Ukweli lazima usemwe, aliyetufikisha hapa ni Nyerere

Watu huwa wanamsifia Nyerere kwa mengi. Ila kitu ambacho kinadefine legacy yake mpaka sasa ni hili janga la katiba alilotuachia.

Kiuhalisia hii katiba ilitengenezwa mahususi kwaajili ya Nyerere. Yeye ndo alitaka "a strong executive with necessary control of the legislature", alitaka katiba inayomfanya kuwa kama mfalme. Kipindi hicho Fundikira waziri wa katiba na sheria, aliona madhara ya hilo na akawa anasuggest rais asiwe na nguvu sana. More like a ceremonial president. Mfumo huu mara nyingi huwa unazuia utawala wa mabavu. Lakini in the end Nyerere akapata katiba anayoitaka.

Utawala wa Nyerere ulikuwa defined kama authoritarian, ambayo ni just a diplomatic way of saying a dictatorship.

Mtu mwenye maono asingethubutu kuacha hii katiba iendelee kutumika wakati anatoka madarakani.

Mwishowe katuachia dubwasha ambalo kupambana nalo itaishia kuwafanya watu watumie nguvu ili kurudisha usawa na haki katika jamii.
Siku akirudi mtatoka hapo mlipo.
 
Ili kutatua tatizo, lazima tufahamu chanzo chake. Lasivyo tutaishia kurudia yale yale.

Matukio ya wakati huo, yalikuwa hayaendani na hii katiba ya kimabavu. Mara nyingi na katika tafiti mbalimbali zinaonyesha hakukuwa na ulazima wa kuwa na katiba ya aina hii.

Ni porojo tu za kisiasa ndo zilitumika kuwaaminisha watu kuwa eti hali ya kisiasa ya wakati ule na uchanga wa nchi ndo zililazimisha kuwepo na hii katiba.
Hatuwezi kutatua tatizo kama muda mwingi tutaumia kuchanganua chanzo cha tatizo na kuwalaumu watu ambao tunadhani ndio chanzo cha tatizo
 
Back
Top Bottom