimo huku tukichochea matumizi ya njia bora za kisasa katika hilo. Kwani kuna faida nyingi zilizowazi katika kilimo.

HITIMISHO
Uzi huu umeandaliwa na mimi The Festival. Naomba usisahau kuupigia KURA, ahsante.
 
Marejeo (References)

Adam Zeidan. (2021, July 21). Industrial Revolution. Industrial Revolution | Definition, History, Dates, Summary, & Facts

EATV. (2016, Aug 08). Utegemezi wa jembe la mkono TZ wapungua kwa 58%. Utegemezi wa jembe la mkono TZ wapungua kwa 58% | East Africa Television

IPP Media. (2019, Dec 27). Kampeni hizi zinaweza 'kufuta' jembe la mkono. https://go.shr.lc/2UZXWyG

Jamiiforums. (2020, Dec 2022).

Karger, D., & De Guzman, D. (1977). Factors Affecting Industrialization of Underdeveloped Countries. <i>Management International Review,</i> <i>17</i>(2), 73-85. Retrieved August 29, 2021, from Factors Affecting Industrialization of Underdeveloped Countries on JSTOR

Samouel and Aram. (2016). Determinants Of Industrialization: Empirical Evidence For Africa. https://www.google.com/url?sa=t&sou...Vaw1FOAdKQS68-eJo1kF4MthX&cshid=1630228141157
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom