Ukweli kuhusu vipimo vya HIV/AIDS

Tiger

JF-Expert Member
Nov 30, 2007
1,747
386
Mimi si mtaalamu wa maswala ya tiba, ila kwa ufahamu wangu nafikiri zipo njia mbali mbali za kupima kama mtu ana maambukizo ya HIV.

Njia ambayo nafikiri tunaitumia sana ni ile ya kupima chemical inayotolewa na WBC kama watahisi kuna virus wamo mwilini, na ya pili ni ile ya kupima virus wenyewe kama wamo kwenye damu.

Swali langu ni je, kwa ile njia ya kupima chemical, kuna uwezekano wa mtu mwenye maambukizi kupima na akaonekana yuko negative?(chukulia mtu huyo kaishi mwaka m1 hajafanya ngono na hana dalili ya kuugua ugonjwa wowote)?

Tafadhali naomba msaada wenu.
 
Acha kujipa moyo,we kapime na matokeo uyakubali.

Asate, lakini ikiwa ni mimi au mtu yeyeto, swala nikwamba muhusika amepimwa zaidi ya mara 1 na ameonekana negative ndio maana swali hili likaulizwa.
 
katika hali ya kawaida (test hazija expire, zimetumiwa inavopaswa) mtu akipima na kuonekana negative (kama ana mwaka haja ji "expose" kwa njia ya ngono, transfusion au njia zingine) basi chances are high hana UKIMWI.

Ila kwa yule anae onekana positive, kuna uwezekano awe negative kwa sababu mbali mbali, hivo anahitaji kupima tena kwa kubadilisha aina ya test.
 
katika hali ya kawaida (test hazija expire, zimetumiwa inavopaswa) mtu akipima na kuonekana negative (kama ana mwaka haja ji "expose" kwa njia ya ngono, transfusion au njia zingine) basi chances are high hana ukimwi.
Ila kwa yule anae onekana positive, kuna uwezekano awe negative kwa sababu mbali mbali, hivo anahitaji kupima tena kwa kubadilisha aina ya test.

bora wewe umemjibu jamaa
 
tiger,kisheria rapid test inapoonesha mtu yuko negative uwezekano upo mdogo kuwa ni kweli yuko negative. ila ikionesha kuwa positive,kipimo halali kinaitwa ELISA inabidi kitumike ili ku-rule out chance ya kutokuwepo kwa hiv.

Hii ni kwa sababu alizotaja hapo juu RR,that rapid test kama haikutunzwa vizuri (nt kept under direct sunlight, joto na unyevu) ama kuharibika inaweza kuleta majibu ya uongo.

Na ukiangalia gharama ya kumuambia mtu kuwa na ukimwi wakati hana ni kubwa zaidi.muhimu kupima kila baada ya miezi 3, kwa mara 3 kujihakikishia.
 
Responce zitolewazo na wbc kunapokuwa hiv1/2 ni tofaut kabisa na unapokuwa na taifodi au maambukiz mengine, kwa hiyo hizo kit zimekuwa dizain kwa hiyo responce inayotokana na hiv tu.
 
Mleta mada, HIV hupimwa kwa njia kuu mbili.
1. kuangalia kinga (antibodies) ambayo mtu aliyepata maambukizo ataitengeneza kwa ajili ya kupambana na virusi na sio kupima wbc (chembe nyeupe za damu kama alivyoeleza mtoa mada) - WBC huwa zinapungua kwa mtu mwenye virusi vya ukimwi kwa kuwa virusi hushambulia chembe nyeupe zenye CD4 marker- lakini WBCs hazitumiki kwa ajili ya kuangalia kama mtu ana maambukizi ya HIV kwa sababu kuna sababu nyingi ambazo husababisha upungufu wa WBC zaidi ya HIV).
2. njia ya pili ni kuchunguza kirusi chenyewe au sehemu fulani ya kirusi hicho. (antigenic detection of HIV).

1. Njia za kupima antibodies
Ziko za aina mbili

a) zile za haraka (rapid or point of care HIV tests),
Hizi hufanywa haraka na client hupata majibu yake ndani ya dakika chache, na hizi hufanywa hapo hapo yaani ofisini kwa mtoa huduma. Tanzania tunatumia njia tatu kwa sasa za haraka ambazo ni determine, Bioline na Uni-Gold. vipimo hivi vya haraka vinauwezo mkubwa wa kupima antibodies (kinga) dhidi ya hivyo virusi na hivyo kugundua kama mtu ameambukizwa au la. Hata hivyo false positive na negative results pia zipo. Kwa hiyo ili kumpa mtu majibu ya uhakika unatakiwa utumie njia mbili hizi za haraka kabla ya kumpa mtu majibu, yaani ukifanya determine ikawa positive na bioline positive then huyu mtu ni positive, lakini mojawapo ikiwa negative utatakiwa ufanye ya tatu, labda utatumia unigold, ikiwa negative then majibu ni negative, ikiwa positive then majibu ni poitive. Kutumia njia mbili kunaondoa kumpa mtu majibu ambayo ni false either positive au negative. Kwa sababu ya gharama utakuta watu wanatumia njia moja na kutoa majibu but standard is to have two positive results from two different testing methods.

b) Kama njia za haraka zina utata, then utatumia njia ya kupima antibodies lakini hii huchukua muda na sio rapid, njia hizi zaweza kufanywa kwa kutumia ELISA for HIV au western Blot. Njia hizi nazo huangalia kinga inayotengenezwa na mwili. Hizi mara zote hufanywa maabara na sio ofisini kama zile za haraka.

Njia zote mbili za kupima antibodies (yaani ile ya haraka - rapid- na ile ya isiyo rapid - b juu) zinaweza zikaonyesha mtu yuko negative hata kama ana virusi na hasa wakati yuko kwenye window period (kile kipindi cha seroconversion ambacho huchukua wiki tatu mpaka miezi sita. kipindi hiki kinga hajijatengezwa au hazijawa katika kiwango ambacho zinaweza kugunduliwa na vipimo hivi vya antibodies.

2. Kuchunguza virusi vyenyewe.
Hii hufanywa kwa watoto wadogo wa chini ya miezi 18 au wale watu ambao wako kwenye window period.
Kwa watoto wadogo chini ya miezi 18 ni vigumu kutofautisha antibodies kama ni za mama au za mtoto, kwa kuwa mtoto huwa anazaliwa akiwa na hizo antibodies alizorithi kutoka kwa mama. kwa hivyo ili kugundua kama mtoto huyu ameambukizwa virusi inabidi sasa utumie njia ya kupima virusi vyenyewe au sehemu fulani ya hivyo virusi. Kinachopimwa yaweza kuwa ni protein katika kirusi kama protein inayoitwa p24 ambayo iko kwenye gamba la nje la kirusi. Pia upimaji wa vinasaba vya kirusi (genetic materials) pia huweza kufanya katika kugundua HIV. upimaji wa njia hii hufanywa mapema zaidi hata kabla mwili haujatengeza kinga, kwa hiyo njia hii huwezesha kugundua virusi hata kabla mwili haujatengeza hizo antibodies (kinga). Njia hizi ni ghali na hazifanywi routinely.
 
Back
Top Bottom