Ukweli kuhusu wafanyakazi waliositishiwa mikataba ya kazi na FINCA Tanzania MFC Ltd

MNYOO JOGOO

Senior Member
Apr 2, 2012
195
94
MWANANCHI FINCA.jpg

Sisi ni wafanyakazi kumi na tatu ambao majina na picha zetu zimetolewa na uongozi wa kampuni ya Finca kwenye Gazeti la Mwananchi la tarehe 13/06/2013 ukurasa wa 27 toleo namba 4736 na tarehe 15/6/2013 ukurasa wa 32, tuliokuwa tumeajiriwa na FINCA TANZANIA M.F.C LTD katika tawi la Iringa. Tunapenda kuwaeleza watanzania wenzetu ukweli juu ya mambo tuliyotendewa na utawala wa kampuni baada ya kuandika barua ya kuhitaji kuongea na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo.
Mnamo tarehe 16/05/2013 tulimtumia mkurugenzi barua ya wito wa wafanyakazi kuhitaji kuzungumza naye kwa nia njema. Tulikuwa tunamhitaji ili tuweze kuwasilisha matatizo yaliyokuwa yanatukabili sisi na kampuni kwa ujumla wake, baada ya hatua za kawaida ndani ya tawi na kanda kutokuzaa matunda. Baadhi ya matatizo/madai hayo ni haya hapa:
  1. Mazingira magumu ya kazi ambayo yamekuwa yakisababishwa na uongozi wa tawi uliopo hasa meneja wa tawi na msimamizi wa mikopo binafsi. Katika hili wafanyakazi tulikuwa tunakumbana na matatizo ambayo tuliyavumilia kwa muda lakini baada ya kuumia kwa muda mrefu tulimuandikia barua Mkurugenzi Mtendaji wa Finca kumueleza.
  2. Wafanyakazi kucheleweshwa kuthibitishwa kazini "late confirmation of employment" bila kupewa sababu za msingi na bila fidia yoyote kwa miezi iliyocheleweshwa.
  3. Kucheleweshwa kwa mikopo ya wafanyakazi kwa miezi mingi kiasi cha kutisha bila kupewa sababu zenye mashiko
  4. Wafanyakazi kuwajibika kutoa majibu katika makosa ambayo hatukuyatenda kwa mfano: Afisa analazimika kuwaambia wateja walipe akiba mara mbili bila sababu za msingi ukizingatia wateja husika walikwisha lipa kwa usahihi na wakasaini
  5. Kamati ya maadili kuendeshwa kibabe bila kufuata utaratibu
  6. Wafanyakazi kuingia gharama binafsi kufanya kazi za kampuni bila fidia yoyote
Haya ni baadhi ya mambo tuliyoyaanisha katika barua tuliyoituma kwa Mkurugenzi Mtendaji kwa lengo la kuzungumza nae na kujadili namna ya kuyatatua baada ya kutumia ngazi za chini kwa muda mrefu bila mafanikio. Katika kushughulikia masuala haya, Uongozi wa Finca Tanzania MFC Ltd ulifanya kama ifuatavyo:
1. TAREHE 16/05/2013 KILA MMOJA ALITAKIWA KUTOA MAELEZO;
Mara baada ya kurejea kutoka katika shughuli zetu za kiofisi siku hiyo ambayo pia barua tajwa ilitumwa, Meneja wa tawi alitutaka kila mmoja kuandika maelezo ya kazi ambazo alizifanya siku hiyo kinyume na utaratibu wa kila siku, ambapo tulimuandikia na nakala zake tunazo.
2. MAJIBU YA MKURUGENZI MTENDAJI TAREHE 17/05/2013
Baada ya kutuma barua kwa Mkurugenzi mtendaji aliipata na kutujibu kwa vitisho. Alidai kuwa atafanya uchunguzi kupitia Polisi kitengo cha uhalifu wa mtandao (Police Cyber criminals Section) ili kubaini aliyehusika kutuma ujumbe huo kwenye anuani yake ya barua pepe lakini pia alitusihi tuendelee na kazi na tulifanya hivyo. Kimsingi majibu husika yalikuwa na mtazamo hasi ukilinganisha na maudhui ya barua tajwa. Baada ya majibu hayo ndipo hatua nyingine za kukatisha tamaa ziliendelea dhidi yetu.
3. TAREHE 20/05/2013 KILA MMOJA ALITAKIWA KUTOA MAELEZO.

