jokaKuu,..kuna makundi mengi sana ambayo yalishiriki ktk harakati za uchaguzi ambayo yanaweza kutoa malalamiko kama haya anayoyatoa Mohamed Saidi.
..mfano mmoja wa makundi hayo ni VYAMA VYA USHIRIKA. vyama hivyo vilikuwa mstari wa mbele ktk harakati za uhuru, lakini Mwalimu alikuja kuvivunja na kuunda mamlaka za mazao.
..kwa mtizamo wangu Mohamed Saidi anaelezea mchango wa wananchi wa mikoa ya Pwani, haswa dsm, ktk harakati za uhuru. personally nimesoma makala zake nikachukua yale ya msingi na kupuuza yale yasikuwa ya msingi.
..waandishi toka maeneo mengine ya Tanzania/Tanganyika hawazuiwi kuandika vitabu na makala kuelezea michango ya wazee wao ktk harakati za kugombea uhuru. kitu kibaya wanachoweza kufanya ni kupuuza michango ya ndugu zao wa maeneo mengine ya nchi yetu.
..waumini wa madhehebu mbalimbali nao wana ruksa ya kuandika ushiriki wa madhehebu yao ktk harakati za uhuru. kwa mfano, nilisoma makala za Padri mmoja mkatoliki akielezea urafiki wake na Mwalimu, na jinsi wamisionari wakatoliki walivyokuwa wakimfadhili wakati wa harakati za kugombea uhuru. makala hizo zilitoka kwenye blog ya Issa Michuzi.
..vilevile kuna Wahindi,Wazungu, etc etc walioshiriki harakati zile. hawa nao wanapaswa kuandika kuhusu mchango wao. why not? tena hawa wanaweza kuwa na malalamiko makubwa-makubwa kwasababu Mwalimu alikuja kutaifisha mali zao.
..tumchukulie Mohamed Saidi kwamba ameandika kitabu chake kutokana na elimu na uelewa wake. tatizo ni kwamba in recent yrs ni yeye peke yake aliyejishughulisha kutafiti na kuandika historia yetu. wangekuwepo waandishi wengine nina hakika wananchi tungeweza kupata picha nzima ya nini kilitokea ktk harakati za kutafuta uhuru.
Umesema jambo la maana sana. Watanzania tuache uvivu wa kusoma vitabu na tujitume kuandika vitabu. Wakati Mwalimu anaingia mamlakani kulikuwa na ombwe la elimu, usomi, utafiti, kila kitu. Lakini inaonekana kuna wanaomlaumu Mwalimu eti alijaribu kupotosha historia ya uhuru wa Tanganyika. Hapana. Huyu huyu Mwalimu tulimtegemea atuundie serikali, atujengee shule, hospitali, na pia atuandikie historia yetu? Saa ngapi? Ni kweli historia ya kwanza ya harakati za Tanganyika iliandikwa na wazungu. Lakini sasa tumesoma, utafiti tunauweza, sources zipo, tujitahidi tuandike na kujazia au kusahihisha pale Mohammed Said alipokosea. Utafiti hauna kikomo na historia si moribund. Juzi nimeshangaa kusoma mahali jinsi mabaharia wa Massachussetts walivyomsaidia Jemadari Washington. Historia hii haifundishwi shuleni hapa Marekani, lakini ukifanya utafiti kidogo utaipata.