Huo ndio ukweli. CCM ilikwisha kwanga muda mrefu sasa, hilo wanachama wake wote na viongozi wao wanalijuwa. Nani atabisha kwa hili ?
CCM ilimuandama kila aliyepinga maamuzi yao tokea kuja kwa vyama vingi. Haikujali mpinzani au mwanachama wake, wangapi walikutana na rungu la chama kwa kupinga mwelekeo wa CCM. Bunge lilitumia uwingi wa CCM kuiadhibu nchi kwa mikataba mibovu na leo ndio hivyo eti Rais na Mwenyekii wa CCM eti ana uchungu wa Madini? hawa watu Mungu anawaona.
Nani hajuwi kuwa Rais JPM anakimbizana na kivuli cha uchaguzi wa 2015 ? na sio uzalendo wa kweli.
Wazalendo hawabadiliki kama kinyonga wako tayari kuadhibiwa kwa kusimamia kile wanachokiamini kwa maslahi ya Tanzania. Uzalendo hauanzi kwa kuwa Rais tu,
Tungemshauri JPM ajitazame kwenye kioo akiwa amevaa suti tokea akiwa mbunge, waziri, mjumbe wa Cabineti na mshauri wa Rais kwa nafasio ya uwaziri jee anastahili kuitwa mzalendo walau kwa hii miaka mitano iliyopita?
Historia haimuweki kwenye kundi hilo isipokuwa kwenye kundi la mtafuta sifa na mkurupukaji wa kiwango cha CCM iliyochoka.
Makosa ya CCM leo yanamugharimu JPM. CCM ilidharau wazalendo wa kweli wa nchi hii, iliamua, ilitesa watanzania kwa mikataba na maamuzi mabovu ya serikali yao. Si bunge la CCM, Mahakama za wateuzi wa CCM wala wasomi wa CCM waliothubutu kupaza sauti, wote walinyamaza kimya.
Nasema tena Kivuli cha CCM kiko kwenye mikataba yote sio ya madini tu , kiko kwenye mabenki yetu, uchumi wetu, ajira zetu, Mahakama zetu, na kila penye ubovu hayo ndio matunda ya CCM. Kama wanavyotaka tuamini katika yale mazuri ya CCM ndivyo hivyo hivyo kwenye mabaya ni CCM tu.
CCM INATAFUTA MLANGO WA KUTOKEA.
Imechelewa, mlango si kuzuiya vyama kufanya siasa, kuwaziba wapinzani midomo bungeni na uraiani halafu ukatumia mwanya huo kufanya usanii wa kizalendo wa madini, mara madawa ya kulevya, mara mahakama ya mafisadi na ukataka usikike wewe tu eti huo ndio uzalendo wa CCM.
Kivuli cha 2015 kinamnyima usingizi Magufuli sasa anajaribu kupora ajenda katikati ya udikteta wa demokrasia. Hatafaulu na katu CCM haitafaulu.
Wenye macho tunakutazama ewe JPM na CCM yako lakini tambuweni mungu anawaona.
Milango yote imefungwa kwa huu wa madini tafuta mwengine na uwe na uzalendo wa kweli basi watanzania wote tutakuunga mkono lakini si haya maigizo.
CCM ijipime wapi ilikosea, JPM aangalie asije akakosea zaidi. Walau hili la Mikataba kidogo linajadilika.
Tumkumbushe JPM na CCM dawa ya yote haya ni KATIBA MPYA YA WANANCHI.
Maigizo mwiko.
Kishada.