Ukweli kwanini binadamu na nchi kwa ujumla hatuwezi kufanikiwa wote!

stakehigh

JF-Expert Member
Aug 9, 2019
6,184
3,145
  • -Jana tarehe 7/4/2021, jarida la forbes lilitoa takwimu nzima ya matajiri katika dunia hii, japokua hua wanatoa kila mwaka lakini ya jana ilikua ngumu kumeza. Watu wengi hua wanapenda kujua tu nani anaongoza then baada ya hapo amemaliza yote anayojua kuhusu utajiri unaochapishwa na forbes.

  • Kuna sababu nyingi sana kwanini nasema ripoti ya jana ni ngumu kumeza na huenda ikawa ndo mwanzo wa kiama cha watu wengi kudumbukia kwenye dumbwi kubwa la umaskini kuanzia mwaka 2030 lakini ili kuelewa haya yote inabidi uelewe jinsi uchumi wa dunia unavyofanya kazi na influence yake katika dunia nzima, (money), (currency), (inflation), (economic burbles), (fiat money).
Mpaka sasa tulipofikia ni wazi kwamba bado nchi nyingi duniani hazijapata uhuru kamili, uhuru tuliopata ni wa kuzurura ndan ya mipaka ya nchi bila kuulizwa chochote lakini karibia upande mwingine mwingi wa maisha bado hatupo na uhuru unaotakiwa. Mpaka nnavoongea sasahv tajiri wa kwanza duniani anaitwa Jeff bezoes akiwa na utajiri wa ($177B), GDP ya Tanzania ni ~($70B), Kenya inaongoza ukanda huu ikiwa na ~($101B). Kwa maneno marahisi Jeff Bezoes ni tajiri kuliko Kenya na tanzania zikiungana mwaka mzima

Dunia nzima kuna jumla ya ($37 trillion), lakini pia jumla ya matajiri wote wana kiasi cha ~$11 trillion, kwa haraka haraka ni kwamba pesa inaobaki kwa ajili ya sisi wengine ni ($26 trillion) ambayo bado ni pesa inayotafutwa na hao hao matajiri wakubwa wa duniani, ukiangalia izi takwimu ni wazi kwamba hizo pesa bado ztaishia kwa hao hao matajiri, kwa wale mnaofuatilia trend za forbes utagundua kwamba utajiri wa mabilionea wa dunia haupungui bali unaongezeka kila mwaka, tukimchukua jeff bezoes kama mfano utaona utajiri wake umekua mara dufu yeye pamoja na matajiri wenzake toka mwaka 2000


  • Sababu kubwa ya kukua kwa utajiri wao ni kwa sababu ya uchumi shirikishi dunia nzima, ukiongelea $177B inamaanisha unaongelea pesa ambazo ni jumuishi dunia nzima, ndan ya hio $177B kuna tsh,ksh na pesa za nchi zingine zote, kwa yoyote ambaye ameshawahi kununua chochote amazon akiwa Tanzania basi aliuza nchi yake ili Jeff bezoes (MMILIKI NA MWANZILISHI) apewe dola in return, Tuseme umenunua kitabu ama nyimbo amazon kwa visa, then visa wataangalia kwenye akaunti yako kama kuna kiasi cha kutosha, kama kuna kiasi cha kutosha basi itatuma request kwenye benki yako wakukate icho kiasi, then benki itabaki na hicho kiasi ila itakua imetengeneza negative asset or some people call it (IOU) kwa maneno marahisi ni kuwaambia BOT kwamba kuna mtu kalipia kitu kwa kutumia tsh, kwahio iandike kama deni then tutatumia pesa zetu uku nchini kumpa mmiliki wa amazon, kwahio inakua umeuza nchi yako katika deni ilihali tsh uliokua nayo kwenye account inabaki kwenye mzunguko

  • Uchumi wa dunia unaongozwa kwa utapeli wa dola ya marekani kasoro nchi za china, Russia, afganistan and cuba. Kwanini nasema utapeli? ni kwa sababu maamuzi yote ya tsh hayatoki serkali bali yanatoka katika mmiliki wa dola ambae ni (Federal reserve), leo hii dola ikiyumba then automatically tsh nayo lazima iyumbe, hii ni kwa sababu ya (fiant currency), kwa lugha rahisi ni kwamba tsh ipo kwenye mzunguko kwa sababu ya uwepo wa dola incase dola ikiondoka kwenye mzunguko basi tsh ndo inakua mwisho wake, huu ni utapeli na umeenda mbali kiasi kwamba hata mapato ya ndan yakiwa hayatoshi basi tunatuma maombi ya mkopo marekani ili watupe tsh ambayo ni hela halali ya Tanzania lakini inafanyiwa maamuzi nje ya Tanzania.

  • Incase serikali ya marekani ikiwa inahitaji pesa Zaidi hua wanakopa kama kigezo cha usawa lakini wanaweza kulipa madeni yao kwa kuchapisha pesa mpya zingine kwa ajili ya kulipia mikopo tu bila kupewa kibali kwingine kokote, so kwa lugha nyingi utegemezi wetu kichumi katika nchi zilizoendelea sio katika misaada bali katika unyonyaji wa uhuru wa kujipatia utajiri ambao unatokana na sadaka za watu wengine kua maskini, ukitengeneza billionea mpya basi unategengeneza maskini wengine ~25.

  • ITAENDELEA…
 
Jef bezo na wengineo hawaizidi Tanzania utajiri.Tuviwanda twake na mali zote haziwezi kufikia thamani ya Tanzanite pale Arusha tu acha almasi na dhahabu.
Kwa nini utajili wa Tanzania uusabie sabie katika GDP wakati kuna mali zipo zimetulia tu mfano samaki wa baharini,ziwani, mifugo,miti,wanyama pori, gesi,ardhi nk. Ambavyo ukiamua kuvinadi hizo hela za Jef si chochote.
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom