Lole Gwakisa
JF-Expert Member
- Nov 5, 2008
- 4,728
- 2,259
Mwanafalsafa1,
Nimemsoma sana Mohammed Said kuhusu uasis wa TANU na juhudi za uhuru wa Tanzania ziliasisiwa na Waislamu. Kwa mujibu wake, Nyerere alipochukua madaraka aliwasahau na kuwatekeleza Waislamu waliomkaribisha Dar-es- Salaam na kwenye TANU. Anakubali kuwa Waislamu walikuwa nyuma kielimu kwa sababu ya sera za ukoloni, lakini hakiri kuwa Nyerere alijaribu kurekebisha kasoro hizo. Jinsi ninavyomsoma nadhani theme yake ni kwamba kwa sababu Waislamu "walianzisha" harakati za uhuru, walistahili kuwa na bigger share of the national cake kuliko ilivyo hivi sasa, na wakristo wamechukua nafasi zote za juu nchini wakati kulikuwa na hujuma za makusudi kuzuia Waislamu wasiendelee kielimu. i.e kufutwa kwa EAWMS mna Jamat Islamiya. So this is a call to Moslems to bring about a true liberation.
Jasusi, mkuu, I always bow to your logical arguments and contents.
Lakini kwa hili la huyu Mohammed Said, presentation yake its pure Pumba through and through.
Kwanza kabisa ukoloni haukusababisha waislamu wasisome, kutosoma ni kutokana na waislamu wenyewe.
Wakoloni waliingia nchini with their own vested interests.
Na ndio maana sehemu nyingi tu nchini ambako wakoloni hawakuweka makao maendeleo ya kielimu hata leo ni duni sana.
Kumsingizia Mwalimu kuwa aliwakandamiza waislamu ni kukosa kuelewa ukweli kwa hali ya juu, Mwalimu alilaumiwa sana tena sana kwa kutaifisha shule za Missionari na kuruhusu WATU WA DINI ZOTE kusoma katika shule hizo.
Na shule hizi za Mission zilizotaifihwa si za dini moja hata zile za wahindi eg Aga Khan (Tambaza) vile vile zilichukuliwa kwa ajili ya watu wote.
Pili, si waislamu walioanzisha harakati za ukombozi.
Leo hii kule Kilwa JK amezindua sanamu ya kuwaenzi babu zetu kwa vita ya ukombozi ya Maji Maji,miaka ya 1905.Waafrika wote mashariki ya Tanganyika walishiriki.
Mifano niliyotoa awali ya kina Mkwawa, Isike ,Meli na Kimweri ni mifano tosha.
Hawa walikuwa wanatetea ustaarabu wa mwafrika.
Tatu mimi nashangaa sana kwa watu hawa kama Mohammed Said kwa kukaribisha sumu ya ubaguzi wa kidini na kuihubiri sumu hiyo.
Meya wa kwanza hapa jijini Dar, Sheikh Amri Abeid aliheshimika sana baada ya uhuru na alichaguliwa kuwa Meya wa Dar es salaam.
Alipofariki mwaka 1964 alipewa heshima isiyo ya kawaida.Kwenye mazishi alikuwepo Jomo Kenyatta,Milton Obote na viongozi wengi tu wa Tanganyika.
Na mimi nilikuwepo, ingawaje nilikuwa kijana mdogo.Mizinga ilipigwa pale kwa heshima yake.
Meya huyo wa Dar.
Hii ndio heshima aliyopewa kiongozi Sheikh Amri Abeid na haikutazamwa kwamba alikuwa muislamu au la , ila kiongozi wa Tanganyika.
Leo kwa heshima yake jina la kiwanja cha Arusha kimepewa jina lake.
Sasa mtu anapo pandikiza udini leo ni kama anaikana heshima ya muafrika ili kuendeleza udini mabao hatukua nao.
Dhana ya "kujiliberate" kama mkuu Jasusi unavyoiweka inakosa mantiki pale ambapo unatanguliza fikra ya kuonewa.
Kimsingi kufuta ujinga ilikuwa kilio cha serikali ya awamu ya kwanza baada ya uhuru.
Kilio hiki kiliitikiwa na sehemu chache sana zilizopata mwanga wa umuhimu wa elimu. Leo miaka karibu 50 baada ya uhuru kwa wengine bado ni kilio kile kile.
Ndugu zagu waislamu na waTanzania wenzangu, lazima tuwekeze katika elimu ya watoto wetu. Na hakuna mchawi wa matatizo ya kukosa elimu kwa sehemu nyingi za mikoa ya pwani na zingine nyingi tu mikoani ila kuheshimu kuwekeza katika elimu ya watoto wetu.