G Sam
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 11,555
- 35,880
Wapo watu wanaojitahidi kupigapiga kelele kuhusu ujenzi unaoendelea wa Chato International Airport (CIA). Watu hawa wanapigia tu kelele mvunguni mwa kitanda lakini ujenzi utaendelea na utakamilika huku kukiwa hakuna hata mtu atakayefanikiwa kuufikisha mbali mjadala huu.
Kwenye ujenzi wa flats za UDSM hapo watu walidanganywa kiasi cha fedha na sisi viherehere tuliojaribu kufika karibu ili tu tuujue ukweli nusura tungeonyeshwa cha mtemakuni.Tuliamua kuufyata fyatuu.
Kwenye ujenzi wa CIA kwanza kuna usiri mkubwa na hata vyombo vya habari ni marufuku kuufuatilia ujenzi huu. Kwenye kazi zinazoendelea pale kila kitu ni sirisiri tu! Hakuna kuhojihoji na mbaya zaidi kama huusiki basi ni marufuku kusogea karibu.
Huu utawala tulio nao sasa ni wa ajabu sana. Kwanza kwenye system wamebanwa na mtu mmoja na huyo akisema kimyaaa basi kunakuwa kimya kweli! Jamaa ana sura ya mbuzi usipime.Mkono wake ni chuma haswaa. Hivi hatujajifunza kwa Tundu Lissu? Ben Saanane? Watu wanafanyiwa unyama kiasi hicho na bado hakuna kuhoji! Hata spika siku akijifanya kiherehere kuandaa matume basi ajiandae kukosa hata mishahara ya kuwalipa wabunge! Jamaa anaweza akafanya hivyo na mambo yakaenda kama vile hakuna lililotokea.
Ukweli ni huo kuwa tuko kwenye system ya "one dimension"inayoendeshwa na mtu mmoja kwenye kila nyanja, ukihoji lolote kuhusu chochote ulicho na mashaka nacho basi unaruhusiwa kuhoji mara moja tu na usirudie tena. Na kwa staili anayoenda nayo basi tujiandae baadaye nchi kukabidhiwa mtu wa aina yake na wake ili asifukue haya makaburi mazitomazito yanayojengwa sasa. Tumeshaamua wenyewe kuingia humo! Nawahakikishia kuwa hatutatoka tena humo labda kwa kitambo kirefu na lazima patokee purukushani.