Baada ya majibu ya Mkurugenzi mtendaji kupitia barua pepe, tulipewa barua nyingine kutoka Idara ya rasilimali watu ya kampuni kututaka tuandike maelezo ya namna kila mmoja alivyohusika katika kuandika na kutuma barua kwa Mkurugenzi mtendaji. Barua hiyo pia ilitutuhumu kuwa hatukufanya kazi siku hiyo ya tarehe 20/05/2013 na kututaka tueleze kwanini hatukufanya kazi siku hiyo, jambo ambalo ni kinyume na uhalisia kwa sababu kila mmoja wetu alifanya kazi siku hiyo lakini alitakiwa ajieleze kwanini hakufanya kazi.
4. TAREHE 22/05/2013 KILA MMOJA WETU ALIPATIWA BARUA YA KUITWA KWENYE KIKAO CHA KAMATI YA NIDHAMU KUJIBU TUHUMA ZA KUTUNGWA DHIDI YETU
Ilipofika tarehe 22/05/2013 kila mmoja wetu alipatiwa barua ya kuitwa kwenye kikao cha kamati ya nidhamu kwa ajili ya kujibu tuhuma zilizoorodheshwa. Tuhuma tajwa ni pamoja na : kutuhumiwa kufanya kikao batili (unauthorized meeting) tarehe 16/05/2013 na kutoa hatamu (ultimatum) kwa Mkurugenzi Mtendaji kukutana na sisi, kushawishi wafanyakazi kugoma, kutotii amri halali ya menejimenti ya kuandika maelezo, na pia kutenda mambo yanayodhalilisha menejimenti ya kampuni. Kimsingi hizi tuhuma zilizushwa na kutungwa kwa lengo la kutukomoa eti kwa kile tulichokifanya " kumtumia mkurugenzi barua". Katika hili mahojiano yalifanyika kati yetu na kamati ya nidhamu, na kila mmoja alihojiwa kwa wakati wake kuanzia tarehe 27/05/2013 hadi tarehe 30/05/2013. Na ndipo kamati ikatoa pendekezo lake kwa mkurugenzi.
5. MATOKEO YA KIKAO CHA KAMATI YA NIDHAMU

Mnamo tarehe 31/05/2013 tulipatiwa matokeo ya kikao cha kamati ya nidhamu ambayo pamoja na kudai kwamba wana uhakika sote tunamakosa ya moja kwa moja katika tuhuma zote tajwa na zaidi ya yote pasipokuwa na ushahidi wa kutosha, kamati ilipendekeza kwa Mkurugenzi mtendaji wa Finca Tanzania kusitisha ajira ya kila mmoja wetu na tukapewa muda wa siku tano za kukata rufaa dhidi ya pendekezo hilo la kamati endapo tunaona ni muhimu kufanya hivyo. Muda huo wa kukata rufaa ulikuwa unaisha tarehe 06/06/2013 kwa maana ya siku tano za kazi. Zaidi ya hili, kamati hii ilitudhalilisha kwa kututenga katika chumba maalumu ambacho kuanzia tarehe 27/05/2013 hadi tarehe 11/06/2013 tulikuwa tunalazimika kukaa humo kuanzia asubuhi hadi jioni pasipo kufanya kazi ya aina yoyote wala kushiriki mambo yoyote ya ofisi na wakati huo pia akaunti zetu katika kompyuta za ofisi zilifungwa. Na kuanzia tarehe hiyo 27/05/2013 kampuni ilileta wafanyakazi mbadala kufanya kazi zetu wakati sisi tukiwa tunaendelea kuhudhuria katika chumba hicho maalumu.
6. RUFAA
Tarehe 04/06/2013 sote tulikusanya rufaa zetu kwa Mkurugenzi na kumueleza kutokuuhusika kwetu na tuhuma tajwa zilizopikwa kwa lengo la kutukomoa. Ambapo tarehe 11/06/2013 alitoa uamuzi. 7. UAMUZI WA MKURUGENZI MTENDAJI Mnamo tarehe 11/06/2013 Mkurugenzi Mtendaji aliamua kusitisha ajira zetu sote bila kusikiliza rufaa zetu kwa kile alichoeleza kuwa anakubaliana na kamati ya nidhamu kwamba sote tumekutwa na makosa katika tuhuma zote zilizoelekezwa dhidi yetu.
8. ZINGATIO
Tunaomba izingatiwe kwamba kumuandikia barua Mkurugenzi Mtendaji kwa nia njema ili tumueleze matatizo tajwa na tuweze kujadiliana nae namna ya kuyatatua kwa lengo la kuboresha mazingira ya kazi na mwenendo wa kampuni kwa ujumla ndio iliyopelekea haya yote. Matokeo yake alitupuuza kwani kimsingi hapakuwahi kuwa na kikao chochote baina yetu wafanyakazi dhidi ya mwajiri wala hapakuwahi kutokea mgomo wa aina yoyote katika Finca tawi la Iringa. Lakini baada ya barua tajwa kutumwa mnamo tarehe 16/05/2013 ndio kilikuwa chanzo cha kuzuka kwa tuhuma tajwa na mambo mengine hata kufikia hatua ya Mkurugenzi Mtendaji kusitisha ajira zetu bila kutusikiliza. Na katika hali kama hii, tunatoa rai kwa waajiri kutumia njia mbalimbali kutatua matatizo pasipo kuyakimbia ili kuweza kuboresha mazingira kwa wafanyakazi na ufanisi katika kutoa huduma na sio kama njia hii iliyotumiwa na Finca ya kusitisha ajira ya watu kumi na tatu kwa mpigo kwa kisa cha barua ya wito kwa Mkurugenzi Mtendaji.
9. UAMUZI WETU
Kwa pamoja tumeamua kwamba tutaiburuza Finca Tanzania katika Tume ya usuluhishi na uamuzi (CMA) Mkoa na ikishindikana tutapeleka rufaa zetu kwenye Mahakama kuu Tanzania kitengo cha kazi ili Mahakama ikatende haki dhidi ya maamuzi haya ya Mkurugenzi Mtendaji wa Finca dhidi yetu.
Wenu katika ujenzi wa taifa Tuliokuwa wafanyakazi wa finca tawi la Iringa.
 
