Ukweli madikteta wapo, wamekuwapo na wataendelea kuwapo, kama binadamu wengine.

Francis12

JF-Expert Member
Sep 30, 2016
7,533
22,278
Madikteta wapo, wamekuwapo na wataendelea kuwapo, kama binadamu wengine.
Wao hutokea, huishi kwa kukatisha maisha ya wengine au kuyahatarisha, kuyaharibu kwa sababu tu, hawataki kuwaona wakifanya kinyume na wanavyodhani ni sahihi.
Na wafuasi wao wapo, wa kuwasaidia, kuwashabikia, kuwatetea na kuwalinda.

Siku yao ikifika, nao huaga dunia, kuzikwa na kuoza. Kama wanadamu wengine.

Usimuogope dikteta. Hawezi kusimamisha muda usisogee! Hawezi kukausha maji ya mito ya dunia ili uhai ukome, hawezi kulishusha jua karibu na uso wa dunia ili viumbe vyote vichomeke na kuteketea. Hawezi.
Anachoweza ni kutesa na kuua, kufanya matendo ya watu wadogo wa kichwa, wasioweza kufikiri, wasioweza kushawishi, wasioweza kuishi kwa amani ya nafsi zao wenyewe.
Dikteta mmoja maarufu, kwa jina Joseph Stalin wa muungano wa kisoviet, aliwahi kusema usimuamini mtu yeyote hata wewe mwenyewe. Huyu ni mtu asiyemuamini hata mama yake mzazi, hata walinzi wake, mke wake na watoto wake. Ni mgonjwa wa akili.
Wasichokijua madikteta ni kanuni za asili, kwamba hakuna nguvu isokuwa na ukinzani.
Katika utawala wa kisiasa unaompa mtu nguvu ya madaraka ya kuongoza jamii za watu mbalimbali, wa makabila, dini na mila mbalimbali, ukinzani hauhepukiki. Na mtawala asiyejua kanuni rahisi kama hiyo huangukia kwenye udikteta. Kazi yake itakuwa kutisha, kukamata, kutesa, kuwaficha na kuua wanaochukizwa na matendo yao. Na matendo hayo hayawezi kukoma kwa sababu, kila kukicha ukinzani unaibuka na/au kuongezeka. Na kwa kuwa yeye hataki ukinzani, basi huendelea kutisha, kukamata, kutesa, kuficha na kuua watu asiowapenda. Kupambana na ukinzani ni kama kulazimisha puto lilojaa hewa kuzama chini ya maji, sharti utumie mabavu, kwa muda wote. Na hapo atabakiwa na mkono mmoja wa kufanya shughuri zake, wakati mkono mwingine utakuwa na kazi ya kulazimisha puto kubaki chini ya maji kwa muda wote.

Ujumbe huu si kwa dikteta awaye yote, bali ni kwa raia wema, wazalendo, majasiri. Ujumbe huu uwafikie vijana wa kitanzania walioanza kunusa harufu mbaya ya udikteta, walioonja ladha mbaya ya udikteta. Nawaambia hivi, dikteta hana rafiki, yeye haamini mtu yeyote, hata yeye mwenyewe. Anaweza kukutumia wewe kuwadhuru wengine, na atawatumia wengine kukudhuru wewe pale utakapojifanya unafikiri tofauti. Katika kumtumikia dikteta hakuna kufikiri, bali kuenda kama anavyotaka yeye. Unatakiwa kuupa ubongo wako likizo ya kudumu, kwa kuwa ukifikiria na yeye akafikiri, lazima siku moja mtatofautiana. Na kwa kuwa Dikteta haamini mtu, hajiamini hata mwenyewe, basi ukishatofautiana naye uko hatarini. Wewe unaweza kudhani kwamba mnaweza kujadili, na kwamba kutofautiana kimawazo ni jambo la asili na kuna njia salama za kupitia kuelekea kwenye maamuzi ya pamoja, lakini dikteta hawezi kuwa na akili hiyo. Akili yake tayari imeathiriwa na maradhi ya kisaikolojia yasiyotibika kirahisi.
 
Mkuu unajuwa kuweka mada vizuri nakupa like kubwa. WaTz tukatae elements zozote zitakazo ashiria u dictator wa aina yoyote, hii nchi tumepewa na Mungu tuiishi kwa Amani, furaha na upendo kwa kila moja wetu.
 
