Ndugu zangu amani iwe nanyi, nimesikitishwa na ushabiki wa kitoto ktk swala kubwa la wizi wa rasilimali zetu hasa madini, samaki ktkt bahari kuu na mazao ya misitu. nilisha andika sana hapa hasa mwaka jana na leo narudia; ccm ndio mkoloni mweusi wa nchi hii kwa kuwa ametutawala tangu uhuru. mikataba yote ya kujinga inayomnyonya mtanzania, ilisainiwa na kupitishwa kwa kejeli bungeni na hawahawa ccm wakiongozwa na huyu Ndungai Job alipokuwa naibu spika. leo wamesahau yote eti nao wanamwonea huruma mtanzania, huu ni unafiki wa kiwango cha juu mno. kikubwa ilipaswa ccm wawaombe radhi watazania kwa udhalimu wa kutanguliza matumbo yao badala ya utaifa. kinachotokea leo ni aibu kwa ccm na taifa kwa ujumla,nawasihi ccm acheni kucheza na akili zetu nyinyi ni sawa na chaka la wezi; maana kula wizi mkubwa nchi hii umeasisiwa na kuratibiwa na ccm. kila mwenye macho haambiwi tazama, bali muda utaongea. mungu waumbue wanafiki hawa.