serikali yetu ni Dhaifu, private company wanatumia mwanya huo kuwadhurumu wafanyakazi. Kumtumia mkurugenzi email au barua ya wito wa kuzungumza naye, siyo kosa ,sasa itakuwaje asitishe ajira za watu wanaoitakia mema Finca. Watu wanataka kutoa mawazo yao kwa ajiri ya kuboresha kampuni harafu wewe unafukuza. Nina wasiwasi na Cv ya mkurugenzi huyu. Finca itaendelea kuwa chini siku zote kutokana na tabia ya aina hii. you should accept challanges ,kila mfanyakazi ana ubongo wake ,zifanyie kazi challenge kuikuza kampuni.
 
Kipindi mnaendelea kupokea salary mlikaa kimya..leo kibarua kimeota mbawa ndo mnaleta matatizo yenu jf sasa si tufanyeje..Komaeni na kitaa
 
sema wafanyakazi wengine wa hizi macrofinance hujihusisha wa wizi au mteja akishachukua mkopo ni lazima nao wapewe cha juu!

Au credid officer anajifanya ndiye mkopaji kama mteja kumbe uwongo!

Huenda kuna mengine uongozi umeyaficha!

Hili ni soko huria sii Ujamaa wakati wa Nyerere!

Huu ni mtazamo mwingine tu!

Songeni mbele kutafuta haki!
 
Kipindi mnaendelea kupokea salary mlikaa kimya..leo kibarua kimeota mbawa ndo mnaleta matatizo yenu jf sasa si tufanyeje..Komaeni na kitaa

lakini yeye kwa jinsi nilivyomuelewa si kwamba anataka umshauri. Kwa sababu ameshasema hatua waliyofikia ya kwenda vyo0mbo vya juu zaidi kisheria. Sasa suala la kupokea salary sidhani kama lina uhusiano hapa katika mada yake.

Na pia ameamua kuliweka wazi kwa sababu katika gazeti FINCA hawakusema ni sababu zipi zilizofikia hapo, kwani huenda baadhi yetu wametuhudumia upande wa mikopo hivyuo tunaweza kuwafikiria kuwa wameiba ndio maana wamafukuzwa.

WAKUU PAMBANENI TU hAKI ITAPATIKANA.

Kuna taarifa nilizisikia kuwa FINCA ni kampuni ya vigogo serikalini, na ndio maana wana kuwa na jeuri sana.


MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
Kama swala linakuzidi umri unakaa kimya, huo ndiyo uungwana kijana. Au unaenda FB kucheki status za kuchekesha.

Cyberteo; uungwana ni kitu adimu kukipata kwa watu wenye uwezo wa kawaidi. Kama hajaathirika yeye basi atkuja athirika hata rafiki yake au ndg yake kwan waajili wengi hii imekuwa kasumba
 
lakini yeye kwa jinsi nilivyomuelewa si kwamba anataka umshauri. Kwa sababu ameshasema hatua waliyofikia ya kwenda vyo0mbo vya juu zaidi kisheria. Sasa suala la kupokea salary sidhani kama lina uhusiano hapa katika mada yake.

Na pia ameamua kuliweka wazi kwa sababu katika gazeti FINCA hawakusema ni sababu zipi zilizofikia hapo, kwani huenda baadhi yetu wametuhudumia upande wa mikopo hivyuo tunaweza kuwafikiria kuwa wameiba ndio maana wamafukuzwa.

WAKUU PAMBANENI TU hAKI ITAPATIKANA.

Kuna taarifa nilizisikia kuwa FINCA ni kampuni ya vigogo serikalini, na ndio maana wana kuwa na jeuri sana.


MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!

You might be telling the truth, coz jamaa wana jeuri iliyopitiliza hata kuweza wazimisha waandishi wa habari waliokuja kuwahoji hao vjana.
 
Poleni sana huo ni utawala gani usiokubali changamoto kama hizo tena ni kwa manufaa ya ofisi ipige hatua mbona Finca wanakuwa kama yale majamaa yanayovaa nguo za kijani....Poleni sana ndugu zangu
 
Poleni sana kwa kukumbwa na mkasa wa kufukuzwa kazi. Pambaneni mpaka kieleweke maana kila anayetoka finca hana hamu ya kurudi, SIJUI KUNA NINI HUKO. Hebu mlioko Finca tujulisheni jamani ili tuwe aware na Finca Tanzania.
 
Back
Top Bottom