Pamoja sana mkuu
Mkuu unajuwa kuweka mada vizuri nakupa like kubwa. WaTz tukatae elements zozote zitakazo ashiria u dictator wa aina yoyote, hii nchi tumepewa na Mungu tuiishi kwa Amani, furaha na upendo kwa kila moja wetu.
 
Madikteta wapo, wamekuwapo na wataendelea kuwapo, kama binadamu wengine.
Wao hutokea, huishi kwa kukatisha maisha ya wengine au kuyahatarisha, kuyaharibu kwa sababu tu, hawataki kuwaona wakifanya kinyume na wanavyodhani ni sahihi.
Na wafuasi wao wapo, wa kuwasaidia, kuwashabikia, kuwatetea na kuwalinda.

Siku yao ikifika, nao huaga dunia, kuzikwa na kuoza. Kama wanadamu wengine.

Usimuogope dikteta. Hawezi kusimamisha muda usisogee! Hawezi kukausha maji ya mito ya dunia ili uhai ukome, hawezi kulishusha jua karibu na uso wa dunia ili viumbe vyote vichomeke na kuteketea. Hawezi.
Anachoweza ni kutesa na kuua, kufanya matendo ya watu wadogo wa kichwa, wasioweza kufikiri, wasioweza kushawishi, wasioweza kuishi kwa amani ya nafsi zao wenyewe.

Dikteta mmoja maarufu, kwa jina Joseph Stalin wa muungano wa kisoviet, aliwahi kusema usimuamini mtu yeyote hata wewe mwenyewe. Huyu ni mtu asiyemuamini hata mama yake mzazi, hata walinzi wake, mke wake na watoto wake. Ni mgonjwa wa akili.

Wasichokijua madikteta ni kanuni za asili, kwamba hakuna nguvu isokuwa na ukinzani.

Katika utawala wa kisiasa unaompa mtu nguvu ya madaraka ya kuongoza jamii za watu mbalimbali, wa makabila, dini na mila mbalimbali, ukinzani hauhepukiki. Na mtawala asiyejua kanuni rahisi kama hiyo huangukia kwenye udikteta. Kazi yake itakuwa kutisha, kukamata, kutesa, kuwaficha na kuua wanaochukizwa na matendo yao. Na matendo hayo hayawezi kukoma kwa sababu, kila kukicha ukinzani unaibuka na/au kuongezeka. Na kwa kuwa yeye hataki ukinzani, basi huendelea kutisha, kukamata, kutesa, kuficha na kuua watu asiowapenda.

Kupambana na ukinzani ni kama kulazimisha puto lilojaa hewa kuzama chini ya maji, sharti utumie mabavu, kwa muda wote. Na hapo atabakiwa na mkono mmoja wa kufanya shughuri zake, wakati mkono mwingine utakuwa na kazi ya kulazimisha puto kubaki chini ya maji kwa muda wote.

Ujumbe huu si kwa dikteta awaye yote, bali ni kwa raia wema, wazalendo, majasiri. Ujumbe huu uwafikie vijana wa kitanzania walioanza kunusa harufu mbaya ya udikteta, walioonja ladha mbaya ya udikteta.

Nawaambia hivi, dikteta hana rafiki, yeye haamini mtu yeyote, hata yeye mwenyewe. Anaweza kukutumia wewe kuwadhuru wengine, na atawatumia wengine kukudhuru wewe pale utakapojifanya unafikiri tofauti.

Katika kumtumikia dikteta hakuna kufikiri, bali kuenda kama anavyotaka yeye. Unatakiwa kuupa ubongo wako likizo ya kudumu, kwa kuwa ukifikiria na yeye akafikiri, lazima siku moja mtatofautiana. Na kwa kuwa Dikteta haamini mtu, hajiamini hata mwenyewe, basi ukishatofautiana naye uko hatarini. Wewe unaweza kudhani kwamba mnaweza kujadili, na kwamba kutofautiana kimawazo ni jambo la asili na kuna njia salama za kupitia kuelekea kwenye maamuzi ya pamoja, lakini dikteta hawezi kuwa na akili hiyo. Akili yake tayari imeathiriwa na maradhi ya kisaikolojia yasiyotibika kirahisi.

IMG_20170808_132358.jpg

Mr mkiki

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom