Ukweli mchungu: CCM haijawahi kufuata Ilani yake wala katiba ya nchi kwa miaka 5

Subira the princess

JF-Expert Member
Mar 3, 2018
2,474
2,644
Wasalaam,

Naomba niweke wazi ukweli halisi bila ushabiki wa kisiasa chama chetu cha mapinduzi mwaka 2015 walikuja na ilani nzuri na ya kupendeza Wakati wa kampeni, baada ya kushinda uchaguzi bwana yule alitupilia mbali ilani ile na kifanya jinsi alivyoona yeye inafaa na jinsi alivyotaka yeye. (show ya MTU mmoja), na akasema bila haya kwamba yeye hashauriki.

Sote tunafahamu na tulishuhudia bwana yule akiapa kuilinda na kuitekeleza KATIBA yetu lakini ikawa kinyume chake tumeshudia akiinajisi katiba na kuongoza kwa matakwa yake, tumeshudia akilidharau bunge letu, mahakama zetu, na uhuru wetu, udhalilishaji wa watumishi wa umma na kiburi kilichopitiliza.

Kwa miaka mitano hii tumeshuhudia ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu kinyume na katiba, tumeshuhudia watu wakipigwa na kuumizwa, watu wakitekwa na kupotezwa (Azori na Ben saa 8), tumeshudia mbunge akipigwa risasi(Tundu Lissu) tumeshuhudia mauaji ya watu waliofungwa kwenye viroba na kutoswa mto ruvu na baharini kinyume na katiba, tumeshudia wote waliomkosoa wakisulubiwa wakiwemo waandishi wa habari na vyombo vya habari vikifungiwa kinyume na katiba.

Kwa miaka 5 hii tumeshudia matimizi mabaya ya fedha nchi ya bajeti iliopitishwa na bunge, tumeshuhudia mtu mmoja akitembea na mamimilioni ya fedha kwenye gari yake na kutumia atakavyo nje ya utaratibu na bila idhini ya bumge(ujenzi wa airport chato).

Hitimisho; huu ni mwaka wa uchaguzi MTU yule yule na CCM wale wale wamejitoa akili wanataka tena miaka,5 ya kuongoza watanzania, wanaomba tena waendelee kuibaka na kuinajisi katiba walioitunga wenyewe. Kila MTU atafakari je tuendelee kuwaamini ccm 2020_2025?

Yajayo yanasikitisha.

Maendeleo yana vyama
 
Back
Top Bottom